RIGHT MARKER
Senior Member
- Apr 30, 2018
- 129
- 473
Ndoa nyingi za siku hizi zinapatikana kwa njia hii...
Baada ya kutendwa na kuachwa na mpenzi wake aliyempenda kwa dhati, sasa anaamua kutafuta mtu yeyote wa kupoza maumivu ya kuachwa.
Penzi jipya la kupoza maumivu linaanza taratibu mwishowe linakolea kwa kasi, kila mmoja anasahau stress zake za nyuma. Kufumba na kufumbua mimba imetunga.
👩🏾"Baby nina mimba yako, wazazi wangu wakijua kuhusu hii mimba sidhani kama watanielewa"
👨🏾"Duh! Kwa nini siku ile hukuniambia nitumie kinga? Kwahiyo tufanyeje yaani nimeshavurugwa"
👩🏾"Mimi mwenyewe nimevurugwa yaani wazazi hawawezi kunielewa. Huyo baba yangu ndo kabisa anaweza hata kuniua"
👨🏾"Basi ngoja nimtafute mzee nije kwenu kuonekana kwa wazazi wako. Umenikosea sana, yaani ulikuwa unajua ni siku zako za kushika mimba halafu hukuniambia"
Hatimaye ndoa imepatikana. Aliyetendwa na barafu wa moyo wake hatimaye amekwenda kuoana kwenye penzi la kupoza maumivu.
BAADA YA MIAKA MITATU MBELE:
📱"Nasikia sikuhizi una ndoa. Hongera sana X wangu niliyekupenda kwa dhati, ni mambo ya dunia yalitutenganisha hata hivyo haikuwa bahati yetu kuoana ila nina imani bado tunapendana"
📱"Duh! Mwana mpotevu umeonekana😃kwahiyo tulivyoachana ulidhani sitopata mwingine? Hata hivyo nilikupenda sana na bado nakupenda. Hii ndoa yangu niliingia tu bila kupenda"
Hatimaye penzi la X linarudi upya, tena linarudi kwa kishindo ili kuvunja ndoa iliyopatikana kwenye penzi la kupoza maumivu. Kinachofuata ni kuvunjika kwa ndoa kisha kukimbizana kwenye ofisi za ustawi wa Jamii na mahakamani kwa ajili ya kuuza na kugawana pesa za nyumba ya familia iliyojengwa kwa shida.
RIGHT MARKER
Dar es salaam.