Geza Ulole
JF-Expert Member
- Oct 31, 2009
- 65,136
- 91,917
Na si wakina wavaa suruali Sykes!Sawa hakuna shida katika hilo
Familia ya Sykes ukimaanisha. Sidhani kama Nyerere alitakiwa kujua kila mtu.
Hapana, ni katika kuweka sawa maandishi. Hoja hapo ni kumzodoa Nyerere na hili hukuanza leo. Ulichotaka ni kuumbia umma Familia pendwa ilikuwa juu sana dhidi ya mvaa kaptula Julius.
Hapana hujaniudhi kabisa Mohamed, umekirihisha kwa sarcasm, innuendos etc
Kuna nyakati nakuonea huruma sana jinsi Nyerere anavyoitesa nafsi yako
Huwa najiuliza, hate dhidi ya Nyerere inakujenga au kukusaidia nini ?
Kitu kimoja hutaweza kukifuta katika historia, Nyerere ni Rais wa kwanza wa Tanganyika huru
sasa unataka kuwa-refunded mchango wa babako? Je katika wachangiaji woote wa TANU, mbona wengine wako kimya?James...
Nitakuondolea hiyo shida yako.
Hebu soma hii hapo chini:
''Kitabu kilikuwa kimetoka na siku hiyo nilikwenda nyumbani kwa Mama Daisy kumpa nakala yake ya kitabu.
Tulikuwa tumekaa kwenye varanda yake nyumba yake Barabara ya Ali Hassan Mwinyi iliyokuwa mkabala na Hellenic Club.
Alikipokea kitabu akawa anatazama picha ya mumewe kwenye jalada na akawa kimya kwa muda mrefu.
Bila shaka alikuwa anawaza maisha aliyoishi na baba yetu wakati wa kupigania uhuru wa Tanganyika katika miaka ya 1950.
Mama Daisy alikuwa shoga wa marehemu mama yangu Bi. Baya bint Mohamed na nyumba zao hazikuwa mbali kwani sisi tulikuwa Mtaa wa Kipata na si mbali na Mtaa wa Stanley.
Nyumba zao zilitenganishwa na Mtaa wa Kitchwele (sasa Uhuru Street).
Naamini kuwa ile mimi mtoto wa shoga yake kuwa ndiye niliyekuja kuandika kitabu cha Abdul Sykes, mtu ambae historia ilikuwa imemfuta bila shaka fikra hii ilikuwa ikizunguka katika kichwa chake.
''Mwanangu Mohamed, baba yako alijitolea sana katika kupigania uhuru wa Tanganyika,'' Mama Daisy alianza kusema.
''Alikuwa na sanduku akiweka fedha zake na kila TANU wakija hapa kutaka kile au hiki yeye alikuwa anaingia ndani analifungua lile sanduku anatoa fedha kuwapa alikuwa hawarudishi mikono mitupu.
Mimi nikawa namwambia, ''Bwana Abdul taratibu lakini hakunisikia, hakuacha kutoa fedha kwa ajili ya chama chake.
Bwana Abdul alikuwa mtu karimu sana.''
Bwana James,
Haikushagazi kuwa Abdul Sykes hayuko katika historia ya kupigania uhuru?
Hebu nipe jibu.
View attachment 2150672
Abdul Sykes na mkewe Mama Daisy Government House katika Garden Party 1950s
Geza...sasa unataka kuwa-refunded mchango wa babako? Je katika wachangiaji woote wa TANU, mbona wengine wako kimya?
Sikuwahi kuuliza hiloNimekueleza kuwa Cecil Matola kafariki 1933 kukufahamisha kuwa hakuishi hadi 1950 pale Abdul na Hamza Mwapachu walipompindua Thomas Plantan aliyekuwa President wa TAA na Clement Mohamed Mtamila Secretary.
Hapa sawa sawa, siyo kumtoa Cecil kiaina na kumwacha Kleist kama muasisi peke yakeUngejuaje kuwa Cecil Matola ndiye alikuwa rais muasisi kama Kleist Sykes asingeandika mswada wa kitabu cha maisha yake na kueleza vipi aliunda African Association na Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika?
Sawia!Waasisi wa AA ni hawa wafuatao: Cecil Matola, Kleist Sykes, Selemani Majisu, Mzee bin Sudi, Ibrahim Hamisi, Zibe Kidasi, Ali Said Mpima, Rawson Watt na Raikes Kusi.
Imekujaje hii!Kleist Sykes anaeleza kwa nini Waislam walikuwa wengi katika AA.
Anasema kanisa lilikuwa linawakataza waumini wao kujihusisha na siasa.
Lakini pia sikubali kubugizwa shudu!Naamini James Comey ataelewa tofauti baina yako na mimi.
Wewe unaandika kwa dhana.
