Kiwanda cha Metafrax Chemicals katika eneo la Perm nchini Urusi chashambuliwa na Drones za Ukraine!!

Kiwanda cha Metafrax Chemicals katika eneo la Perm nchini Urusi chashambuliwa na Drones za Ukraine!!

Echolima1

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2019
Posts
9,662
Reaction score
8,023
Ndege zisizo na rubani za Ukraine za masafa marefu zilishambulia kiwanda cha Metafrax Chemicals katika eneo la Perm nchini Urusi, takriban kilomita 1,700 kutoka mpaka wa Ukraine, katika mojawapo ya operesheni za ndege zisizo na rubani za Ukraine zilizoripotiwa kushambulia ndani zaidi eneo la Urusi tangu vita vianze.

Kituo hicho, ambacho ni mojawapo ya wazalishaji wakubwa wa methanoli na kemikali nchini Urusi, hutoa vifaa na vipengele kwa watengenezaji kadhaa wa ulinzi wa Urusi wanaohusika katika uzalishaji wa mifumo ya ndege, ndege zisizo na rubani, injini za roketi, vilipuzi, na vifaa vya elektroniki vya kijeshi..

Putin hawezi tena kuimaliza hiyo vita maana sasa ni wazi kwa miaka 5 hii imeonyesha kabisa Ngoma ni nzito kwake bora asalimu amri kijana kwa kutaka mazungumzo na Ukraine maana kwa mabavu imeshindikana kabisa!!!

 
zilishambulia kiwanda cha Metafrax Chemicals katika eneo la Perm nchini Urusi, takriban kilomita 1,700 kutoka mpaka wa Ukraine,
Dah,
1,700km ni ndani sana. Mdharau mwiba mguu huota tende ndiyo hiyo sasa.
Putin kazi anayo
 
Dah,
1,700km ni ndani sana. Mdharau mwiba mguu huota tende ndiyo hiyo sasa.
Putin kazi anayo

Kadiri siku zinavyoenda, uwezo wa kivita wa Ukraine unazidi kuongezeka. Ukraine mpaka sasa imeangamiza viwanda zaidi ya 10 vya Urusi vya kusafisha mafuta. Uwezo wa Urusi kuzalisha mafuta umeshuka kwa karibia 40%, hali inayozidi kuyumbisha uchumi wa Urusi. Uchumi wa Urusi uliokuwa ukikua kwa7% kabla ya vita umeshuka mpaka 0.4%.
Ukraine imefanikiwa kutumia robots kupigana. Wiki 3 zilizopita, Ukraine kwa kutumia robots iliwatandika wanajeshi wa Russia mpaka kusalimu amri, wakachukuliwa mateka na kupokonywa eneo walilokuwa wanashikilia.

Urusi inakabiliwa na tatizo jingine kubwa la kukosa wataalam vijana mbalimbali muhimu ambao wameamua kukimbilia Ulaya, kuepuka kulazimishwa kwenda vitani, na pia uchumi unaozidi kudorora.
 
Urusi baada ya kuishiwa mbinu, imebakia kuyatishia mataifa ya Ulaya na Ukraine kwa silaha za nuclear.
Hahaha,
Na hizo Nukes haitawahi kutumia, ni vitisho tu.

Putin akiendelea kushupaza shingo Urusi itageuka mlenda muda si mrefu
 
Back
Top Bottom