Kiwanda cha miwa cha Mkulazi ni kilio kwa wananchi

Kiwanda cha miwa cha Mkulazi ni kilio kwa wananchi

Mashamba huwa yanapigwa moto, miwa kufyekwa na kupelekwa kiwandani, kuna time frame, la sivyo miwa inaharibika ikicheleweshwa kuwa processed.

Viwanda ni Turiani Mtibwa na Kilombero navyo havipo karibu ni mbali na vina miwa yao. Nafikiri pia kutahitajika makubaliano, ambayo yatachukua muda, mwaka huu miwa imeshamiri vizuri na mvua.

Hasara na POLE kwa wakulima! Na wastaafu ambao mafao yao yametumika ndivyo sivyo!

Everyday is Saturday......................... 😎
Yaani ukiwaza sana hasara kwa huyo mtanzania basi inabidi utazame chini na kuchora na kidole bila kufahamu unachokichora.
 
Habari!

Hiki ni kiwanda cha miwa cha mkulazi(Mbigili).

Hapa kiwandani baadhi ya miwa imekomaa lakini kiwanda haifahamiki kitaanza lini usindikaji.

Ni kiwanda ambacho kipo wilaya ya Kilosa, ujenzi wake unasuasua sana.

View attachment 1477117

Baadhi ya miwa ikiwa tayari kuvunwa lakini kiwanda hakieleweki.

Rais Magufuli aliiagiza benki ya Azania kuwapa mikopo wakulima wa nje(outgrowers) kupitia vyama vyao vya ushirika(AMCOS). Azania benki ilitoa pesa hapo awali lakini sasa imegoma kuendelea kutoa pesa kwa vile kiwanda hakieleweki.

Mbaya zaidi wakandarasi waliotoa huduma ya kulima, kusambaza mbolea, madawa na mahitaji mengine hawajalipwa mpaka sasa.

"Maisha yamekuwa magumu sana, pesa zetu hatulipwi na mimi nilikopa benki baadhi ya mtaji wangu".......alisikikaa mmoja kati ya wakandarasi.

"Nilitoa shamba langu kwa ajili ya kulima miwa, tuliambiwa ina faida sana kuliko mpunga, mpaka leo miwa inadumaa tukiwafuata Amcos wanatuambia Azania hawataki kutoa pesa mpaka kiwanda kikamilike".........alisikika mmoja kati ya wakulima wadogo wadogo.

Baadhi ya wakandarasi wamejaribu kuonana na waziri Jesta Muagama bila mafanikio.

Ndugu yangu hawa wanasiasa wa serikali hii ni hatari sana kwa maisha yetu, wanakuja hapa wanatuambia limeni tu kiwanda kitaanza kazi punde, tunawapa kazi makampuni ya kulima tukienda benki wanasema hatutoi pesa mpaka kiwanda kikamilike"......alisikika mmoja kati ya viongozi wa Mbigiri-Amcos.
Kimsingi hali ni mbaya sana hapa ila watu wanaogopa kupaza sauti. Kila mmoja akiambia iki ni kiwanda cha rais Magufuli anaogopa kupaza sauti kwa hofu ya kuambiwa anamchonganisha Rais na wananchi.

"Tuliambiwa rais Magufuli angekuja mwezi wa Januari mwaka huu ili kukifungua kiwanda, mpaka leo mwezi wa sita kimya. Hali ni mbaya kwelikweli umasikini unazidi kutujaa ni bora tungelima mpunga tu"........mkulima alilalamika lakini alihofu kutaja jina lake.

Chanzo chetu cha habari kilijaribu kuuona uongozi wa Azania benki na majibu yao yalikuwa yaleyale....HAWATOI PESA MPAKA KIWANDA KIKAMILIKE.

"Rais anapaswa kuingila kati ili atuokoe sisi wakandarasi maana toka mwezi wa 12 mwaka jana hatujalipwa pesa zetu na benki na taasisi tulizokopa pesa wanaanza kuuza dhamana zetu tulizoweka".....mmoja kati ya wakandarasi alizidi lalamika.

Majungu ya kimachinga yamezorotesha ukamilikaji wa kiwanda.
Rais anatakiwa afanye maamuzi sasa urafiki na marehemu kwa mjomba uliisha mjomba alipofariki
 
Majungu ya kimachinga yamezorotesha ukamilikaji wa kiwanda.
Rais anatakiwa afanye maamuzi sasa urafiki na marehemu kwa mjomba uliisha mjomba alipofariki
Unamzungumzia 'njomba'?
Marehemu kaacha familia tusisahau hilo.

Everyday is Saturday............................... 😎
 
Bado tu mambo hayajatengemaa?
Hii investment ilikuwa ya NSSF na washirika wake I.e pension Funds ambazo ndiyo wamiliki au shareholders wa Azania Bank. Changamoto ipo hasa hizi merging za Pension Funds bado mambo hayajatengamaa. . Poleni wakulima.
 
Inasikitisha sana taifa kuwa na watu wengi wasiokuwa na maarifa basic ya uchumi na biashara.
Tatizo watz wengi wetu ni wajinga mno.

Tunasifia kitu hata hatujui madhara yake.

Nimekutana na mtu mmoja anamsifia Rais Magufuli.
"Rais huyu noma sana...ni kiboko....aendelee hivi hivi....hakuna kuongeza mshahara toka aingie madarakani.....tutaheshimiana tu."

Yeye ni mchuuzi anauza matunda sokoni.

Hapo hapo analalamika biashara mbaya sana.....watu hawanunui matunda.
 
🙄🙄🙄😒😒😒😏😏😶😶😑😑😐😐🤨🤨🤐
 
Waendelee kudhamini ndoa za wasanii tu kukitangaza hicho kiwanda
Chao

Ova
 
Mkulazi na bagamoyo sugar ya mzee bakharesa kilianza mkulaz lakn maajabu mzee ameanza uzalishaji wao bado mpaka leo

Wakulima walihamasishwa kulima miwa lakn kiwanda hakizalishi

TUSIAMINI MANENO YA WANASIASA
 
Back
Top Bottom