Kivuko.com

Kichuguu

Platinum Member
Joined
Oct 11, 2006
Posts
17,048
Reaction score
22,790
Nimeona Tangazo la Kivuko.com pale kwa michuzi nikafurahishwa sana nikidhani kuwa hiyo inaweza kuwa njia bora ya watanzania kuachana na bidhaa feki wanazoletewa kutoka China kila kukicha. Kama kuna mtu aliyewahi kununua hapo Kivuko.com ninaomba anisaidie experience yake kabla sijajiingiza kichwa kichwa.

Jambo moja limenisitua kidogo ni kuwa bei zake ziko inflated sana, kwa mfano bei ya TV aina ya Panasonic - VIERA / 50" Class / 1080p / 600Hz / Plasma HDTV, wao wanaiuza katika dolari za kimarekani 1883 kama invyoonkena hapa chini kabla ya kodi na usafiri, lakini TV hiyo hiyo ninaweza kuipata Best Buy kwa dolari za kimarekani 999.99 kabla ya kodi na usafiri kama inavyoonekana hapa chini.










Inawezekana tofauti hizi za bei zikatokana na factors mbalimbali, lakini nadhani tofauti ya karibu mara mbili ni kubwa mno; je mliowahi kuitumia service hii mna uzoefu wa namna gani?
 
Duh bei ni almost double ile ya Best Buy...huu ni ulanguzi wa hali ya juu. Nawahurumia Watanzania
 
Duh bei ni almost double ile ya Best Buy...huu ni ulanguzi wa hali ya juu. Nawahurumia Watanzania

lakini ni afadhali kuliko kununua feki za kutoka China, labda jamaa wakawa wanauza "PAMASOMIC VEIRA" from China badala ya Panasonic Viera from Japan! Usilete mchezo katika dunia hii ya mchina.
 
lakini ni afadhali kuliko kununua feki za kutoka China, labda jamaa wakawa wanauza "PAMASOMIC VEIRA" from China badala ya Panasonic Viera from Japan! Usilete mchezo katika dunia hii ya mchina.

Halafu wahindi wa Kariakoo wanavyowaingiza watu mjini kwa kuwaambia.........hii TV "jina la ajabu" haina tofauti na SONY/JVC/PANASONIC/HITACHI.......kwani aliyetenegeneza HITACHI ndio aliyetengeneza......."hiyo hiyo Jina la ajabu"........halafu utakuta bei pia ni ya ajabu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…