Kiwanda cha Matairi Arusha tuliambiwa kingeanza kufanya kazi, nini kinaendelea?

Kiwanda cha Matairi Arusha tuliambiwa kingeanza kufanya kazi, nini kinaendelea?

Koryo2

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2016
Posts
2,056
Reaction score
2,519
Bajeti ya 2020/2021 tuliaminishwa kuwa kiwanda cha General Tyre cha Arusha kingekarabatiwa ili kiwanda kianze kuzalisha matairi. Mpaka sasa ni kimya na sisi wananchi hatuji kinachoendelea.
 
Nchi hii viwanda tulishafeli
Sahv ni mwendo kamari,watu kufungua kumbi za starehe bar,lounge basi ndicho tunachoweza

Ova
 
Kile kiwanda mitambo yake iko outdated, kukifufua ni gharama kuliko
 
Kwa akili za Watanzania wenye mamlaka ya maamuzi, wako tayari kutengeneza mazingira ya kukimalizia kabisa hicho kiwanda ili tu wapate 10% ya kuagiza matairi kutoka nje.

CCM hawajawahi kuwa na uchungu na hii Nchi! Labda Mwalimu Nyerere na wenzake wachache! Ika sera zao nazo zilikuwa ni kitanzi kwa mashirika mengi.
 
Kitafufuliwa na serikali pendwa ya awamu ya sita.

Rais wetu ni msikivu sana na Mnyenyekevu.

Wakazi wa Arusha tunampenda sana.
 
Kitafufuliwa na serikali pendwa ya awamu ya sita.

Rais wetu ni msikivu sana na Mnyenyekevu.

Wakazi wa Arusha tunampenda sana.
Issue syo kufufuliwa
Je kwa mfumo wa nchi hii
Watakubali kukifufua au mtaendelea
Kutegemea mataili toka kwa wavimba
Macho nk

Ova
 
Bajeti ya 2020/2021 tuliaminishwa kuwa kiwanda cha General Tyre cha Arusha kingekarabatiwa ili kiwanda kianze kuzalisha matairi. Mpaka sasa ni kimya na sisi wananchi hatuji kinachoendelea.

Kiwanda cha Matairi Arusha nimepata investor kutoka China wanakitaka kukijenga upya kwa technologies ya kisasa. Ni utaratibu upi ukikapata?​

Issue syo kufufuliwa
Je kwa mfumo wa nchi hii
Watakubali kukifufua au mtaendelea
Kutegemea mataili toka kwa wavimba
Macho nk

Ova
Macho madogo wanatupiga sana.
 
Back
Top Bottom