Tatizo letu watanzania ni kutokuwa na uzalendo wa kujenga nchi yetu...mambo yafuatatayo yanaonyesha tuko hivyo
1. Walimu hususani wa shule za msingi na sekondari za serikali kuchelewa kufika kazini na kutoa visingizio mbalimbali... ohoo usafiri mgumu n.k. Pia hawafundushi kwa moyo
2. Wafanyakazi wa idara zote za serikali kudai rushwa au kutengeneza mazingira ya rushwa ndipo kazi ifanyike. mfano upatikanaji wa leseni mbalimbali, matibabu hospitali za serikali, usalama barabarani, vituo vya polisi n.k
3. Wafanyakazi wa maofisini (asilimia kubwa) hawafanyi kazi kwa kujituma... muda mwingi wa kazi (valuable time) huutumia kupiga soga.. na wakati mwingine huingia kwenye mitandao na kufanya surfing. hii ni quality time, mtu yapaswa azalishe. Inakuwa vizuri kama umetimize lengo lako la siku ndio upige domo (kama kuna performance management system) au upoteze muda kwenye surfing
4. Viongozi wote wapo kwa maslahi binafsi na si kwa maslahi ya wananchi wao.Wengi ni wala rushwa, mafisadi na wana uchoyo ulio kithiri. Wakielezwa ukweli wanatoa vitisho. Mfano Chiligati na Mkapa enzi zake.
5.Hatupendi kujishughulisha na kuwa na mbinu mbadala za kujiongezea kipato au kusaidia kuboresha maisha ya wengine. Mfano, toka umemaliza shule (labda university) umewahi ku impart knowledge yako kwa mtu mwingine (academic knowledge)?
6.Tukitoka kazini ni kuendekeza starehe tu, kama vile kwenda club, baa, grocery, uzinzi au kujishughulisha na masuala yasiyo kipaumbele kwa maisha yetu. Eti tumechoka kwa kufanya surfing na kupiga soga!!!! Lol
7.Sio wabunifu at all. mfano, viongozi especially hata Rais anatumia nguvu na ubabe kuwaambia watu wa bandarini waharakishe upakuaji na upakiaji wa makontena ili kuondoa msongamano... Hana solution! hiyo kazi itafanyika vipi? Tatizo pale ni kipato... pay the godamns workers (loaders/offloaders) well. Hakika hautaona kontena pale. Maskini wale ndio the least paid employees!! Ndio maana wanaiba power windows za magari. Kule Holland (Roterdam), wafanyakazi wa Bandari wanalipwa kuliko wa sekta nyingine. Hakuna kulala pale. Hebu Mr. President aende akapate somo pale.. then akienda bandarini ataenda na solution
8. Mkulima analima mazao ya kumtosha kwa miezi minne au mitano tu ya mwaka.. na wakati ana shamba kubwa ameacha majani tu yanaota. Miezi mingine yote anakuwa omba omba. Nimesikia Tanzania tunalima asilimia 1% tu ya arable land...what a shame!
Kwa maisha haya tunayoishi, hakika hatutatoka kwenye umaskini na hatuwezi kuwa wabunifu hata kidogo.
Nyumbu limevumbuliwa toka enzi za marehemu sokoine ... toka kipindi kile hadi leo hakuna version mpya ya magari hayo... at least sasa hivi tungekuwa na sungura basi.