KERO Kivuko cha Busisi- Kigongo hakina ferry zote ni mbovu. Wananchi wanataabika. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza ingilia kati suala hili

KERO Kivuko cha Busisi- Kigongo hakina ferry zote ni mbovu. Wananchi wanataabika. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza ingilia kati suala hili

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Sawa wanakuja wenyewe
Hali ni mbaya sana. Kuna watu wenye wagonjwa ng'ambo ya pili wameshindwa kuwavusha wawahi hospitalini Bugando. Kuna wenye watoto wachanga nk.
 
Tayari wameanza kuharibu mamboz.. Maendeleo yavurugike

Duh.. Watu wamechoka kazi zao..
 
Duuh kwanii lile daraja bado tu halijakamilika
Taarifa iliyotolewa juzi ni kuwa linafunguliwa Feb 2025. Almost limekamilika. Kinachotakiwa Mkuu wa Mkoa aje site.
 
Hizi ni habari za muda huu. Tunaomba Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mh Ntanda uingilie kati. Wasafiri wanataabika sana.
Pale kuna daraja dogo la muda ambalo linapitika na liko imara. Mkuu wa mkoa aruhusu daraja hilo litumike kwa uangalifu mkubwa
 
Ni bahati mbaya tu watu wa kule sio watu wa kulalamika sana; vivuko vya pale Busisi sio reliable kabisa, ni mara nyingi tu watu hasa wenye gari ndogo kukaa pale kwa zaidi ya saa 6 wakisubiri kuvuka upande wa pili, hasa siku za weekend, narudia, ni mara nyingi tu. Huwaoni viongozi wakifika mara kwa mara pale cause wakazi wa huko ni wapole, sipati picha siku wakiamua kuwalazimisha watu watoke ma ofisini, sijui. Enzi za Magufuli, plan ya kumaliza daraja ilikua lini kweli? Deadline I think imepita siku nyingi sana, juzi walisema February 2025, sina hakika kama itakua. Kinacho kwamisha nina hakika sio mkandarasi, wana siasa wa ccm wanajulikana. Kwa wasiofahamu kivuko hicho, ndio kivuko kinacho unganisha mikoa ya Geita, Kigoma, Kagera na mkoa wa Mwanza; again ndio kivuko kinacho unganisha mkoa wa Mwanza na Burundi, Rwanda, Uganda na Congo ya upande wa Kivu, Bukavu. Ni kivuko muhimu kinacho liingizia pesa nyingi sana taifa; huaga sijui hasa KPI za mawaziri hasa wa ujenzi na fedha huaga ni zipi!? Poor us, RIP JPM
Kama inashindikana, kwanini serikali isiweke lami barabara ya Sengerema to Kamanga? Watu wapitie kivuko cha mtu binafsi badala ya hicho cha serikali, cha serikali ni ukweli ulio dhahiri kabisa kwamba serikali haina uwezo wa kufanya biashara, period
 
Darajani wanapita wenye connection zao tu
 
Pale kuna daraja dogo la muda ambalo linapitika na liko imara. Mkuu wa mkoa aruhusu daraja hilo litumike kwa uangalifu mkubwa
Ametusikia. Amesharuhusu, tunavuka sasa. Abarikiwe kwa vyote.
 
Back
Top Bottom