Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Nashukulu mkuu maxence.
Je maendeo hayo mengine niliyokoleza kwa rangi nyekundu, ulioyataja wewe, estimate ye kiwanja mf heka moja, ni kiasi gani fa fedha?
Asante
Nashukuru sana mkuu Max kwa a very useful infor mkuu,ubarikiwe.......Mhhh Sinkala...
Yo Yo, ninachoweza kukusaidia kwa haraka naona hakina tofauti na wengi lakini huenda kikawa na mchango kwa kiwango flani kuelekea unachokitafuta.
Kama unatafuta Kiwanja Dar kama walivyokwambia wengi ni kwamba kuna walanguzi kibao.
Viwanja visivyopimwa kwa Dar ni risk sana na vina bei za kubambikiza sana. Vilivyopimwa vingi vipo mikononi mwa wajanja wachache lakini bei zao ni reasonable na transfer ndiyo inakuchukua muda endapo unahitaji kuharakisha mchakato.
Binafsi nilinunua kiwanja (2,005m2) last two years kwa Tshs 5,000,000 lakini toka kwa ambaye alikwisha kinunua toka serikalini.
Bei kwa atleast 1,500m2 za kiwanja kilichopimwa ipo kati ya 6mil - 10mil (Tshs). Lakini bei hiyo inategemeana na maeneo... Usitarajie bei hiyo upewe Masaki au Mbezi Beach ama Magomeni etc. Ni bei za viwanja vilivyopimwa pembeni mwa mji. Unaweza kubahatika ukapata hata kwa 4mil kiwanja cha size hiyo.
Endapo utakuwa serious niandikie barua pepe nami nikuunganishe na jamaa ambaye najua ana viwanja vinne tayari nawe utaelewana naye directly au ukihitaji nishiriki negotiation yenu naweza kukupa kampani.
Nyumba uliyoweka inaweza kujengwa kwa viwango vizuri sana kwa Tshs 300,000,000 (endapo materials zilizotumika ni za standard ya kati na hutumii parquet flooring system na wala huongezi Swimming pool).
Kuna members humu ni Professionals wa kuchora naweza kuwasihi pembeni wakusaidie michoro (ila najua gharama zao ziko juu) au hata ushauri wakati wa kujenga.
Mengine ni baada ya kuwa na kiwanja mkuu.
Mkuu tatizo ni kwamba bongo kila mtu mjanja unaweza kulizwa hivi hivi nilisikia viwanja Kigambonino na mji mwema lakini watu walilizwa nasikia,kama ulivyosema kuulizia jamaa wa ardhi umenena.....Ngoja nilonge na mdau mmoja alafu nitakutafuta..Location ni muhimu sana. Lakini currently viwanja vinapatikana maeneo ya Wazo, Kigamboni, Mji Mwema, Chanika/Pugu, Bunju, Mwanagati & Majohe. Maeneo mengine labda nimwulize jamaa wa Ardhi kwa usahihi zaidi.
Kuna viwanja maeneo ya Wazo ambayo bei zake sio mbaya sana na hapaja kaa kiuswahili sana. Vimepimwa na wizara ya ardhi. Vina hati tayari.
Kama utapenda wewe nenda kaviangalie halafu utakuwa na wigo mpana zaidi wa kuchagua maeneo yatakoyo kufahaa.
Samahani hivi viwanja vinauzwa na ardhi au watu walishavinunua? Na inabidi ninunue kwao?
Njimba
Wizara haiuzi viwanja isipokuwa unapewa kama ni haki yako kwa kuwa ni mwananchi unatakiwa ulipe vifuatavyo
Fees for certificate of Occupancy
Registration Fees
Survey Fees
Deed Plan Fees
Stamp Duty on Certificate and Duplicate
Land Rent
Fees nilizotaja hapo unalipia mara moja isipokuwa Land Rent utakuwa unalipia kila mwaka.
Haya Mkuu,
Unajua kama uswazi hakukufai itakubidi uende masafa sana kule kunakoitwa Mbezi-Msumi kunakufaa sana.Kiwanja Medium density unajikatia kwa 5Mil/=tu. Gharama ya kujena Mkuu kama utaezeka kigae cha bongo ni kama taslimu 35Mil/=Kama kigae cha Sauzi na tile ya Spain BASI tenga 105Mil/= tu.Hata hivyo nina ushauri wa bure endapo utapiga kwenye kilonga longa changu Voda saba tano nne mbili sita moja nane sifuri tatu.Piga asubuhi au jioni.
Ahsante kwa kunielewesha.
Sasa ngoja turudi kwenye swali langu la msingi, ngoja labda niliulize kam ifuatavyo, utaratibu wa kuvipata hivi viwanja ukoje? Unaenda ardhi? Au sehemu gani?
Ahsante