Kiwewe kizito chawakumba walioshiriki au kushirikishwa katika jaribio la kigaidi la kumuua Mh. Tundu Antiphas Lissu!

Kiwewe kizito chawakumba walioshiriki au kushirikishwa katika jaribio la kigaidi la kumuua Mh. Tundu Antiphas Lissu!

Wewe humu jf kutwa unadhihaki watu Dua gani utatuma liwapate waliopewa nguvu na Mungu kuongoza Taifa? Mnafikiri kuongoza nchi ni sawa na Kuongoza Familia... Ajari ya Lissu anaweza pata yeyote ila kuombea Dua baya kwa waliotenda ni mbaya kwako even Yesu aliwasamehe hadi waliomchoma mkuki mbavuni... akiwaambia hawajui walitendalo japo walikuwa wamedhamilia... Kuombea watu Mabaya wadhania Dua hiyo itapokelewa as if wewe ni msafi sana.. Wewe Muombee tu Lissu apone kabisa na uombee na wengine Duniani walio kwenye Majanga hata zaidi ya Lissu Wapone kisha tubu dhambi zako.
Tulia sindano ikuingie vizuri kalioni
 
Akikupiga kofi shavu la kushoto mgeuzie na shavu la kulia akupige.. ndio mlivyofundishwa na sio kulipiza
Unaogopa eeh???haaaa haaaaaa haaaa
Wewe ulipokuwa unammimina Marisasi hukuujua huo msemo.
Bandugu Mutulie Basindano Babaingie Muzuri(in new muchepuko fake wa Diamond from Burundi)
 
Hakika wewe umegundua jambo !!! Jaji anaongea mambo yasiyomuhusu kabisa !!! Uchunguzi wa nje au ndani anahusikaje ?? Na kwanini anaogopa uchunguzi wa nje kwa kiasi cha kujiaibisha kuingilia,mambo ya kiusalama ? Siayasubiri yamfikie,ktk meza yake kwa kuhitajika taaluma yake ya sheria???? Na kwanini baada ya jaribio la kumuua Lisu kubuma ?.kwakweli kuna jambo kubwa sana nala kuitia nchi Aibu linalokumbatiwa na wakuu wa nchi lisilipuke.kwanini sasa ?Mara mwanajeshi na yeye anapigwa risasi tu eti kwakua Lisu kapigwa rizasi !!! Na waliompiga wasikamatwe ili iwe suluhu ya issue ya Lisu !!!.kweli mjeshi hatakama ni mstaafu afanyiwe hivyo,hili jeshi la nchi hii lingelala tu kuona mwenzao anadhalilishwa eti na wasiojulikana!!!!.sio nchi hii ingechimbika?? Alafu anainuka na mjeshi kutete kibiti kwa gharama ya maisha ya Lisu !! Jamani,wakubwa na viongozi wa nchi hii,chonde,msitudharau kiasi hiki !!. Tuna akili,na tuna connect dorts za kauli toka kwa magufuli,kumkamata Lisu kila leo,nakupigwa risasi kwa Lisu.magufuli kinywa chake kimekua kiki thibitisha uadui na Lisu,upinzani kwa ujumla wake,na yeyote anayemkosoa.hivyo hizi yowe za viongozi,kwa sasa picha yake inaonyesha wazi bidii za makusudi kumnusuru magufuli tu,na sio vinginevyo.najeshi kuingizwa,sasa tujue magufuli anajiandalia kutawala milele,kwakua tutatumiwa jeshi kwenye uchaguzi kama ilivyokua Zanzibar !! Mungu wewe ndie mwanajeshi mkuu dunia yote.Tuponye na kila mpango ovu wowote wa ccm dhidi yetu.epusha raia,wapinzani,watoto,wanawake walemavu na wazee,ambayo ni makundi dhaifu kuuwawa kirahisi,na vijana weto ,kwamatumizi mabaya ya majeshi ya nchi yatakayofanywa na magufuli,Nakuamini sana na kukutegemea kwa hili na mengine yote,Amen.
You are so amazing!
 
