Kiwango cha ulaji wa mayai nchini kwa mtu mmoja kwa mwaka kimeshuka kutoka mayai 300 hadi mayai 106

Nyendo

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2017
Posts
1,336
Reaction score
4,731
Kiwango cha ulaji wa mayai nchini kwa mtu mmoja kwa mwaka kimeshuka kutoka mayai 300 hadi mayai 106.

Kauli hiyo imetolewa jana Oktoba 17, 2021 na Waziri wa kilimo, Profesa Adolf Mkenda wakati akifunga maadhimisho ya kilele cha siku ya chakula duniani iliyofanyika kitaifa mkoani Kilimanjaro.

"Ulaji wa mayai nchini kwa mtu kwa mwaka ni mayai 106 ,kiwango hiki ni cha chini ukilinganisha na kiasi kinachopendekezwa ambacho ni mayai 300 kwa mtu kwa mwaka," amesema Profesa Mkenda. Soma hapa:Watanzania hawali nyama na kunywa maziwa inavyotakiwa.

Profesa Mkenda amesema walaji wa mayai ni wale wenye kipato cha juu na cha kati ambapo wengi wao ni waliopo maeneo ya mijini na vyuoni.

Amesema pamoja na kiwango ulaji wa mayai kuwa chini, uzalishaji wake umeongezeka kutoka bilioni 3.58 kwa mwaka 2019/20 hadi 4.5 kwa mwaka 2020/21 sawa na ongezeko la asilimia 26.

Profesa Mkenda amesema ongezeko hilo la uzalishaji linatokana na kuongezeka kwa vituo vya kutotoleshea vifaranga vya kuku kutoka vituo 26 kwa mwaka 2019/20 hadi vituo 28 kwa mwaka 2020/21 na wananchi wamehamasika katika kufuga kuku.

"Nawasihi wafugaji na wakulima muendelee kujifunza teknolojia mbalimbali ambazo zinaweza kuongeza uzalishaji wa mayai hapa nchni,"amesema Profesa Mkenda
 
Kwa kipato gani walichonacho Watanzania wengi hadi waweze kula mayai? Mlo mmoja tu kwa Watanzania wengi ni mgogoro mkubwa halafu wafikirie eti kula mayai? 😳
 
Ujinga huwa ni kuchukua jumla ya uzakishaji wa mayai kwa mwaka na kugawa kwa idadi ya watu[emoji28][emoji28][emoji28]

Bila kujua kuna wanaume wa Kinondoni DSM na Buza wanakula mayai 960 kupitia kiepe yai kila siku[emoji1550][emoji1550], na wengine kama mimi na mzee wangu hatuli maana hatuyapendi.
 
Najaribu kuwaza wakati huo watu wanakula mayai 300 kwenye sehemu zenye misongamano hali ilikuwaje...
 
Hapo ni rahisi tu kugundua shida ipo wapi kama uzalishaji umepanda halafu utumiaji umeshuka at ceteris peribus basi shida ni kipato

Kwamba kwa kuwa kipato kimepungua basi watu wameamua kuacha kutumia mayai
 
Kiwango cha ulaji wa mayai nchini kwa mtu mmoja kwa mwaka kimeshuka kutoka mayai 300 hadi mayai 106.

Kauli hiyo imetolewa jana Oktoba 17, 2021 na Waziri wa kilimo, Profesa Adolf Mkenda wakati akifunga maadhimisho ya kilele cha siku ya chakula duniani iliyofanyika kitaifa mkoani Kilimanjaro.

"Ulaji wa mayai nchini kwa mtu kwa mwaka ni mayai 106 ,kiwango hiki ni cha chini ukilinganisha na kiasi kinachopendekezwa ambacho ni mayai 300 kwa mtu kwa mwaka," amesema Profesa Mkenda. Soma hapa:Watanzania hawali nyama na kunywa maziwa inavyotakiwa.

Profesa Mkenda amesema walaji wa mayai ni wale wenye kipato cha juu na cha kati ambapo wengi wao ni waliopo maeneo ya mijini na vyuoni.

Amesema pamoja na kiwango ulaji wa mayai kuwa chini, uzalishaji wake umeongezeka kutoka bilioni 3.58 kwa mwaka 2019/20 hadi 4.5 kwa mwaka 2020/21 sawa na ongezeko la asilimia 26.

Profesa Mkenda amesema ongezeko hilo la uzalishaji linatokana na kuongezeka kwa vituo vya kutotoleshea vifaranga vya kuku kutoka vituo 26 kwa mwaka 2019/20 hadi vituo 28 kwa mwaka 2020/21 na wananchi wamehamasika katika kufuga kuku.

"Nawasihi wafugaji na wakulima muendelee kujifunza teknolojia mbalimbali ambazo zinaweza kuongeza uzalishaji wa mayai hapa nchni,"amesema Profesa Mkenda
Kuna mtu atakuwa anakula mayai yangu kwani mwaka huu siijakula yai hata moja
 
Kwa kipato gani walichonacho Watanzania wengi hadi waweze kula mayai? Mlo mmoja tu kwa Watanzania wengi ni mgogoro mkubwa halafu wafikirie eti kula mayai? [emoji15]
Kwanza Kipato hakitatosha. Itkawaje kwa familia ya watu watani, e.g Baba, mama.na Watoto watatu?
Halafu mayai yenyewe haya ya Kuku wa Kizungu??
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
JAMANI MTANISAMEHE. LABDA MIMI NI MJINGA. NAOMBA KUULIZA. HIVI WEWE MWANAUME UNAWEZAJE KULA MAYAI? UNATAKA UWEJE? HIVI UNAMUONAJE mwanaume ANAYEKULA MAYAI, NA MWANAUME ANAYEKULA MIHOGO. AH. NAOMBA NIISHIE HAPA
 
Jamani huo muda wa kula mayai mnautoa wapi? Mbona watanzania tunaendekeza na kupenda anasa. Nchi bado kabisa katika kila nyanja tumebaki kuendekeza anasa tu kula kula tu.
 
Mwandishi hakumuelewa Mh. Waziri. Hi nchi hatujawahi kuwa na wastani wa ulaji mayai 300. Hayo ni mapendekezo ya wazungu.
 
Ni mjinga, umesamehewa.
JAMANI MTANISAMEHE. LABDA MIMI NI MJINGA. NAOMBA KUULIZA. HIVI WEWE MWANAUME UNAWEZAJE KULA MAYAI? UNATAKA UWEJE? HIVI UNAMUONAJE mwanaume ANAYEKULA MAYAI, NA MWANAUME ANAYEKULA MIHOGO. AH. NAOMBA NIISHIE HAPA
 
JAMANI MTANISAMEHE. LABDA MIMI NI MJINGA. NAOMBA KUULIZA. HIVI WEWE MWANAUME UNAWEZAJE KULA MAYAI? UNATAKA UWEJE? HIVI UNAMUONAJE mwanaume ANAYEKULA MAYAI, NA MWANAUME ANAYEKULA MIHOGO. AH. NAOMBA NIISHIE HAPA
Tofauti Ni kwamba Cha mayai kinanuka,Cha mihogo chenyewe Ni shega tu.
 
Back
Top Bottom