Ni bahati mbaya tu watu wa kule sio watu wa kulalamika sana; vivuko vya pale Busisi sio reliable kabisa, ni mara nyingi tu watu hasa wenye gari ndogo kukaa pale kwa zaidi ya saa 6 wakisubiri kuvuka upande wa pili, hasa siku za weekend, narudia, ni mara nyingi tu. Huwaoni viongozi wakifika mara kwa mara pale cause wakazi wa huko ni wapole, sipati picha siku wakiamua kuwalazimisha watu watoke ma ofisini, sijui. Enzi za Magufuli, plan ya kumaliza daraja ilikua lini kweli? Deadline I think imepita siku nyingi sana, juzi walisema February 2025, sina hakika kama itakua. Kinacho kwamisha nina hakika sio mkandarasi, wana siasa wa ccm wanajulikana. Kwa wasiofahamu kivuko hicho, ndio kivuko kinacho unganisha mikoa ya Geita, Kigoma, Kagera na mkoa wa Mwanza; again ndio kivuko kinacho unganisha mkoa wa Mwanza na Burundi, Rwanda, Uganda na Congo ya upande wa Kivu, Bukavu. Ni kivuko muhimu kinacho liingizia pesa nyingi sana taifa; huaga sijui hasa KPI za mawaziri hasa wa ujenzi na fedha huaga ni zipi!? Poor us, RIP JPM
Kama inashindikana, kwanini serikali isiweke lami barabara ya Sengerema to Kamanga? Watu wapitie kivuko cha mtu binafsi badala ya hicho cha serikali, cha serikali ni ukweli ulio dhahiri kabisa kwamba serikali haina uwezo wa kufanya biashara, period