Phidsnipes
New Member
- Oct 8, 2026
- 3
- 0
Naandika uzi huu nikiwa mmoja wa wakazi wanaotaabika na kero endelevu ya uchafuzi wa mazingira na hewa unaofanywa na Kiwanda cha Maranile Industries Limited, kilichopo eneo la Misugusugu / Saeni (Kibaha, Mkoa wa Pwani).
Kiwanda hicho kinachojihusisha na uzalishaji wa Ethanol, pombe kali pamoja na gesi ya Carbon Dioxide, kimekuwa kikitumia mbinu ya kuachilia hewa/gesi zenye harufu kali sana ya kemikali na chachu nyakati za usiku wa manane hasa kuanzia saa 7:00 usiku hadi saa 8:30 usiku.
Mambo yanayojitokeza usiku:
Pamoja na hatua zilizowahi kuchukuliwa siku za nyuma na Baraza la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) pamoja na Uongozi wa Manispaa ya Kibaha dhidi ya viwanda vya eneo hili, Maranile Industries bado haijabadilika na inaendelea kukiuka sheria za usimamizi wa mazingira kwa siri za usiku.
Tunaomba NEMC Mkoa wa Pwani / Makao Makuu kufanya ukaguzi wa ghafla wa usiku wa manane (night surprise inspection) kati ya saa 7:00 na 9:00 usiku ili kujionea wenyewe hali halisi.
Tunamwomba Mkuu wa Wilaya ya Kibaha na Mkuu wa Mkoa wa Pwani kuingilia kati ili kulinda afya za raia na wakazi wa Misugusugu na Kongowe.
Uzalishaji usiwahi kuwekwa mbele kuliko afya na haki ya wananchi kupata hewa safi na salama.
Nawasilisha.

- Harufu Kali na Inayosukuma Tumbo: Harufu inayotoka kiwandani hapo nyakati hizo za usiku ni kali kiasi cha kuamsha watu waliolala na kusababisha kichefuchefu, maumivu ya kichwa, na kero kubwa ya kupumua.
- Kukwepa Ukaguzi wa Mchana: Ni dhahiri kuwa usafishaji wa mitambo na uachiaji wa hewa hii chafu unafanyika usiku ili kukwepa wakaguzi wa mazingira na serikali ambao mara nyingi hufanya doria zao nyakati za mchana.
- Athari kwa Afya na Watoto: Watoto wadogo na wazee ndio wanaoathirika zaidi na hewa hii nzito yenye sumu/kemikali inayopenya hadi ndani ya nyumba.