Alikuwa Dodoma Mkuu kusimamia kazi aliyotumwa na Baba yake ili kuhakikisha inakamilika. Bashite pia anahusika na kupotea kwa Ben Saanane na kutekwa na kuteswa kwa Roma na wenzie. Kumbuka ahadi yake ya wangepatikana kabla ya Jumapili na kweli wakapatikana. Hivyo alikuwa anajua huko walikofichwa huku wakiteswa. Msikilize hapa lakini Cha kustaajabisha hakukamatwa wala kuhojiwa kwa kauli yake hiyo.


Mungu yupo Leo Na milele.Damu ya Lissu haitapotea Bure.Trust me my best friend.
 
Tusubiri mwisho wake utafika tu kiwewe hiki bado kitendawili kati ya ndani yao na nje yao kila aliyetenda anaweweseka
 
Bashite alianza kufeli kuanzia darasa la saba.
Form for alifeli.
Form six hapajui ajawahi kukanyaga.
Kuvamia kituo cha habari kafeli.
Vita vya shisha kafeli.
Vita vya madawa ya kulevya kafeli.
Jaribio la kumbambikizia Gwajima mtoto kafeli.
Kumteka Roma kafeli.
Jamani Upande wa Lisu ndio sasa kafeli zaidi tena zaidi.
Ushauri:
Omwana wa malanja nikikushauri utanisikia?
Aiseeee nimechekaaaa kwa sauti..Form six anapasikia tu??
 
Hapo nyuma kidogo niliwahi kuuliza, je yawezekana wakuu wa vyombo mbali mbali nchini walijua kilichokuwa kinaendelea kuhusu hatma ya Mh. Tundu Antiphas Lissu? Je yawezekana waratibu na watekelezaji walikuwa na uhakika Mh. Tundu Lissu hangeendelea kuwa hai saa 24 baada ya kumiminiwa idadi kubwa ya risasi mwilini?

Ukweli kwamba Mwenyezi Mungu kasikiliza maombi ya wengi na hivyo kumuepusha na kifo Mh. Tundu Antiphas Lissu, kumewachanganya wahusika hadi kila moja anaibuka na tamko lake! Je kuibuka kwa kauli na vitendo kutoka kwa viongozi mbalimbali huku hali ya Mh. Tundu Antiphas Lissu ikiendelea kuimarika, kunatupa picha gani?

Hali hii bila shaka imesababishwa na kiwewe kizito kilichowakumba washauri, waratibu, na watekelezaji wa jaribio la kigaidi la kumuua Mh. Tundu Antiphas Lissu! Tusubiri kuona mengi, kusikia mengi na kushuhudia mengi kwani walichopanga kutenda hawa waovu Mwenyezi Mungu kawakatalia na sasa wanahaha nafsi zao zikiwasuta!
Dhambi ya kunuia kuua haijawahi kumuacha mtu salama.
 
Kila wakijitokeza mbele ya press nawaona jinsi mimacho inavyowatoka baada ya mipango yao ovu kugonga mwamba.
 
wtf... Thread ya Kijinga i thought una jambo jipya muhimu umebaini kumbe upuuzi tu kama mlevi wa chibuku... Watanzania acheni kuongea pumba hadharani ulitakiwa ukatoe maoni haya kwenye thread zilizopita na sio kuanzisha thread as if Umebaini kitu kipya....

FICHA UPUMBAVU WAKO.
Roho zinawauma kwa azma yenu ovu kushindwa kuzaa matunda. Nguvu zenu za giza zimeshindwa...uwezo wa Mungu umetamalaki.
 
Hivi ni kweli Bunge hawajui kuwa Chadema kwa kushirikiana na Familia ya Lissu ndio wanaomuuguza Mh. Lissu hospita Nairobi.

Spika hana Ruhusa ya Mh. Mbowe (KUB) ya kumuuguza Lissu Nairobi.

Iweje malipo ya michango ya Wabunge yafanyike hospital bila kuwapa taarifa Wanaomuuguza Mgonjwa?Chadema na Familia ya Lissu.

Tena kutoa taarifa ya malipo muda mfupi baada ya kushutumiwa kuweka mfukoni Fedha za michango.

