Kiwango cha chini cha mshahara VPL 2014/15: Azam-1.5ml, Yanga na Simba-laki tatu

Kiwango cha chini cha mshahara VPL 2014/15: Azam-1.5ml, Yanga na Simba-laki tatu

Yethero Mgale

JF-Expert Member
Joined
Apr 19, 2012
Posts
525
Reaction score
228
Katika ligi ya vodacom ya 2014/15, Azam ndiyo timu inayoongoza kwa kuwalipa masilahi mazuri wachezaji wake kwani wachezaji wanaopokea mshahara mzuri kwa mwezi ni Kipre na Herman Tchetche ambao ni 4 mil kwa mwezi na anayepokea kiwango cha chini ni 1.5 kwa mwezi.
Wakati Yanga ni 3.6 mil kwa kiwango cha juu na laki 3 kwa chini.
Simba ni 3mil kwa laki 3

Source: RFA
 
Unaujua mshahara wa kpah sherman!!
Mshahara wa Andrey Coutinho unaujua?!
Mshahara wa Emmanuel Okwi je?!

Hao RFA wamedanganya, na wewe mtoa post pia muongo.
 
Mkuu hizi figure siyo static, zinabadilika kwa sababu moja au nyingine ikiwemo sababu ya mkataba. Sasa wewe unakuja kupinga kama umekurupushwa pasina kutoa huo unaouita ukweli. Kajipange
 
Hiyo mitimu yenyewe haina hata viwanja vya mazoezi ni bora hata wawe wanawapata wachezaji wa kuwalipa sh.30,000/= kwa mwezi kuliko kufanya anasa wakati hata viwanja hawana ni aibu mitimu ina miaka zaidi ya 80+ hazina hata viwanja wanachojua wao ni misifa tu
 
Azam waache wawalipe wachezaji vyovyote wanavyotaka, Yanga ni bingwa bila kujali wachezaji wanalipwaje! Sina data kamili za mishahara ya wachezaji kama Niyonzima, Sherman na wengineo, ninachokiona kuwa kiwango cha 4m/- kwa Azam na 3.6m/- kwa Yanga si sahihi.
 
Emannuel Okwi analipwa USD 3000 kwa mwezi, ambazo ni zaidi ya 6 milioni.
Kuhusu Simba kulipa laki tatu ni sawa, na hizo hua ni kwa wale wachezaji wanaopandishwa toka timu za vijana.. akipafomu vizuri hupongezwa kwa kupewa mikataba minono, mf. Mkude, Isihaka na Ndemla. Hii inawafanya wajitahidi sana.
 
Back
Top Bottom