Kiwanja hatua 15x15 kinatosha nyumba ya vyumba vitatu na sebule na choo?

Kitatosha vyumba vitatu tuh kwa ukubwa wa hatua 5 kila chumba
 
Habari za jioni ndugu zangu,

Naomba kuuliza kiwanja chenye ukubwa wa 15x15 kinaweza kutosha nyumba ya vyumba vitatu sebule jiko na choo Kwa wanaojua naombeni msaada mnijulishe wadau maana Kuna sehemu nataka nianze ujenzi
Jenga nyumba kwa kwenda juu.Usiisambaze kama unaanika udaga kwenye jiwe Wanyaturu wanaita ng'ongo.Itatosha hadi vyumba 7000.
 
Habari za jioni ndugu zangu,

Naomba kuuliza kiwanja chenye ukubwa wa 15x15 kinaweza kutosha nyumba ya vyumba vitatu sebule jiko na choo Kwa wanaojua naombeni msaada mnijulishe wadau maana Kuna sehemu nataka nianze ujenzi
Minimum size ya chumba NI sq 12 (4*3=12), hivyo vyumba 3 Sawa na 36sqm, sebule minimum size 5*um =28sqm, bafu 2.5*3m=7.5sqm, dining 4.5.*4=18sqm , minimum, kitaalamu ni small size, But not recommended much, weka parking, ya magari3, 30sqm. Weka chemba na Sehem ya maji ..16dqm, nk alafu Kumlisha hizo, then Toa kwenye 225sqm. Ila nashauri Tumia MEDIUM SIZE ROOM. sio small size
 
Akirudi na swali apigwe makwenzi.
 
Kama ni mita hapo ni 225sqm. Viwanja vingi vya Sinza ni 225sqm na kuna nyumba na parking ya gari moja. Hata Mikocheni kuna viwanja hivyo vya 225sqm.
 
Pima kwa tape measure uje nikupe ushauri nyumba itakayotosha apo nkuchoree na ramani yake
0759009331
 
Labda utoe ramani ya kaghorofa, chini sebule, dining, jiko, store ndogo,chumba kimoja na public toilet, then juu vyumba vitatu master vyote. Hapo utabalance nafasi.
 
Hii setting akiibadili ikawa ghorofa atakuwa amecheza kweli. Unajua ghorofa zinasave sana space na kuweka muonekano mzuri sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…