Kivuli cha Kwame Nkrumah katika TANU

Kivuli cha Kwame Nkrumah katika TANU

Kwani Thomas ni Ustadhi ?.
Ngongo,
Niliacha kukujibu nikawa nikikuona napita wima naamini unaelewa sababu ya mimi kukufanyia hivyo.

Lakini nitakujibu huenda hii ikawa fursa njema kwetu ya kuwa na mijadala yenye staha na heshima nikiamini kuwa wewe ni mtu mwema na kwa kipindi ambacho umenisoma hapa umenitambua kuwa mimi si mtu wakirushiana matusi na yeyyote awaye yule.

Mimi napenda mijadala yenye adabu.

Nianze kwa kukujulisheni ndugu zangu kuwa hapa mimi sipo kubishana nipo hapa kusomesha historia ya jamii ambayo mimi nimetoka.

Jamii ya watu wa Dar es Salaam ambao tuna historia yetu ambayo kwa bahati mbaya haikupatwa kuandikwa na kutambulika.

Unaweza ukaniuliza swali na mimi katika jibu langu nitajibu swali lako na kuongeza na mengine nikiamini kuwa muulizaji atanufaika na elimu hiyo ambayo hana.

Swali la Mangi Mkuu Thomas Marealle kufahamiana na Kwame Nkrumah.

Swali hilo linatokana na post yangu ya Marealle pamoja na picha yake na mkewe wakiwa uwanja wa ndege Accra Ghana.

Katika kujibu swali kuhusu kufahamiana kwa Nkrumah na Marealle mimi nikaenda mbele zaidi kumnufaisha muulizaji kuwa Abdul Sykes alifahamiana na Kenyatta kabla ya Nyerere.

Nikaeleza pia Kenneth Kaunda alifahamiana na Aly Sykes kabla ya Nyerere.

Abbas Sykes akiwa mtoto mdogo wa shule ya msingi alipelekwa na baba yake kusoma King's College Budo na alisoma darasa moja na Edward Mutesa aliyekuja kuwa Kabaka wa Buganda na Rais wa Uganda.

Baadhi ya watu wamekasirika kwa nini nimeeleza historia hii.
Wao wameona kuwa nia yangu haikuwa njema.

Kwengine tofauti na hapa nyumbani ni kuwa ninapoeleza historia mfano wa hii maswali ninayopata yanakuwa kama hivi.

Ilikuwaje Abdul Sykes akafahamiana na Jomo Kenyatta?

Hapo sasa mimi naeleza historia ya Abdul Sykes akiwa kiongozi wa TAA na nini ilisababisha kufanyika mkutano Nairobi kati yake na Kenyatta mwaka wa 1950.

Na kufahamiana kati ya Ally Sykes na Kenneth Kaunda maswali yanakuja katika mtindo kama huo wa Abdul Sykes na Jomo Kenyatta na mhadhara unanoga sana.

Ajabu hapa watu wanakasirishwa na historia hii na hawataki kuisikia.

Sasa inapokuja Abbas Sykes kusoma King's College maswali yanakuwa ya kupendeza sana kwani huniuliza huyu baba yake alikuwa nani hadi ampeleke mtoto wake kusoma King's College, Uganda kwani Tanganyika hakukuwa na shule bora kwa kiwango cha Budo?

Hapo ndipo nawaeleza Kleist Sykes alikuwa nani katika Tanganyika ya kikoloni.

Mwisho wataniuliza mbona historia hii haifahamiki?

Sasa elewa kuwa hawa wanaoniuliza maswali haya ni watu waliobobea katika historia ya Afrika na wanamjua Mwalimu Nyerere vizuri wanataka kujua uhusiano wa hawa ndugu watatu na Julius Nyerere.

Nawaeleza.

Nilifanya mhadhara Zentrum Moderner Orient (ZMO) Berlin.
Niliwatia simanzi wasikilizaji wangu wakaingia huzuni kubwa sana.

Nilikuja kufahamishwa baadae kuwa waliohudhuria mazungumzo yale waliingiwa na simanzi kwa kuwa wahadhiri wengi wamepata kupita ZMO na historia zao kuhusu Tanganyika haifanani na yangu hata kidogo kiasi wakahisi wamedanganyika kuamini kitu kilichokuwa na kasoro kubwa sana.

Katika waliokuja kunisikiliza alikuwa ofisa kutoka Ubalozi wa Tanzania.

Mhadhara huu upo katika maktaba ya ZMO Berlin: ''Tanzania: A Nation Without Heroes.''

Labda nikugusie kuhusu suala la ''Ustadhi.''

Mimi sikujaaliwa kusoma elimu ya dini ya Kiislam kwa kiwango cha kuweza kuitwa ''ustadh,'' yaani mwalimu.

Ingawa ningependa kuwa ustadh kama vile ninavyopenda kama ningekuwa na sifa nikaitwa Dr. (Ph. D).

Kwa hiyo mimi si ustadh kama wewe ulivyo kuwa si shamasi au mchungaji, mlokole nk.

Mimi elimu yangu yote ni sekula na kiwango cha wastani cha dini yangu.
Picha hiyo hapo chini nikiwa ofisini kwangu Berlin, ZMO:

1647353473251.png


 
Kolola,
"Marealle."

Hapana sikudakia.
Hii ni katika kuieleza historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika.

Mangi Mkuu Chief Thomas Marealle alikuwa rafiki mkubwa wa Abdul Sykes na kila akifika Dar es Salaam ilikuwa lazima amtembelee Abdul nyumbani kwake.

Na machifu wote wakifanya hivi.

Nimesoma barua ambazo Thomas Marealle alikuwa akiandikiana na Ally Sykes wakati wa kupigania uhuru wa Tanganyika.

Hizi barua zinasisimua sana.
Huwa najiuliza sana kwa nini Abdul Sykess alimpindua baba yake kwenye uongozi wa TAA, tena kwa kumfanyia vurugu kubwa,,.. Kwa nini Abdul Sykess hakutumia njia ya busara ya mazungumzo?
 
Huwa najiuliza sana kwa nini Abdul Sykess alimpindua baba yake kwenye uongozi wa TAA, tena kwa kumfanyia vurugu kubwa,,.. Kwa nini Abdul Sykess hakutumia njia ya busara ya mazungumzo?
Laki...
Mkasa mzima wa mapinduzi yale ya 1950 nimeeleza katika kitabu cha Abdul Sykes.
Mwalimu Thomas Plantan si kuwa alikuwa anapingwa na Abdul Sykes peke yake.

Schneider Plantan ambae ni mdogo wake pia alikuwa anaupinga uongozi wa TAA uliokuwapo.
Historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika una mambo mengi sana ya kusisimua.
 
Back
Top Bottom