Kivuli cha Kwame Nkrumah katika TANU

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
KIVULI CHA KWAME NKRUMAH KATIKA TANU

Hayo maneno hapo chini yaliyoandikwa na Kwame Nkrumah nimeyaona hapa jamvini na yamenikumbusha ushawishi wake kwa wanasiasa wa Tanganyika wakati wa kudai uhuru.

Hebu kwanza msome Nkrumah kisha ndiyo tusonge mbele:

In 1934, Kwame Nkrumah applied to the Lincoln University for an admission to study. One year past and he had not received an offer or a response.

He then wrote an emergency letter to the Dean of Students at the University in 1935 reminding him of his request for an admission to study at the university.

The university wrote back to him asking him to write a brief story of his life and his reasons for wanting to study at the school.

The following is the summary of what Nkrumah wrote to the university:

"I neither know where to begin nor where to end because I feel the story of my life has
not been one of achievements.

Furthermore, I have not been anxious to tell people of what may have been accomplished by me.

In truth, the burden of my life can be summarized into a single line in "The Memoriam," quoted by Cecil Rhodes; "somuch to do, so little done ..."

In all things, I have held myself to but one ambition and that is to make necessary arrangements to continue my education in a university in the United States ofAmerica, that I may be better prepared to serve my fellowman ...."

Tomorrow will be exactly 64 year when Nkrumah won independence for Ghana 🇬🇭.

It is time for us all to overcome Neo-Colonialism and win true liberation for the entire continent of African.

Katiba ya TANU ilinakiliwa neno kwa neno kutoka katiba ya Convention Peoples' Party (CPP) ya Ghana.

TANU ilifanya hivi kwa kukwepa vizingiti vya Waingereza endapo wangekuja na katiba nyingine.

Kwa kuwa hii katiba ya CPP ilikuwa Waingereza wameshaikubali Ghana na kuipitisha wasingeweza kuikataa Tanganyika.

Picha hiyo hapo chini inamuonyesha Chief Thomas Marealle na mkewe wakiwa uwanja wa ndege wa Accra walipokwenda kuhudhuria sherehe za uhuru wa Ghana mwaka wa 1957.

 
Kumbe Thomas Marealle alianza kufahamiana na Kwame kabla ya wakina Nyerere.
Malcom,
Abdul Sykes alifahamiana na Kenyatta 1950 kabla ya Nyerere.

Ally Sykes alifahamiana na Kenneth Kaunda 1953 kabla ya Nyerere.

Abbas Sykes amesoma darasa moja King's College, Budo na Kabaka Edward Mutesa aliyekuja kuwa Rais wa kwanza wa Uganda.

Hizi zote ni historia za kusisimua sana.

Nimezieleza kwa kirefu katika kitabu cha Abdul Sykes.
 
Ni kweli Marealle alienda UN kudai uhuru kabla ya Nyerere?
 
MALCOM LUMUMBA kauliza ''Kumbe Thomas Marealle alianza kufahamiana na Kwame kabla ya wakina Nyerere''

Hapa subject ni Nyerere and Marealle. Hayo mengine yanakujaje?
 
MALCOM LUMUMBA kauliza ''Kumbe Thomas Marealle alianza kufahamiana na Kwame kabla ya wakina Nyerere''

Hapa subject ni Nyerere and Marealle. Hayo mengine yanakujaje?
Nguruvi3,
Haya mengine yamekuja kwa muktadha huu huu wa muulizaji kushangaa kuwa Chief Thomas Marealle alimjua kwanza Nkrumah kabla Nkrumah hajafahamiana na Nyerere.

Nikaona si vibaya nikawaeleza viongozi wengi ambao walijuana na wapigania uhuru wengine mapema sana.

Hukupendezewa mimi kuongeza taarifa hii ya Kenyatta, Kaunda na Kabaka ambayo naamini si wengi wanaijua?

