Kiwanja,Nyumba Dar es salaam

Kiwanja,Nyumba Dar es salaam

Nimenunua kiwanja wazo mwaka jana aprili, nilinunua kwa mtu aliyekichukua serikalini aliniuzia kwa mil 7.5, ni 1,500m2
 
gharama za ujenzi pia hutegemea kama wewe mwenyewe ndio unasimamia
au wewe upo nje ya nchi na unatuma pesa kwa jamaa na yeye ndio
anasimamia. napenda kuamini kwamba (na nemeona kwa wengi) wale wanaotuma pesa za ujenzi gharama zao huwa juu sana kuliko wale
wanaosimamia wenyewe. hivyo ukiambiwa nyumba ni milioni 250 basi
kama upo nje ya nchi wewe kadiria millioni 400 au zaidi :-(
 
Tahadhali,kigamboni imeshauzwa ile,labda kama ni kibada/Tua ngoma. Mji mwema ni noma sana kwa usalama na bei. Kuanzia Kibada kwenda Mwasonga kupitia Kisarawe II hadi Dsm zoo ni ukanda wa hatari kwa sasa kwa viwanja visivyopimwa. Habari za mitaani zinasema kigamboni city inakuja kujengwa ukanda huo.

Kama una mtu wa kukusaidia kupata kiwanja basi mji mpya wa Kinyerezi/Kifuru ni pazuri. Viwanja vimepimwa,hewa safi na sio Uswazi kwa sasa. Ndo eneo ambalo linakuja kwa kasi sana kwa ujenzi na makazi mazuri.
 
Mhhh Sinkala...

Yo Yo, ninachoweza kukusaidia kwa haraka naona hakina tofauti na wengi lakini huenda kikawa na mchango kwa kiwango flani kuelekea unachokitafuta.

Kama unatafuta Kiwanja Dar kama walivyokwambia wengi ni kwamba kuna walanguzi kibao.

Viwanja visivyopimwa kwa Dar ni risk sana na vina bei za kubambikiza sana. Vilivyopimwa vingi vipo mikononi mwa wajanja wachache lakini bei zao ni reasonable na transfer ndiyo inakuchukua muda endapo unahitaji kuharakisha mchakato.

Binafsi nilinunua kiwanja (2,005m2) last two years kwa Tshs 5,000,000 lakini toka kwa ambaye alikwisha kinunua toka serikalini.

Bei kwa atleast 1,500m2 za kiwanja kilichopimwa ipo kati ya 6mil - 10mil (Tshs). Lakini bei hiyo inategemeana na maeneo... Usitarajie bei hiyo upewe Masaki au Mbezi Beach ama Magomeni etc. Ni bei za viwanja vilivyopimwa pembeni mwa mji. Unaweza kubahatika ukapata hata kwa 4mil kiwanja cha size hiyo.

Endapo utakuwa serious niandikie barua pepe nami nikuunganishe na jamaa ambaye najua ana viwanja vinne tayari nawe utaelewana naye directly au ukihitaji nishiriki negotiation yenu naweza kukupa kampani.

Nyumba uliyoweka inaweza kujengwa kwa viwango vizuri sana kwa Tshs 300,000,000 (endapo materials zilizotumika ni za standard ya kati na hutumii parquet flooring system na wala huongezi Swimming pool).

Kuna members humu ni Professionals wa kuchora naweza kuwasihi pembeni wakusaidie michoro (ila najua gharama zao ziko juu) au hata ushauri wakati wa kujenga.

Mengine ni baada ya kuwa na kiwanja mkuu.
Nashukuru sana mkuu Max kwa a very useful infor mkuu,ubarikiwe.......
Location ni muhimu sana. Lakini currently viwanja vinapatikana maeneo ya Wazo, Kigamboni, Mji Mwema, Chanika/Pugu, Bunju, Mwanagati & Majohe. Maeneo mengine labda nimwulize jamaa wa Ardhi kwa usahihi zaidi.
Mkuu tatizo ni kwamba bongo kila mtu mjanja unaweza kulizwa hivi hivi nilisikia viwanja Kigambonino na mji mwema lakini watu walilizwa nasikia,kama ulivyosema kuulizia jamaa wa ardhi umenena.....Ngoja nilonge na mdau mmoja alafu nitakutafuta..
 