Ni kweli hasa pale unapoulizwa kitu unajibu kingine, panachoshaNingeweza kukueleza mengi lakini nachelea kukuchosha na kuwachosha wasomaji wengine.
Nguruvi..Sikuwahi kuuliza hilo
Hapa sawa sawa, siyo kumtoa Cecil kiaina na kumwacha Kleist kama muasisi peke yake
Sawia!
Imekujaje hii!
Lakini pia sikubali kubugizwa shudu!
Ni kweli hasa pale unapoulizwa kitu unajibu kingine, panachosha
Haya mimi nilikuwa napita nikaona vema nikuamkue kidogo hapa barazani.
Safari hii nitalipa kahawa mimi, huwezi kununua kila siku!
Nakutakia kheri
Masalam
MS, sikutaka kujibu au kuuliza etcNguruvi..
Ikiwa nakuchosha acha kujibu si lazima unijibu.
Wako watu wengi hunisoma wakapita wima na hamsini zao
Nguruvi...MS, sikutaka kujibu au kuuliza etc
Kila ninaposoma jambo nikaona lina 'hila au namna' na wengi hawataelew najisikia '' guilty' kwamba naona kisicho sawa nakaa kimya. Hakuna kitu neutral, mathalani ninajua bandiko hili lina maana ya kusema '' Nyerere hakuandika katiba'' lakini limeandikwa kwa ufundi sana
Nina dhima ya kusema ninachojua. Kwamba aliyeandika katiba ya TANU ni Bwana Julius, Mwana wa Kambarage Burito Nyerere, mdogo wake Chief Wanzagi pale Butiama karibu na fort Ikoma.
Iwe kwamba Julius aliandika , ali copy &paste neno kwa neno, alikabidihiwa ilivyo kutoka popote, ukweli unabaki pale pale ! aliyeiandaa nyaraka hiyo ni Julius Nyerere
Laiti ingalikuwa si yeye, kuanzia 1929 Kleist Sykes hadi 1952 Abdul Sykes akiwa kiongozi hatukuwahi kuwa na katiba hata kurasa moja. Kama ipo tuonyeshe kutoka kwenye nyaraka za Abdul Sykes au Shajara za Kleist! kurasa moja tu!
Kwahiyo ujio wangu hakuwa kutafuta mnakasha, tumeshaongea sana.
Ujio wangu hapa ni 'kuwang'ata shikio' wasomaji lipo jambo hapo! katiba ni daraja anayelengwa kuzodolewa ni Julius mwana wa Mwitongo mtoto wa Bi Nyangeta
Baada ya haya, nikasema nikujulie hali na sasa naendelea na safari yangu
masalam
Kwani kuandika kitabu ni kitu cha ajabu?Nguruvi...
Amini upendacho lakini mimi nimetafiti maisha ya Abdul Sykes na nimeandika kitabu.
Kabla ya kitabu changu hamkuwa mnaijua mengi kuhusu historia AA, TAA na TANU wala mlikuwa hamjui mengi kuhusu Julius Nyerere mwenyewe.
Wala mlikuwa hamjui chochote kuhusu mchango wa Earle Seaton katika kuisaidia TAA kukabiliana na Waingereza.
Hamkuwahi hata kusikia Constitutional Development Committee wala hamkuwajua wajumbe wake walikuwa nani.
Wala hamkujua kuwa mmoja wa wajumbe hawa ambae jina lake hulioni ni Earle Seaton.
Wala hamkujua urafiki uliokuwako baina ya Earle Seaton na Abdul Sykes.
Mimi ndiye niliyeeleza haya yote na huku kuandika upya historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika ndiko kulipopelekea Mimi kuàlikwa kuzungumza Northwestern University, Evanston, Chicago kwa mwaliko wa Mkuu wa Idara ya Historia Prof. Jonathon Glassman.
Katika kunishukuru alisema kuwa kuna mengi hawakuyajua hadi niliponyanyua kalamu yangu kuandika historia ya Sykes.
Kwangu mimi hili si jambo dogo.
Leo Sykes yuko katika Dictionary of African Biography anasomwa na Dunia nzima.
Kwenye ukweli uongo hujitenga.
Lakini faraja kubwa nilipata kwa kumsikia Prof. Haroub Othman akinambia kitabu changu kimebadili kabisa "legacy" yaani urathi wa Nyerere na alimfahamisha Mwalimu uso kwa macho nyumbani kwake Msasani.
Yako mengi.
Haya yanatosha kwa sasa.
View attachment 2150979
Geza...Kwani kuandika kitabu ni kitu cha ajabu?
Geza...Na si wakina wavaa suruali Sykes!
si ulisema wakina Sykes na Baba yako walimfundisha kuvaa suruali Nyerere? alikuja Dar na Kinyasa au Rubega niniGeza...
Mimi si mtu wa kuingia katika mjadala kama huo wa mavazi.