Ikiwa nimekuudhi kwa kuandika haya basi niwie radhi ndugu yangu.
 
Ni kweli Marealle alienda UN kudai uhuru kabla ya Nyerere?
Laki...
Hili sina ujuzi nalo.
Wewe umesikia wapi?

Ufahamu wangu mimi kuhusu Tanganyika kufanya mawasiliano na UNO kwa kusudi la kudai uhuru nimesoma katika Nyaraza za Sykes (Annual Report of the Secretary of Tanganyika African Association, 7 January, 1951).

Earle Seaton aliishauri TAA Political Subcommittee kuanza mazungumzo na UNO kuhusu hali ya Tanganyika kama nchi chini ya udhamini wake.

Baada ya kuundwa kwa TANU ndiyo Mwalimu Nyerere akaenda UNO February, 1955 kama msemji wa TANU chama cha kupigania uhuru wa Tanganyika.

Sasa Marealle atakwenda UNO kuwakilisha chama kipi?
 
Haya mengine yamekuja kwa muktadha huu huu wa muulizaji kushangaa kuwa Chief Thomas Marealle alimjua kwanza Nkrumah kabla Nkrumah hajafahamiana na Nyerere.
Sawa hakuna shida katika hilo
Nikaona si vibaya nikawaeleza viongozi wengi ambao walijuana na wapigania uhuru wengine mapema sana.
Familia ya Sykes ukimaanisha. Sidhani kama Nyerere alitakiwa kujua kila mtu.
Hukupendezewa mimi kuongeza taarifa hii ya Kenyatta, Kaunda na Kabaka ambayo naamini si wengi wanaijua?
Hapana, ni katika kuweka sawa maandishi. Hoja hapo ni kumzodoa Nyerere na hili hukuanza leo. Ulichotaka ni kuumbia umma Familia pendwa ilikuwa juu sana dhidi ya mvaa kaptula Julius.
Ikiwa nimekuudhi kwa kuandika haya basi niwie radhi ndugu yangu.
Hapana hujaniudhi kabisa Mohamed, umekirihisha kwa sarcasm, innuendos etc
Kuna nyakati nakuonea huruma sana jinsi Nyerere anavyoitesa nafsi yako

Huwa najiuliza, hate dhidi ya Nyerere inakujenga au kukusaidia nini ?

Kitu kimoja hutaweza kukifuta katika historia, Nyerere ni Rais wa kwanza wa Tanganyika huru
 
Shukraani mno mkuu,but muda mwingine ni vema to let it go, unatoa mada nzuri tu na sisi wasomaji/wachangiaji tunatakiwa tuisome ili kuielewa sio kuuliza maswali!,unakuta mchangiaji bila hata kujaribu kuisoma mada ili aielewe, tayari ameshakimbilia kuuliza swali ambalo nalo linaonyesha ni jinsi gani alivyo, it's time now historia ya nchi yetu na Africa hapa iandikwe kwa ukweli(facts)sio politics, kuna mengi kuhusu hasa nini kilitokea hapa nchini, pale Angola (Mr.Savimbi alikua mzalendo au msaliti?),Zimbabwe je wapiganaji wa uhuru walipigana clean war or walifanya war crimes?even SA kuna mengi watu hawajui ukweli wake, tusiwalaumu foreigners wanapotuandikia historia wakati sisi wenyewe tuna uchoyo wa ukweli.
 
Nguruvi3,
Wala mimi siwezi kumsema vibaya Nyerere kwa kuwa hakuwajua wanasiasa wa Kenya.

Mwaka wa 1950 ndiyo mwaka Abdul Sykes aliingia madarakani kama Secretary wa TAA, Dr. Vedasto Kyaruzi akiwa President.

1950 Nyerere alikuwa bado hajachukua uongozi wa TAA hadi April 1953.

Vipi mimi nishangazwe kuwa kwa nini hakufahamiana na Kenyatta?

