KERO Responded Kiwanda cha Kagera Sugar kilipe madeni ya Wakulima wa Miwa, wana hali ngumu!

KERO Responded Kiwanda cha Kagera Sugar kilipe madeni ya Wakulima wa Miwa, wana hali ngumu!

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Mzee wangu ni mkulima wa miwa Wilayani Missenyi hapa Mkoani Kagera, moja ya jambo ambalo linanifanya niandike hapa ni kwa kuwa tunapoelekea nitamuona baba yangu anaanza kuwa chizi au kuongea peke yake kutokana na msongo wa mwazo alionao wa kutolipwa malipo ya mazao yake kutoka katika Kiwanda cha Kagera Sugar.

Baba pamoja na wakulima wenzake wengi hawajalipwa malipo yao ya kuuza mazao katika kiwanda hicho tangu Desemba 2025, msimu umeshafungwa na sasa wanajiandaa kuelekea katika msimu mwingine lakini hana fedha ya maandalizi, hana fedha ya kuendesha familia yake wa kuwa malipo anayodai ni makubwa.

Kiwanda kiliwaahidi kitawalipa wiki chache tangu wafanye hiyo biashara, kila wakifuatilia wanaambiwa “tutawalipa tu”, sasa kilicho cha wazee wetu siyo cha mtaji mkubwa hivyo malipo kutofanyika kwa wakati ni mwanzo wa kuwayumbisha kiuchumi kisha wakati Serikali inasema inatengeneza mazingira mazuri ya kuwawezesha Wananchi wake.

Hii siyo sawa, tunaomba Wiziri wa Kilimo pamoja na Wizara ya Ajira iingilie Wakulima wa Kagera wanaoidai Kagera Sugar walipwe stahiki zao, kwani wameshafika hadi kwa viongozi wa Kiserikali ngazi ya wilaya kote huko hakuna majibu ya kueleweka.

Kiongozi wa Wakulima atoa neno ~ Kiongozi wa Wakulima wa Miwa, Wilbroad Cyprian asema “Mazungumzo yanaendelea na Kagera Sugar kuhusu malipo ya Wakulima wa Miwa
 
Mkuu wao yy anajilemba zake uko!! Wala hajali kuhusu watanganyika kwakweli.
Kazi ni kipimo cha utu
 
Back
Top Bottom