Hauna maana yoyote.
Geza...si ulisema wakina Sykes na Baba yako walimfundisha kuvaa suruali Nyerere? alikuja Dar na Kinyasa au Rubega nini
Hongera ila acha hii mambo hamna Uhuru ambao unakuja na kutimiza matarajio ya kila aliyeupigania! Lazma kutakuwapo na watakaojihisi hawajafaidika nao kutokana na sababu zao binafsi! Corrective history haisaidii chchote zaidi ya kujenga uhasama! Mimi binafsi naona Nyerere alijitahidi to the extent ya kutaifisha shule za dini ila kila mtoto apate nafasi ya kusoma! na huko Ghana na Kenya unapokusifu hilo halikufanyika!Geza...
Inaelekea wewe ni mgeni na kalamu yangu.
Mimi nimepewa tuzo hapa kwa uandishi wa historia ya Tanzania.
Ingekuwa uandishi wangu ni wa namna hiyo wa kutukana ningedharauliwa.
Angalia picha hiyo hapo chini napokea cheti changu kutoka kwa Bwana Mkubwa Maxene Mello:
View attachment 2151047
Geza...Hongera ila acha hii mambo hamna Uhuru ambao unakuja na kutimiza matarajio ya kila aliyeupigania! Lazma kutakuwapo na watakaojihisi hawajafaidika nao kutokana na sababu zao binafsi!
madaktari watano mbona ume-mention wawili tu? Hao wengine ni madaktari wa nini? je watoto wa Mwapachu hawakuja kuwa viongozi senior yaani mawaziri serikali ya CCM (Mtoto wa TANU)? Hivi unajua injustices ngapi zilitokea huko Ghana kwa Nkrumah na hapo Kenya kwa Kenyatta baada ya Uhuru?Geza...
Mimi nazungumzia zaidi kufutwa historia ya kweli ya TANU na uhuru wa Tanganyika na kupachikwa historia ambayo kwa hakika si historia ya TANU.
Hebu soma hapo chini:
TUTEMBEE KATIKA BARABARA YA KUMBUKUMBU...VINGINEVYO ITAOTA MAJANI
Siasa za kikoloni zilikuwa zikibadilika na kwa hivyo zilihitaji damu changa zenye mawazo na mbinu mpya ili kuongoza harakati za kudai uhuru wa Tanganyika.
Serikali ya kikoloni ilikuwa kila kukicha inabadili mitindo, hila na mbinu za ukandamizaji ili kuendeleza utawala wake.
Ukitazama mwelekeo wa siasa na mazingira ya wakati ule, uongozi wa wazee katika TAA, kwa hali yao na kutokana na mambo yaliyokuwa yakiwakabili, walikuwa hawana uwezo wa kukabiliana na changamoto ya ukoloni.
Lakini pamoja na yote hayo, wazee hawakutaka kuachilia madaraka.
Jambo hili lilizusha mvutano baina ya wazee viongozi wa African Association na wanasiasa vijana waliosomeshwa na Waingereza.
(Rais wa TAA wakati ule alikuwa Mwalimu Thomas Plantan, mtoto wa Affande Plantan (Chief Mohosh) ambae baba yake alikuwa Chifu wa Kizulu kutoka Imhambane, Mozambique aliyeingia Tanganyika (Germany Ostafrika) mwishoni 1800 akiongoza askari mamluki 400 wa Kizulu kuja kulitia nguvu jeshi la Wajerumani chini ya Hermann von Wissman lililokuwa linapambana na Abushiri bin Salim na Mtwa Mkwawa).
Vijana waliokuwa wanataka mabadiliko ndani ya TAA walikuwa Abdulwahid na Ally Sykes, Tewa Said Tewa, Stephen Mhando, Dossa Aziz, James Mkande kwa kuwataja wachache.
Pamoja na hawa vijana wanamji wa Dar es Salaam walikuwapo madaktari watano – Dr. Joseph Mutahangarwa, Dr. Luciano Tsere, Dr. Michael Lugazia, Dr. Vedasto Kyaruzi na Wilbard Mwanjisi.
Haya yalikuwa ni mapambano baina ya kizazi kipya na kile cha kale.
Katika mvutano huu wa madaraka kwa upande wa vijana waliokuwa wakiinukia katika siasa za Tanganyika alikuwepo kijana wa Kidigo kutoka Tanga aliyesomea Makerere na Uingereza - Hamza Kibwana Mwapachu.
Mwapachu alikuwa ameajiriwa na Idara ya Maendeleo ya Jamii kama 'Assistant Welfare' Officer, Ilala Welfare Centre mjini Dar es Salaam.
Historia ya Mwapachu katika siasa inaanza Makerere College, Uganda ambako alijihusisha na mambo ya siasa wakati alipokuwa mwanafunzi.