Hayo maneno mengine unayosema ''kuzodoa,'' ''kaptula,'' mimi sijapata kuyasema popote.

Siwezi kuwa mjinga na kukosa adabu kwa kiasi hicho.

Baba yangu akivaa kaptula akienda kazini.

Abdul Sykes akivaa kaptula kama uniform ya Market Master.

Kipi cha kunishangaza mimi?

Unionee huruma mimi kwa kuandika historia ya TANU ambayo ndiyo historia ya wazee wangu katika kupigania uhuru wa Tanganyika?

Mimi si kuwa nakuonea huruma wewe bali nawasikitikia wengine zaidi walioandika historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika bila ya umakini unaostahili, waandishi kama Kimambo na Temu (1969), Ulotu (1971) na Chuo Cha CCM Kivukoni (1981).

Hujiuliza nikasema hivi hawa hawakujua kuwa hao waliowafuta katika historia wana watoto wao ambao iko siku watakuja kuandika historia za wazee wao?

Nadhani unaeteseka ni wewe si mimi.

Kitu kama kinakutesa unakiacha.

Wewe ndiyo uaneteseka kwa kuwa unaumia kila ukisoma historia ya kweli ya Nyerere na TANU na ndiyo maana kila ukiona nimeandika utakuja.

Wala mimi sina chuki na Julius Nyerere.

Nimehariri kitabu cha Julius Nyerere, ''Tanzania The Story of Julius Nyerere,'' na kukitafutia publisher.

Kazi hii nilipewa na Jim Bailey mmiliki wa gazeti la Drum na aliyeniunganisha na Jim Bailey ni Ally Sykes.

Nimemwandika Julius Nyerere katika kitabu cha Abdul Sykes kama alivyostahili kuandikwa chanzo changu kikiwa Nyaraka za Sykes.

Waadishi wa ''Nyerere Biography,'' walinihoji kuhusu Nyerere na wakanisifia kuwa katika watu wanaoifahamu historia ya Nyerere mimi ni mmoja wapo na hawakuishia hapo wakasifia Maktaba yangu kuwa ni kati ya maktaba tatu bora - ya Salim Ahmed Salim, Brig. Hashim Mbita na yangu.

Haya yameandikwa katika kitabu hiki cha Mwalimu Nyerere.

Kuniambia kuwa siwezi kumfuta Julius Nyerere hili wala sihitaji wewe unifahamishe ni jambo liko wazi kabisa.

Ila mimi nitakuambia kitu.

Mazungumzo ya kumwingiza Nyerere ndani ya uongozi wa TAA yalifanyika nyumbani kwa Hamza Mwapachu Nansio akiwapo Abdul Sykes na Ali Mwinyi Tambwe.

Abdul Sykes alitamani nafasi ile wampe Chief David Kidaha Makwaia lakini uamuzi ulipopita kuwa nafasi ile wampe Nyerere, Abdul hakusita na alimuunga mkono kwa hali na mali yake.

Kisa hiki wengi hapa mnakifahamu kwa kuwa nimekieleza mara kadhaa.

Hayo mengine naona hayana maana sana kwangu kuyasemea.

 
Hayo maneno mengine unayosema ''kuzodoa,'' ''kaptula,'' mimi sijapata kuyasema popote.
Siwezi kuwa mjinga na kukosa adabu kwa kiasi hicho.
Mohamed uwe na kumbu kumbu!
Unionee huruma mimi kwa kuandika historia ya TANU ambayo ndiyo historia ya wazee wangu katika kupigania uhuru wa Tanganyika?
Hakuna tatizo kuandika historia ya wazee wako !
Nadhani unaeteseka ni wewe si mimi.Kitu kama kinakutesa unakiacha.
Nateseka kuona jinsi jina la Nyerere linavyokutesa! kwakweli inanitesa, ni kwanini uteseke hivyo wakati unajua historia haiandikwi inajidhihiri.
Ile ya Rais wa Tanganyika imeshajidhihiri sijui kama itafutika. Ni Nyerere
Wewe ndiyo uaneteseka kwa kuwa unaumia kila ukisoma historia ya kweli ya Nyerere na TANU na ndiyo maana kila ukiona nimeandika utakuja.
Hapa kuna tatizo, historia ya Wazee wako haina shida.

