KERO Kivuko cha watembea kwa miguu 🚸 eneo la Njia panda ya chuo UDSM

KERO Kivuko cha watembea kwa miguu 🚸 eneo la Njia panda ya chuo UDSM

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

Salum Fumo

Member
Joined
Jan 3, 2018
Posts
14
Reaction score
4
Kabla ya kijazi interchange eneo hili lilikuwa linaruhusu wananchi (wanafunzi/wakazi/watembezi na sisi wazururaji) kuvuka kutoka upande mmoja hadi mwingine bila shida. Ila baada ya kuwekwa flyover uwezo huo umeondoshwa na option iliyokuwepo kwa watu hap ni ya hatari sana.

IMG-20241019-WA0005.jpg

Nafahamu kuondoa wavu uliowekwa na kuruhusu wananchi kuvuka ni hatari kwasababu barabara zote (inayoshuka na inayopandisha) huwa vyombo vinavyopita vinatembea kasi sana. Lakini mbadala tunaotumia wananchi kwasasa ni hatarishi zaidi.

Siwezi sema mengi ila hapa kunahitaji kivuko cha juu kama utaona hakuna umuhimu wewe nenda katoke upande wa mawasiliano vuka hapo kwenda upande wa chuo.

(Tusisubiri mpaka watu wafe hapo ndo tuje kuaddress hatari iliyopo. Hata tukiwekewa daraja la juu kama lile la Buguruni litasaidia sana.)

IMG-20241019-WA0003.jpg
 
Siwezi sema mengi ila hapa kunahitaji kivuko cha juu kama utaona hakuna umuhimu wewe nenda katoke upande wa mawasiliano vuka hapo kwenda upande wa chuo.

Baada ya hilo daraja usawa wa barabara ya kwenda Simu2000 si kuna kivuko cha zebra na kina taa kabisa?
 
Wao pia wanaweza kuzunguka pale mataa kwa usalama wao. Inabidi muwaelekeze na muwe mfano mzuri.
Uhalisia haupo hivyo mkuu. Kwanza kuzunguka ambako kivuko kipo unaposteza muda mwingi. Muda ambao kama ilikuwa ni unatoka upande mmoja kwenda upate wa pili mfano kupata huduma ya Stationery chap now inabidi utumia dakika 20+ nzimq kuzunguka huko unakosema. Yaani ni impractical. Unasema sahihi ila ni impractical, labda kwa kuwa muda wetu hatuuthamini that's why hata miundombinu inawekwa kutupotezea muda. Ukisema hapo hakuna umuhimu wa kivuko kaka basi hata pale mbezi magufuli hakukuwa na haja ya kivuko.

Halafu sio lazima kuweka kivuko cha juu kaka. Wangeondoa wavu sehemu ndogo watu wakavuka kawaida kama ilivyo upande wa riverside. Hakuna hii miwavu.
 
Kipo aisee tena kila siku naacha pale watu wanavuka na juzi kati askari alinipiga cheti pale nilipita na taa nyekundu
Malipo yamepokelewa kwenda POLISI TANZANIA
Ankara: 9910842559309
Kiasi: 30000 TZS
Risiti: 924274280241412
2024-09-30T14:02:14
Kupitia: GWX101248403503
 
Back
Top Bottom