Kiwanda kinachotengeneza Barakoa zinauzwa Muhimbili kiko wapi na kinamilikiwa na nani?

Nitashangaa sana kama viongozi wa serikali yetu wanaojinasibu kwa uzalendo kila siku watakuwa wanahusika na hiyo biashara.

Muhimu tuambiwe ni nani mmiliki wa hicho kiwanda, sio kila siku tunalazimishwa kuamini barakoa toka nje zina matatizo ya kiafya wakati ni wao ndio walioruhusu ziingie.

Sikutegemea kama kuna watu watawaza biashara katikati ya hali hii tuliyonayo.
 
Cha kushangaza hawajawahi kutengeneza pamba ya kuoshea vidonda , lakini eti barakoa wanatengeneza!
Machine za hiki kiwanda zimetoka China. Malighafi zote za kutengeneza hizo barakoa zinatoka China waliopo mitamboni kwenye uzalishaji ni Wachina, halafu kuna lofa mmoja anasema usitumie barakoa za nje.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…