Kiwanja cha ukubwa wa miguu 20 kwa 20 je kinatosha kwa plan hii?

Kiwanja cha ukubwa wa miguu 20 kwa 20 je kinatosha kwa plan hii?

Mi
Wakuu habarini za majukumu?

Kama kichwa cha habari kinavosema je kwa ukubwa wa kiwanja hicho naweza jenga nyumba ya vyumba vinne kimoja masta public toilet pamoja na store kisha nikapata nafasi ya kuchumbia kisima kirefu pamoja na parking?

Naomba kuwasilisha kwenu 🙏
Miguu ya 20 kwa 20 nyie mnaotoa ushauri mmeelewa ni sawa na Mita ngapi?
 
Ukijenga nyumba ya 10m kwa 15m umapata nyumba kubwa tu cheki na wataalam
 
Kinatosha, isipokuwa nafasi itayobaki itakuwa finyu pengine pande mbili hadi tatu...
 
Siwezi kusema kinatosha au hakitoshi bila kuona ramani ya nyumba unayotaka kujenga.
Nyumba inaweza kuwa navyumba vinne ila nyumba hiyo ikawa ndogo kwa nyumba ya vyumba viwili.
 
Miguu 20 kwa 20 ni kidogo mnoo mkuu, tofautisha miguu kwa METER, zingekuwa ni meter 20 kwa 20 kingetosha bila tabu.
 
Wakuu habarini za majukumu?

Kama kichwa cha habari kinavosema je, kwa ukubwa wa kiwanja hicho naweza jenga nyumba ya vyumba vinne kimoja masta public toilet pamoja na store kisha nikapata nafasi ya kuchimba kisima kirefu pamoja na parking?

Naomba kuwasilisha kwenu 🙏
Kinatosha sana
 
Watu wanashindwa kutofautisha miguu 20 na mita 20, 20mx20m ni kiwanja kikubwa tu, yaani 400sq.m, ukijenga nyumba ya wastani wa 160sq.m unabakiwa na eneo kubwa sana.

Lakini miguu 20x20 ni size ya kawaida sana, ukijenga 150sq.m kinachobaki hapo hata sio eneo kubwa sana.
 
Hakitoshi

Jenga two master bedrooms sitting room, corridor ndogo na one small room.

nje shimo kubwa, choo cha nje, jiko na store, utabaki na kasehemu ka kuotea jua
 
Miguu 20 sio sawa na 20meter, kanunue measuring tape ni chini ya buku 10 tu, kapime uwe unaongea na vipimo vya uhakika.
 
Wakuu habarini za majukumu?

Kama kichwa cha habari kinavosema je, kwa ukubwa wa kiwanja hicho naweza jenga nyumba ya vyumba vinne kimoja masta public toilet pamoja na store kisha nikapata nafasi ya kuchimba kisima kirefu pamoja na parking?

Naomba kuwasilisha kwenu

Kinatosha bila shaka yyte wala usipate wasiwasi....kiwanja mita 20 kwa 20 maana yake ni 400sqm ni kiwanja standard kabisa....siongei kwa ushabiki bali mm nadesign raman na kusimamia ujenzi...km hatua ni kubwa za mtu mzima bs wanasema ni sawa na mita tu.
 
Attachments

  • FB_IMG_1656268797329.jpg
    FB_IMG_1656268797329.jpg
    42.7 KB · Views: 165
Back
Top Bottom