Kiwanda gani naweza fungua/anzisha kwa gharama ya millioni nne?

mitale na midimu

JF-Expert Member
Joined
Aug 26, 2015
Posts
10,420
Reaction score
17,735
Binafsi ni muumini wa kilimo na Teknolojia. Najaribu kuwaza kiwanda gani naweza kununua au kutengeneza kwa gharama ya millioni nne za kitanzania angalau kije kufunguliwa na kiongozi wangu wa mtaa.

Kiwanda chochote cha kuongeza thamani bidhaa za shamba au asili.

Naamini hakuna ambacho kimewahi shindikana humu.

Msaada please.
 
Nunua vyerehani nane alafu muite magufuli aje kufungua kiwanda cha kubadili katani na pamba kuwa nguo.
 

Kwa kiwango cha pesa ulicho nacho nakushauri ufanye kati ya biashara zifuatazo:
1. Nunua mashine za kutengeneza peanut butter. Mashine hizo ni peanut grinder, peanut roster na meza ya kufanya sorting. Hiyo hela itatosha na utabakiwa na kiasi fulani cha kunjnua raw materials (karanga) za kutosha za kuanzia.

2. Biashara ingine nunua mashine ya kusaga na kukoboa unga wa mahindi na uwe unapaki. Mashine hizo fanya zitumie motor moja ku run mashine zote mbili ili kuokoa gharama. Hapa sidhani kama utakuwa na hela ya materials ya kuanzia.

Pia kwenye case zote mbili nime assume utakuwa na shed ya kuweka hizo mashine.

Kila la heri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…