Kiwango cha chini cha elimu ya diwani iwe diploma

Prezidah

JF-Expert Member
Joined
Feb 1, 2013
Posts
750
Reaction score
182
Ni Furahi Daya WanaJF!!

chonde chonde naomba sana wale watakaoteuliwa kuunda Bunge la Katiba wazingatie vigezo vya mtu kuwa diwani at least isipungue Diploma na Mwenyekiti wa Halamashauri lazima awe na Digrii. Nasema hivi kwa sababu madiwani wamepewa mamlaka makubwa kikatiba (current) kusimamia halmashauri lakini kutokana na elimu ndogo wamekuwa kikwazo cha maendeleo kazi kuomba posho tu na kufukuza wakurugenzi pale wanapokuwa strict.
 
Hivi niulize kuna kikomo cha kiwango cha elimu kwa wabunge au mtu anaetaka kugombea
 
Hivi niulize kuna kikomo cha kiwango cha elimu kwa wabunge au mtu anaetaka kugombea

mkuu hata darasa ni wabunge in short hakuna kikomo but concern yangu iko na madiwani ingawa naunga mkono kikomo kiwepo na kwao pia
 
Hapana, kusiwe na mahitaji ya viwango vya elimu kwa wanaogombea nafasi za kisiasa. Kufanya hivyo kunasababisha utitili w Ph.D za kununua; badala yake ningeshauri kuwa na usaili wa awali kabla candidacy ya mtu haijapita. Iwekwe bodi ya wanazuoni kuwasaili watu hawa katika nyanja tofauti tofauti ili kupima upeo wao kabla hawajakubaliwa kuwa wagombea (Candidates).
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…