Nadhani Maxence Melo atakuwa na jibu zuri kwa swali hili
Mhhh Sinkala...
Yo Yo, ninachoweza kukusaidia kwa haraka naona hakina tofauti na wengi lakini huenda kikawa na mchango kwa kiwango flani kuelekea unachokitafuta.
Kama unatafuta Kiwanja Dar kama walivyokwambia wengi ni kwamba kuna walanguzi kibao.
Viwanja visivyopimwa kwa Dar ni risk sana na vina bei za kubambikiza sana. Vilivyopimwa vingi vipo mikononi mwa wajanja wachache lakini bei zao ni reasonable na transfer ndiyo inakuchukua muda endapo unahitaji kuharakisha mchakato.
Binafsi nilinunua kiwanja (2,005m2) last two years kwa Tshs 5,000,000 lakini toka kwa ambaye alikwisha kinunua toka serikalini.
Bei kwa atleast 1,500m2 za kiwanja kilichopimwa ipo kati ya 6mil - 10mil (Tshs). Lakini bei hiyo inategemeana na maeneo... Usitarajie bei hiyo upewe Masaki au Mbezi Beach ama Magomeni etc. Ni bei za viwanja vilivyopimwa pembeni mwa mji. Unaweza kubahatika ukapata hata kwa 4mil kiwanja cha size hiyo.
Endapo utakuwa serious niandikie barua pepe nami nikuunganishe na jamaa ambaye najua ana viwanja vinne tayari nawe utaelewana naye directly au ukihitaji nishiriki negotiation yenu naweza kukupa kampani.
Nyumba uliyoweka inaweza kujengwa kwa viwango vizuri sana kwa Tshs 300,000,000 (endapo materials zilizotumika ni za standard ya kati na hutumii parquet flooring system na wala huongezi Swimming pool).
Kuna members humu ni Professionals wa kuchora naweza kuwasihi pembeni wakusaidie michoro (ila najua gharama zao ziko juu) au hata ushauri wakati wa kujenga.
Mengine ni baada ya kuwa na kiwanja mkuu.