Elections 2010 Kiyabo "arejea" CCM

MwanaHaki

R I P
Joined
Oct 17, 2006
Posts
2,401
Reaction score
707
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama Cha Jamii (CCJ) - almanusura niandike CCM! - Richard Kiyabo, leo "amerejea" na kukabidhiwa kadi rasmi na Katibu Mkuu, Yusuf Makamba.

Habari zilizotangazwa sasa hivi na Taarifa ya Habari kwa Ufupi ya saa 10 jioni ya TBC1 zimetangaza.

Taarifa zitaendelea kuwafikia.
 
siasa za tanzania zingelikuwa hazisikitishi basi zingechekesha
 
Hehe.. huyu nae fasta! Ila nasema wale wanaoenda CCM sasa hivi wajue wamechelewa! Watakachopata sasa hivi kwa ajili ya kuhama wajue ndo hichohicho... anything else ni ahadi hewa za Mungwana... :becky:
 
Aisee! Kila la kheri ndugu Kiyabo
 
napenda kumuuuliza Mpendazoe, wakati unaenda CCJ ulifikiria kwa makini"??????????????? au ... maana Kiyabo tayari ndani ya CCM.. au ulistuka ukaamua kuamia chap chap chadema... baki huko huko Chadema na pigania jimbo Segerea!!
 
Anguko kubwa sana kwa Kiyabo. Hata hivyo alikuwa parasite. Existence yake ilitegemea sana wale vigogo waliokuwa na hofu ya kutoswa / kuvuliwa uanachama wa ccm waliomtuma kuanzisha ccj ili wakitoswa waje moja kwa moja kuchukua madaraka na kushiriki uchaguzi mkuu.
 
Hizi njaa za Tanzania ni balaa kweli kweli. Kama uliamua kwenda kuanzisha chama cha upinzani, kisha unarudi tena kwenye chama ulichokuwa unakipinga within a year basi utakuwa mgonjwa wa UBONGO.

 

Attachments

  • Kiyabo.jpg
    28.8 KB · Views: 35
Hizi njaa za Tanzania ni balaa kweli kweli. Kama uliamua kwenda kuanzisha chama cha upinzani, kisha unarudi tena kwenye chama ulichokuwa unakipinga within a year basi utakuwa mgonjwa wa UBONGO.


Ukisikia mtu kuwa taahira na ZUZU, huu hapa uthibitisho!
 

Ama kweli ukistaajabu ya Musa utaona ya Firauni! Yawezekana CCJ was a just a scam meant to be used as scapegoat by CCM member runneraways?
 
Hizi njaa za Tanzania ni balaa kweli kweli. Kama uliamua kwenda kuanzisha chama cha upinzani, kisha unarudi tena kwenye chama ulichokuwa unakipinga within a year basi utakuwa mgonjwa wa UBONGO.


Hata suti ilishapwaya sasa ana uhakika wa kurudisha afya.
 
Sayansi ya Makamba ya Ushindi inachekesha kweli wakati wao wanaokota mtu mmoja mmoja na pengine wnapigwa changa la macho kama vunjo na mbeya vijijini unaambia kuna mahali baada ya kukolewa na sera za vyama vya upinzani serikali nzima ya kijiji inavunjwa hao ndio wahamaji sio hawa waganga njaa,
Kwani alienda wapi baada ya CCJ kuvunjwa
 
Cheko lake tu limekaa kitaahira taahira - ananikumbusha mgonjwa mmoja taahira pale hospital ya MILEMBE!
 

bora katambaa fasta hatutaki wanafiki kama hawa wanaonunuliwa kwa vijinsenti vya kifasadi inavyoelekea wanaweza hata kuuza wake zao kwa mafisadi kwa hizo njaa zao......tupa kule.ngoma itambae
 
Kuna story moja huyu kiyabo aliitunga kuhusu kuvamiwa na kuporwa nyaraka zake za CCJ.
alisema "nilizingirwa na jamaa waliovalia sare za USALAMA wa TAIFA...... wakanikaba na kunipora nyaraka...."
Jamani kila siku nakumbuka hii story najaribu kuunganisha doti nakosa pa kushika.

Hivi Usalama wa Taifa wana sare kweli? kama wanazo huyu mwenzetu alizijuaje?
Na kama zipo ni sare gani hizo? maana za jeshi na polisi twazijua hata za madereva wa serikali (viongozi) twazifahamu
 
Jamani kwa nini Mnamlaumu? Labda sasa ameshasoma sera za CCM na kuzielewa
 
Nadhani alikosa nafasi ya jikoni CHADEMA ambapo walishamstukia na kumweka benchi.
Hongera zake kwa kudhihirisha UCHU wake hadharani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…