Mwaka wa 1947 Mwapachu akiwa Tabora alichaguliwa kuwa katibu wa African Association, Julius Nyerere akiwa Naibu Katibu.
Huu ulikuwa ndiyo wakati Wasomi wa Makerere ''Makerere Intellectuals,'' jina walilopewa na Judith Listowel walikuwa wameanza kujishughulisha na TAA.
Hamza Mwapachu na Abdul Sykes walikuwa na usuhuba mkubwa sana.
Kipande hiki hapa hakitoshi kueleza nini wazalendo hawa wawili walifanya katika kupigania uhuru wa Tanganyika.
Mwaka wa 1950 Mwapachu alikuwa na umri wa miaka 37 na Abdul Sykes alikuwa na umri wa miaka 26, mdogo kwa Mwapachu kwa miaka 11.
Vijana hawa wawili, Hamza Mwapachu na Abdul Sykes walikuja kugeuza mwelekeo wa TAA na wakaingiza ndani ya chama hicho aina mpya ya uongozi uliokuwa haujapata kuonekana katika historia ya Waafrika wa Tanganyika.
Lakini wote wawili walifariki dunia katika ujana.
Hamza Mwapachu akiwa na umri wa miaka 49 mwaka wa 1962 na Abdul Sykes miaka 44, mwaka wa 1968.
Jambo la kusikitisha na kushangaza ni kuwa wote wawili ilipokuja kuandikwa historia ya TANU hakuna hata ukurasa mmoja uliokuwa na majina yao.
Halikadhalika madaktari hawa watano historia yao haifahamiki.
Wote wamesahauliwa na historia.
Hakuna kati yao hawa ambaye hii leo jina lake linahusishwa na historia ya uhuru wa Tanganyika.
Tusichoke kutembea katika barabara waliyopita hawa wazalendo mashujaa wa uhuru wa Tanganyika.
Picha: Kushoto ni Dr. Joseph Muhangarwa, Dr. Luciano Tsere, Dr. Vedasto Kyaruzi, Hamza Mwapachu, Abdulwahid Sykes, Thomas Saudtz Plantan na Tewa Said Tewa.
View attachment 2151061
Mengine yoote hayakuwa na sababu, hii aya ya mwisho haswa ndio kusudio lakoLakini faraja kubwa nilipata kwa kumsikia Prof. Haroub Othman akinambia kitabu changu kimebadili kabisa "legacy" yaani urathi wa Nyerere na alimfahamisha Mwalimu uso kwa macho nyumbani kwake Msasani.
Geza...madaktari watano mbona ume-mention wawili tu? Hao wengine ni madaktari wa nini? je watoto wa Mwapachu hawakuja kuwa viongozi senior yaani mawaziri serikali ya CCM (Mtoto wa TANU)? Hivi unajua injustices ngapi zilitokea huko Ghana kwa Nkrumah na hapo Kenya kwa Kenyatta baada ya Uhuru?
Nguruvi...Mengine yoote hayakuwa na sababu, hii aya ya mwisho haswa ndio kusudio lako
Kubadilisha legacy ya Nyerere!
Ni hivi Nyerere ndiye aliyeandika katiba ya TANU, si wengine kati ya 1929-1953.
Nyerere ndiye aliisambaza TANU nchi nzima! unajua ninamaaminisha nini
Nyerere ndiye Rais wa kwanza wa Tanganyika huru, hakuna Rais mwingine
Nyerere habari zake zipo katika maktaba zote za dunia hii, na wala hakuingizwa huko na mtu, watu walitafuta habari zake na kuziingiza huko.
Utafanya kila unaloweza, mwana wa Mwitongo atabaki kuwa wa Mwitongo ni Julius mjukuu wa Burito, mtoto wa Nyerere na Nyangeta. Hutaweza kubadili legacy yake!
Napita barazani mara narudi, safari hii naondoka. Wasalimie Kipata na Tandamti
Watu tumepita pia humo na tupo kimya!Nguruvi...
Hakika ndivyo ilivyokuwa ikifahamika hadi pale nilioandika kitabu cha Abdul Sykes ndipo wakajua kuwa historia waliyokuwa wakiamini haikuwa, ''kweli tupu.''
Wakataka kujua imekuwaje historia hii mpya haikupata kufahamika.
Ndipo nilipoalikwa University of Iowa na Northwestern.
Baada ya hapo nikaalikwa Zentrum Moderner Orient (ZMO), Berlin.
Ikitokea fursa In Shaa Allah nitakueleza nini kilitokea ZMO.
Kiamuacho uratha, yaani ''legacy,'' ya mtu yeyote ni matendo yake.
Mimi sina uwezo wa kubadili uratha wa mtu yeyote.Da
View attachment 2151221
Darasani University of Iowa na Prof. James Giblin
Geza...Watu tumepita pia humo na tupo kimya!