Kiwango Cha bwana mdogo Feisal Salumu kinazidi kutitia kwenye tope zito la udongo mfinyanzi

Unaushahidi gani kwamba ngasa hakuambulia kitu.

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
Umemjibu vizuri..

Halafu Hawa wanaopiga kelele humu kwa kusema 4 M ni peanut, wengine Wana lipwa laki kadhaa tu. Na wanafanya kazi Kila siku hawaachi..

Dogo alitakiwa ashauriwe vizuri ila sio hii mihemko..

Na naona watu wanajitahidi kumuongelea Ili asisahaulike.
 
Asa ulitaka nilipwe kiasi gani kama kazi yangu ni kukata majani? Kila mtu alipwe kwa anachostahili.
Unaona million 4 kwa mwezi nyingi ( kwa wachezaji ambao career zao ni fupi).
Mfano,
Mchezaji awe kwenye Peak kwa miaka 10 mpaka 15.
4×12×15= 720 Millions
Baada ya hapo ndio basi tena, kama hakuwekeza popote aje tuchome Mishkaki.
 
Kosa lipo wapi Sasa kwa timu au kwa feisali?? Afuate utaratibu tu.

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Kweli kabisa mkuu.

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Nafikiri point sio kurudi yanga. Yanga Isha prove kuwa inafanya poa hata bila yeye.

Ila uhalisia ni kuwa ana washauri wabaya, madhara ya ujinga i.e. ujinga unamgharimu
Dogo ni kilaza wa mwisho kabisa. Ngoja tuone mwisho wake utakuwaje. Anaitwa timu ya Taifa akitambulika kama mchezaji wa Yanga ambako hayupo!!

Ni Tanzania pekee ndiyo unaweza kuona maajabu kama haya.
 
Yanga wanataka kuua kiwango cha mchezaji huyu - mbeleni wewe mchezaji ukitaka kujiunga Yanga angalia sana kipengele ya kuvunja mkataba wako, hii timu siyo kabisa.

Kama mchezaji hakutaki si mwache anende, masuala ya kung'ang'aniana ni ya miaka ya 90 wakati kina Kipese wanacheza.
 
Asubiri mkataba uishe ndiyo aondoke yanga Ina wachezaji wengi sana.

Dogo anaua kipaji chake mwenyewe na Yule aliyemdanganya kwani angesubiri mkataba uishe nani angemzuia kuondoka

Dogo kajichanganya mwenyewe.

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Fair play ni kuangalia mchezaji kwanza namna atakavyoathirika, hata Man kwa mfano waliamua kuachana na Ronaldo baada ya kuona hana nia ya kuipigania timu. Club kumkomoa mchezaji si fair play.

Huu mfano uigwe na Yanga, Man hawakutaka kujua nani ama Club gani imemdanganya Ronaldo, wakamaliza wenyewe - then jamaa akaibukia anakokutaka yeye - huo ndiyo Mpira wa leo.

Ronaldo said: "Following conversations with Manchester United we have mutually agreed to end our contract early. "I love Manchester United and I love the fans, that will never ever change. However, it feels like the right time for me to seek a new challenge
 
Mkataba wa Ronaldo ni tofauti na mkataba wa feisal mkuu

Hapa tupo Tanzania hatupo huko unapo paongelea .

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Sema kama mchezaji ana itikadi za kimbumbumbu, asijaribu kwenda Yanga. Mchezaji aina ya Fei Toto ni wa kudharauliwa tu. Maana siyo muungwana, ni mzushi, hana shukrani, na hajitambui.
 
Yanga acheni ulizi muacheni dogo akatafute riziki sehemu nyingine mbona msuva alikaa mwaka mzima lakini anakiwasha mpaka leo dua la kuku halimpati mwewe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…