Kuna viwanja maeneo ya Wazo ambayo bei zake sio mbaya sana na hapaja kaa kiuswahili sana. Vimepimwa na wizara ya ardhi. Vina hati tayari.
Kama utapenda wewe nenda kaviangalie halafu utakuwa na wigo mpana zaidi wa kuchagua maeneo yatakoyo kufahaa.
 
Ninachoweza kukushauri tafuta mchoraji (Architect) akuchoree ili uweze pata nyumba unayoiihitaji pia kabla ya kuanza tafuta mkadiriaji gharama (Quantity Surveyor) ili akupe gharama halisi kabla ya kuanza. ikiwezekana tafuta wote wawili uwape budget yako ili design isivuke hapo usije ishia kwenye paa.

ni muhimu kujua gharama kabla ya kuanza ujenzi kuepuka kuwahisi mafundi wanakufanyia ufisadi.
 
Kuna viwanja maeneo ya Wazo ambayo bei zake sio mbaya sana na hapaja kaa kiuswahili sana. Vimepimwa na wizara ya ardhi. Vina hati tayari.
Kama utapenda wewe nenda kaviangalie halafu utakuwa na wigo mpana zaidi wa kuchagua maeneo yatakoyo kufahaa.

Samahani hivi viwanja vinauzwa na ardhi au watu walishavinunua? Na inabidi ninunue kwao?

Njimba
 
Samahani hivi viwanja vinauzwa na ardhi au watu walishavinunua? Na inabidi ninunue kwao?

Njimba

Wizara haiuzi viwanja isipokuwa unapewa kama ni haki yako kwa kuwa ni mwananchi unatakiwa ulipe vifuatavyo

Fees for certificate of Occupancy
Registration Fees
Survey Fees
Deed Plan Fees
Stamp Duty on Certificate and Duplicate
Land Rent

Fees nilizotaja hapo unalipia mara moja isipokuwa Land Rent utakuwa unalipia kila mwaka.
 
Haya Mkuu,
Unajua kama uswazi hakukufai itakubidi uende masafa sana kule kunakoitwa Mbezi-Msumi kunakufaa sana.Kiwanja Medium density unajikatia kwa 5Mil/=tu. Gharama ya kujena Mkuu kama utaezeka kigae cha bongo ni kama taslimu 35Mil/=Kama kigae cha Sauzi na tile ya Spain BASI tenga 105Mil/= tu.Hata hivyo nina ushauri wa bure endapo utapiga kwenye kilonga longa changu Voda saba tano nne mbili sita moja nane sifuri tatu.Piga asubuhi au jioni.
 
Wizara haiuzi viwanja isipokuwa unapewa kama ni haki yako kwa kuwa ni mwananchi unatakiwa ulipe vifuatavyo

Fees for certificate of Occupancy
Registration Fees
Survey Fees
Deed Plan Fees
Stamp Duty on Certificate and Duplicate
Land Rent

Fees nilizotaja hapo unalipia mara moja isipokuwa Land Rent utakuwa unalipia kila mwaka.

Ahsante kwa kunielewesha.

Sasa ngoja turudi kwenye swali langu la msingi, ngoja labda niliulize kam ifuatavyo, utaratibu wa kuvipata hivi viwanja ukoje? Unaenda ardhi? Au sehemu gani?

Ahsante
 
Hii inflation ya bei za viwanja bongo, nataka kuamini kuwa ililetwa na mihela ya ufisadi wa kati 2004 - 2007, maana kipindi hichi bei zilipanda sana, kuna jamaa 2006 alinunua kiwanja mbezi beach 15m, halafu akakiuza within a month kwa 60m.