Historia ya kweli kuna shida , ukweli kwa mujibu wako na mujibu wako hauwezi kuwa ukweli kwa kila mtu.

Hapa nateseka kidogo hasa unapowachanganyia vijana mchele na mapumba halafu kuwaambia ndio ukweli, hapana. Ukiawaambi ni ukweli wa wazee wako hakuna shida. Wazee wako si Tanganyika.

Ninaposema pumba usikirihike nina maana fyongo kama ile ya Abdul kutohutubia popote nje ya Mwembe Togwa lakini anatakiwa akuzwe kama Rais wa Tanganyika! na historia ya Familia iwe ya Tanganyika! lahaula sheikh! tusitiri , tunajitahidi kukusitiri
Ukasema walikataa baadhi ya mambo uliyowashauri wakaandika yao!
Kuniambia kuwa siwezi kumfuta Julius Nyerere hili wala sihitaji wewe unifahamishe ni jambo liko wazi kabisa.
Basi kama unakubali hilo hakuna tatizo
 
https://www.facebook.com/
Nguruvi,
Mimi sikejeli wala kukebehi.

Nakueleza historia ya TANU kama ukweli wake ulivyokuwa.

Na nimenyanyua kalamu baada ya kuona hizo historia zilizoandikwa zimepotoshwa.

Nani alikuwa anaijua historia ya African Association, TAA hadi kuundwa kwa TANU kwa kiwango nilichoeleza mimi?

Kadi ya TANU No. 1 Territorial President Julius Kambarage Nyerere, kadi No. 2 Ally Kleist Sykes, kadi No. 3 Abdulwahid Kleist Sykes, kadi No. 4 Waziri Dossa Aziz, kadi No. 5 Denis Phombeah (Mnyasa) Kadi No. 6 Dome Okochi Budohi (Mkenya).

Nani alikuwa anaijua historia hii?

Katika hao wanachama wa TANU sita ambae sikupata kuwajua ni wawili - Nyerere na Phombeah.

Hawa nimewasoma katika Nyaraka za Sykes.

Lakini hao wote sita nimeeleza historia zao katika kitabu cha Abdul Sykes.

Kitabu hiki kimevunja rekodi tunakwenda toleo la tano Kiswahili na Kiingereza.

Kwa nini kitabu hiki kimependwa kiasi hiki?

Sababu ni kuwa hii ndiyo historia ya kweli ya TANU na uhuru wa Tanganyika.

Nikejeli na "Mwembe Togwa," na maneno yote upendayo mimi sirejeshi kejeli narejesha maneno ya kweli katika historia ya kupigania uhuru wa Tanganyika kwa ushahidi wa picha na nyaraka.

Ndiyo maana hapa nimeingia na jina langu halisi.

Wewe unaweza ukatukana, ukakejeli na kukebehi.

Anakujua nani?
Mimi niko hapa kwa picha na sauti.

Hakuna asiyenifahamu.

Mimi nimebeba dhima ya elimu yangu na heshima ya walimu wangu na heshima ya mama yangu aliyenifunza adabu.

Sithubutu kukurejeshea ufedhuli.
 
Marealle alienda kudai Uhuru wa Wachagga, hakuwa na Chama.
 
Mzee,
Nimepata shauku, andiko la Nguruvi linatakiwa kudhibitishwa.
Kwa ufahamo wako, ni kweli kuwa Ally Sykes hakuwai toa hutuba yoyote ya kudai uhuru nje ya Mwembe Togwa au nje ya Dar esam Salaam?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…