Mbona hii Serikali inazidi kujiweka uchi mbele ya hadhara kwenye hili suala la Lissu,Wanajichanganya mno,kila siku wanazidi kuharibu badala ya kujenga,Je hatukuamini kuwa Lissu angepona?

Pesa zichangwe tarehe 8 sijui zije kulipwa tarehe 20 kweli inaingia akilini tena kwa kificho?

Huyu mama naye wa wizara ya afya,utafikiri sio mwanamke?hana uchungu wa kimwanamke?Mgonjwa ameanza kutibiwa tarehe 7 baada ya siku 14 Wizara inatangaza kutaka kumtibu popote duniani kweli?hapana Dada angu Ummy muongope Allah,kuwa na hofu na Mungu,duniani hamna Mungu Mtu na ndio mana Lissu ameweza kunusurika,Ummy wewe ni Muislam,unajuwa maana ya Jina lako katika Uislam,kumbuka heshima ya Jina lako!!

Yule aliyeapishwa Juzi,anajitokeza kufafanua mambo yasiyomuhusu,eti Jaji Mkuu,kiongozi wa Mhimili wa Mahakama anafanya Press na waandishi wa habari,tena anachagua upande,sasa ikija kesi mahakamani na huo upande ukiwa ndio mshtakiwa?itoshe kusema na aone kuwa heshima aliyopewa na Mbowe ni busara na Hekima kwa Mhimili wa mahakama,aone maendeleo ya mahakama zetu kabla yake licha ya changamoto chungu mzima,asikubali kutufanya tukose imani na mahakama katika uongozi wake.
Pole .Naomba tu nikwambuie kitu usichokijuaa
Mimi tangu nijue anayeratibu haya nimeacha kabisa kumlaumu MTU.Msamehe ummy hana ubavu wowote.
 
Tutaona mengi, tutasikia mengi na tutashuhudia mengi...kila mtuhumiwa atatoka na kauli yake kivyake. Kuna mwingine ameamua kuachilia michango ya kusaidia matibabu wiki mbili baada ya tukio. Yuko mwingine yuko tayari kusimamia matibabu baada ya kusikia hali ya mgonjwa inazidi kuimarika na [B]Mlaleo[/B] yeye kaja kivyaKE na matusi...viti vinapata moto na kuvikalia lazima uwe fyatu. Mwingine naambiwa kawa kama gurudumu, anajazwa upepo aweze tu kumaliza siku salama, laana iko kazini.
Huyo wa upepo ngoja nimgoogle
 
Ongea utakacho kwani unashuhudia uongo tu. Hivyo hakuna heshima atakupa mtu mwenye akili nzuri tafuta mashabiki wapumbavu watafurahia ulichoandika... kama hujui nchi inavyoendeshwa mnazania ni mchezo mchezo tu... mtasononeka hadi mpate midonda ya tumbo... Usidhanie siku utaamika ukute nchi imekuwa safi huko kwako ni kuchafu pekee...

jambo usilolijua ni bora kunyamaza kuliko ushuhuda wa uongo hakika utapotea.
....Umeanza kuweweseka! na badoo utaongea yootee.
 
Upo sahihi wamechangishana huko kutuma hela za matumizi hosptalini hawajatuma sijui walikua na maana gani kutangaza kuchangisha na pesa mpaka sasa wanayo,Mungu anawaona
 
Tutaona mengi, tutasikia mengi na tutashuhudia mengi...kila mtuhumiwa atatoka na kauli yake kivyake. Kuna mwingine ameamua kuachilia michango ya kusaidia matibabu wiki mbili baada ya tukio. Yuko mwingine yuko tayari kusimamia matibabu baada ya kusikia hali ya mgonjwa inazidi kuimarika na Mlaleo yeye kaja kivyaKE na matusi...viti vinapata moto na kuvikalia lazima uwe fyatu. Mwingine naambiwa kawa kama gurudumu, anajazwa upepo aweze tu kumaliza siku salama, laana iko kazini.
Mkuu "Mag3" hebu jazilizia nyama kidogo juu ya huyo "Mwingine naambiwa kawa kama gurudumu, anajazwa upepo aweze tu kumaliza siku salama, laana iko kazini".
 
Back
Top Bottom