Kiwanda cha madini adimu kujengwa kijijini cha Ngwala Mkoani Songwe

Kiwanda cha madini adimu kujengwa kijijini cha Ngwala Mkoani Songwe

Mpepetaji

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2025
Posts
346
Reaction score
213
Kampuni ya Mamba Minerals Ltd inayowekeza kwenye mradi wa madini adimu imeweka wazi mpango wake wa kujenga kiwanda cha kusafisha na kuongeza thamani madini adimu kijijini Ngwala Mkoani Songwe badala ya kusafirisha madini hayo yakiwa ghafi.

Hayo yamesemwa wakati wa uzinduzi wa zoezi la ulipwaji fidia wananchi waguswa wa mradi takribani 192 zoezi ambalo limezinduliwa na Waziri wa Madini Mh. Anthony Mavunde.

Akitoa maelezo ya awali,Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Mamba Minerals Ltd Ndg. Ismail Diwani amesema zoezi hilo la fidia litagharimu kiasi cha Tsh 5.3 Bilioni kwa kuhusisha wananchi waguswa wa mradi 192 ambapo mpaka sasa wananchi 116 wamepokea malipo yao tayari.

“Hatua hizi ni za awali kuelekea kwenye utekelezaji wa mradi ambapo shughuli rasmi za ujenzi wa mradi zitaanza Disemba 2025 sambamba na ujenzi wa kiwanda cha kusafisha madini adimu na ujenzi wa mtambo wa kufua umeme utakaozalisha megawati 12”Alisema Ismail

Waziri Anthony Mavunde ameipongeza Kampuni ya Mamba Minerals Ltd kwa ujenzi wa kiwanda cha kusafisha madini hayo hapa nchin ikiwa ni uongezaji wa thamani wa madini hayo kabla ya kusafirishwa ikiwa ni sehemu ya kuitikia wito uliotolewa na Mh. Rais Dkt. Samia S. Hassan juu ya uongezaji thamani madini nchini.

Naye Mkuu wa Wilaya wa Songwe Mh. Solomon Itunda amesema mradi huu utachochea ukuaji wa sekta ya madini Mkoani Songwe kwa kiwango kikubwa na hivyo kuufanya mkoa huu kuwa kati ya wachangiaji wakubwa katika kukuza uchumi wa nchi kupitia sekta ya madini.
snapins-ai_3647591358139833056.jpg
snapins-ai_3647591358207029497.jpg
 
madini adimu? hayana jina? huu ni utapeli
 
Back
Top Bottom