Malaika Mkuu
JF-Expert Member
- Nov 5, 2014
- 902
- 909
Kampuni kubwa ya Nishati duniani, Shell, imeeleza kuwa imepiga hatua kubwa katika miezi ya karibuni kwenye majadiliano yake na serikali ya Tanzania kufanikisha ujenzi wa kiwanda kikubwa cha kuchakata gesi asilia (LNG) mkoani Lindi.
Hizo ni habari njema kwa Tanzania ambayo licha ya utajiri mkubwa wa nishati hiyo, haijakamilisha mipango ya ujenzi wa kiwanda hicho ambacho kinatarajiwa kugharimu mabilioni ya dola.
Mradi utafungua fursa za kibiashara, kukuza uchumi wa nchi na kutoa maelfu ya ajira kwa miaka mingi.
Afisa mwandamizi wa shell, Wael Sawan amerliza shirika la habari la Reuters kuwa serikali ya Tanzania na kampuni yake wamefika hatua kubwa ndani ya mwaka mmoja kuliko ilivyokuwa awali.
Sheli ina leseni ya kuendesha vitalu viwili (Block 1 na Block 4) vilivyoko bahari ya Hindi. Kwa pamoja vina futi za ujazo trilioni 16 ya gesi asilia inayoweza kuvunwa. Kampuni hiyo inakusudia kuwekeza kwenye mradi huo kwa kushirikiana na aquinor kutoka Norway.