De Opera
JF-Expert Member
- May 23, 2013
- 780
- 1,664
Wakati tukiinyoshea Yanga kidole na kuituhumu kuwa kiwango kimeshuka basi, tusiisahau Simba pia. Tunajua Simba inaonekana kwa sababu Yanga anafanya vibaya. Simba inapata matokeo ambayo ni mpaka mtu ashike roho hadi mpira umalizike ndio aiachie. Ukiondoa mechi za ligi kuu.
Kwa kundi la CC alilopo Simba angekuwepo Yanga, Yanga angekuwa anaongoza kundi kwa points zote haijalishi stuation aliyo nayo sahivi. Zile timu zote ni vibonde kwa aina za uchezaji zilizoonesha hadi sasa na jinsi class ya Simba ilivyo.(Nipigeni mawe) 😁
Kinachoiangusha Yanga ni upungufu wa Saikolojia.
Tunaangalia gemu za CC alizocheza Simba. Kashinda kwa tabu, kapigwa kizembe. Simba hajakutana na timu ngumu.
Simba angekutana na Tp Mazembe, angekula si chini ya goli 2.
Simba angekutana na Mc Alger, angekula si chini ya goli 3.
Kocha wa Simba ni mzuri ila kwa wakati huu tu wa upepo. Ukitaka kujua, angalia subs anazofanya katika matarajio ambayo anapaswa kufanya sub za aina gani.
Kingine ni Wachezaji wa Simba hawajakumbushwa kutafuta kwanza goli, ubinafsi uje tukiwa tunaongoza magoli ya kutosha. Kila mchezaji anacheza kama anatafuta maisha yake mwenyewe.
Streika wa Simba wanaonekana hawana maana kwa sababu ya kirusi cha namba 10. Kinaangalia goli zaidi badala kiangalie nani kapita nimpe (Penetration pass).
Kagoma ni mchezaji ambaye sio poa kumuanzia nje kwa sababu ni mchezaji ambaye si mtu wa ku- label sana. Huyu huwa namuita mzee wa kuwagombansha(Gombania goli) zile krosi zake mara nyingi zimekuwa na faida kuliko za kapombe ambaye aidha zimgonge mpinzani na mpira utoke nje.
Mimi nimeona hivo, kwani wewe umeonaje? Eti mpwa?
#Ubaya_Ubwela #Simba_sc #Yanga
Mimi ni ubaya Ubwela, mwiko waachie wavuvi. 😄