eka moja ni sh ngapi Malila?
Kuanzia pale Kisemvule,Kibamba, Mwanambaya,Dundani inabidi uwe na kiasi kisichopungua 25M mpaka 40M kwa vile vya barabarani vinavyopakana na viwanda, wenye mashamba kupitia madalali feki wanapayuka tu, lakini ukiruka mita kadhaa nyuma ya barabara unapata kwa bei poa kabisa, mpaka laki tano kwa eka. Tatizo eneo lote kuanzia Kongowe halijapimwa,sasa unaweza kununua nyuma/ndani ndani kwa bei poa halafu baadae ukakosa njia au huduma muhimu.