Kiwango cha mshahara wa wakuu wa idara

Trubetzkoy

JF-Expert Member
Joined
Oct 31, 2018
Posts
349
Reaction score
678
Habari ndugu watanzania. Ni imani yangu kuwa mu buheri wa afya.

Katika mfumo wa uongozi wa elimu huwa kuna afisa elimu (mkoa, wilaya) ambapo chini yake wanakuwepo wakuu wa idara mbalimbali mfano, idara ya taaluma (afisa elimu taaluma), idara ya takwimu (afisa elimu takwimu) etc.

Naomba kujua kiwango cha mshahara wanachopata hawa watu. Pia ningependa kufahamu upatikanaji wa hivi vyeo, ni mamlaka ipi inayohusika na uteuzi wa hawa watu?

Msaada tafadhali.
 
Omba kujua kwanza idara zilizopo ktk taasisi hizo ili ujue kama hao uliotaja ni wakuu wa idara au la, asante
 
Hakuna Kiwango cha mshahara kwa mkuu wa Idara Bali watu hulipwa kwa ngazi ya mshahara kulingana na sifa zake kitaaluma/kitaalam. Ukuu wa Idara Ni uteuzi/temporary
Ukiwa mkuu wa idara halmashauri unachukua m3.

#MaendeleoHayanaChama
 
Hakuna Kiwango cha mshahara kwa mkuu wa Idara Bali watu hulipwa kwa ngazi ya mshahara kulingana na sifa zake kitaaluma/kitaalam. Ukuu wa Idara Ni uteuzi/temporary
Wanateuliwa na nani?
 
Mkuu wa Idara wa Halmshauri hulipwa 3.4 million maana ni scale ya LSEE Ila hawa wa chini yake mfano afisa elimu taaluma sio wakuu wa Idara na Wana scale ya mshahara wa kawaida tuu kama walimu wengine Ila Wana advantage ya seminar, workshop's, training, Extra duty , perdiem
 
Utofauti wao ukoje mkuu wa idara na afisa elimu taaluma?
 
Dah ila serikalini bhana...mi private sector hiyo salary nilikuaga napata 6 years ago kama net salary. Gross ilikua 5 na tulikua tunaona normal
 
Hao wachini wote hupokea mishahara ya walimu kulingana na daraja lake. Hakuna maajabu chagua CCM mwalimu utaisoma namba
 
Mkuu nenda kazini UKIONA hailipi unatoka sio lamza kwan
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…