Kiwanda cha kusindika nyama chazinduliwa Tanzania

Uwe na siku njema.
 
Kwahiyo alienda kujenga mahali umeme hakuna?maji si unadrill tu tena ni cheap kuliko kutumia ya serikali....kwa ulivyosema huo mkopo utamshinda

Umeme upo ila unakatika hovyo na power yake ni ndogo, ila kwa saivi ndio naona kuna msongo mkubwa wa umeme umeongezwa area hiyo. Maji alikuwa ananunua ya serikali 12m per month. Viwanda vya nyama vinatumia sana maji na hasa ukute wana process na ngozi ndio balaa zaidi. Option ya kudrill maji kweli ingesaidia sasa sijui project plan yake ilikaa vipi hadi akakwama.
 
Kuna msemo usemao ''if you live off people's praise, criticism will destoy you! Tatizo kubwa kabisa la awamu hii ni kutaka kujitangaza na kusifiwa kwa mambo ambayo ni ya kawaida. Hivi mnajua Tanzania ilikuwa imepiga hatua kisasi ambacho hata tunayofanya sasa tulitakiwa tuyafanye kwa kificho ili tusijiabishe? Kwa nini jambo dogo la kawaida tunalitangaza na kutaka kila mtu asifie? Mpaka sasa huwa naona aibu jinsi serikali yote ilivyokuwa inahamia uwanja wa ndege kupokea ndege moja! Kwa nini tusiwe na utaratibu wa tukasubiri hata zikaja zote halafu tukatenga siku moja ya kuzindua?
 

Naona maelezo yako ni irrelevant.. Hapo hakuna kusifiwa. Ni kueleza kitu katika uhalisia wake.

Sasa unapoongelea kitu in past tense kwamba ilikuwa ila sasa sivyo tena hivyo vinavyofanyika kwa kizazi cha sasa ni kigeni. Na pia tambua kila mtu ana utashi wake katika kuongoza.
 
Utashi wa kijinga kabisa huu wa kupenda kusifiwa na kuabudiwa kama Mungu. Na ndiyo maana nikakuambia kuwa 'if you live off people's praise, criticism will destoy you! Unapopenda kusifiwa na kuabudiwa kubali pia kukosolewa na kudhaurauliwa. Wahenga walisema debe tupu haliachi kuvuma. Ukifanya mazuri huna haja ya kupaza sauti ili watu waone. Hata ukimya au sauti ndogo inaweza kuwa kufanya watu waone kuliko kupayuka. Ni kweli kila mtu ana utashi wake lakini huu utashi mwingine ni kama laana.
 
Nashukuru Sana mkuu kwa kunitoa tongotongo,nilidhani ni branch ya kiwanda.kwa kweli,Mimi huwa nasikia tunajenga viwanda,Ila huwa sijui viko wapi,na huwa sivioni, nashukuru,Ila serikali ifanye kazi ya kuelewesha wananchi wake kazi kubwa inayoifanyika kwenye nchi yetu.
 
Watanzania tuna asili ya ubishj hata kama kitu kinaonekana, mifano ipo hai sana na vitu vipo wazi lkn bado unakuta mtu anabeza na kudharau sana kana kwamba ni vitu vya kawaida tu kama vile tulikuwa navyo,
Kiukweli Tz hatuna uzalendo wa maendeleo tunayoyauna hivi leo zaidi ya kubeza na matusi bila kutaka kujua mambo zaidi

Chalinze kuna viwanda kibao tu kule na vipo ndani ndani maaana kuna mtu anaweza sema mbona havionekan akiwa ana pita pale barabarani
Lkn Pwani imejikuta imezungukwa na kila ya kiwanda aisee


Serkali imefanya mazingira ya uwekezaji kuwa rafki sana kwa wawekezaji wa ndani na nje hasa sekta ya viwanda,
 
Vipi kile cha mwanza hadi nyama ya mbuzi ikapanda bombadia kwenda dubai iliishia wapi?

Kwa habari kamili ni kuwa ile nyama ya mbuzi ilipelekwa airport ikapigwa picha baada ya hapo ikarudi kuozea kwenye mafridge.
 
Kama hiki ndio kiwanda cha nyama kikubwa EAC, basi viwanda vya nyama EAC viko kwenye nyumba za kuishi watu. Na huo ukubwa ni wa eneo au mitambo? Kama ni eneo waongezeni eka 50 kiwe kikubwa duniani Kurugeni ya Habari ipate jambo la kumsifia raisi!
Aiseeee!!
 
Shida siyo watu, ila ni pale Kiongozi anapojifanya anajua kila kitu na wote wengine hawajui au hawajawahi kuona. Mwanza eneo ls Usagara kuna Kiwanda kikubwa na cha Kisasa kinaitwa Chobbo Enterpr. Hiki kina uwezo wa kuchinja ngombe takriban 1000 kwa siku na kimeanza kazi takriban miaka 5 iliyopita! Nowadays nobody is proud of! Ukifika leo hutatamani kuinvest kwenye viwanda kama hivi!
Sasa unapomuona mtu mkubwa akishabikia ufunguzi na siyo uendeshaji, kwa vyovyote lazima umshangae
 

Hiki kiwanda sio mali ya serikali bali ni mwekezaji
So uendeshaji wa mtu binafsi naamin unajua jinsi atavotaka kurudisha fedha yake,
So serikali imeitwa kwenda kuzindua tu kwani wizara yenye mamlaka ni wajibu wake kukitangaza na kuwatangazia watanzania ili wajue watapata wapi soko la mifugo yao na fursa zingine kama ajira,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…