Hii barabara mpya ya lami mbezi kawe kwenda whitesands imepandisha sana bei za property mbezi africana. Lakini ukiwa na 50m-70m mkononi unapata kiwanja cha 1200msq(30x40)mbezi africana/bahari beach. Depending na location(accesibility, corner plot, fenced or not). Plot kubwa zaidi itabidi ujifungashe na kuanzia 70m mpaka za 250m zipo.

Maeneo ya mbweni(mbele ya tegeta upande wa baharini) ambayo ni mazuri na hewa safi, ukitenga 25m- 35m unapata kiwanja cha 1200msq...ila hizi bei hazipo stable kabisa. Na wakati mwingine zinaangalia mtu. Ukipaki rangerover vogue ofcourse jamaa wanaanzia mbali na wanakua wagumu kushuka.
 
Haya Mkuu,
Unajua kama uswazi hakukufai itakubidi uende masafa sana kule kunakoitwa Mbezi-Msumi kunakufaa sana.Kiwanja Medium density unajikatia kwa 5Mil/=tu. Gharama ya kujena Mkuu kama utaezeka kigae cha bongo ni kama taslimu 35Mil/=Kama kigae cha Sauzi na tile ya Spain BASI tenga 105Mil/= tu.Hata hivyo nina ushauri wa bure endapo utapiga kwenye kilonga longa changu Voda saba tano nne mbili sita moja nane sifuri tatu.Piga asubuhi au jioni.

mlinganisho wako sio sahihi sana. hujasema size ya hiyo nyumba, pia spain tiles na SA tiles za paa silete tofauti ya kutoka 35m hadi 105m!! nadhani unaweza ukampa muongozo usio sahihi, angalia ujenzi mzima kwa undani
 
Ahsante kwa kunielewesha.

Sasa ngoja turudi kwenye swali langu la msingi, ngoja labda niliulize kam ifuatavyo, utaratibu wa kuvipata hivi viwanja ukoje? Unaenda ardhi? Au sehemu gani?

Ahsante

Unaanzia kwenye Municipal Council zetu iwe Temeke, Kinondoni au Ilala. Unapeleka maombi yako huko inategemea na viwanja walivyokwisha kupima kama watakuwa navyo kwani maombi ni mengi kuliko mahitaji ya wananchi.
 
1.Ni sehemu gani nzuri zenye nafasi ambazo sio uswzi sana pazuri kwa kujenga?

SEHEMU NZURI NI BUNJU B, VIWANJA VYA MRADI 20,000, MBWENI, KIGAMBONI KARIBU NA BAHARI, ILA BUNJU B KWENYE VIWANJA VILIVYOPIMWA NDIO POA.

2.Kiwanja low density bei gani?

KULE KWA KIWANJA CHA HATUA KWA UPANA 35 KWA 25 NI 10-15M/=. LOW DENSITY INA MAANA SEHEMU ZENYE VIWANJA VISIVYOBABANANA, AMBAPO BUNJU B NDIO KULIVYO, ILA IO MILIONI 10 AU 15 NI KWAMBA UNAMVUA MTU KIWANJA, SERIKALINI VILIUZWA KAMA MILIONI 2 TU!

3.Na estimation ya kujenga nyumba yenye kufanana na hii ni kama Tsh ngapi?
IO NYUMBA SIJAIONA, ILA ESTIMATES ZA KUJENGA NYUMBA YENYE VYUMBA 4, MASTER, STORE AND PUBLIC TOILET INCLUDED INAWEZA KUKUGHARIMU SIO CHINI YA MILIONI 60-70!
KAMA UKIONGEZA NA SERVANTS QUARTER YA VYUMBA 2, CHOO NA BAFU INAWEZA KUONGEZEKA MPAKA MILIONI 90!
 
Back
Top Bottom