Elections 2010 Kiyabo "arejea" CCM

Elections 2010 Kiyabo "arejea" CCM

Richard Kiyabo,
Mkuu wangu kama Mpendazoe ni kaka yako basi wee huna hata aibu na ustaarabu kwani kutoa siri za nyumba ya ndugu yako inatisha sana. Na mbona hukuzungumza kwamba uliwahi kumsalandia pia mkewe Mpendazoe? Au unataka vijana wa mjini tukutoe uchi na ufuska wako!
 
Kweli nimeamini ya wahenga "mwana mwenye hekima ustili aibu ya Babaye, lakini mwana mpumbavu ufunua utupu wa mamaye" .Kiyabo huyu huyu ambaea alikuwa mwenyekiti CCJ, akahamia CHADEMA kwa mbwembwe baadae akakimbilia NRA kwa vifijo mwishowe akarudi CCM kwa kishindo (mambo haya yote ndani ya miezi isiyozidi tisa) Leo hii anasema nduyeye Mpendazoe afai hata ujumbe wa nyumba kumi! kweli kua uyaone. cha kujiuliza hapa wakati wanaanzisha CCJ na kumpokea Mpendazoe hakujua kuwa katelekeza familia? je wakati wanaenda wote CHADEMA hakujua kuwa kaka yake afai kuwa mwenyekiti wa tawi? Je wakati wanachaguliwa kuwa Mbunge wa CCM alishindwa kuwaambia WASUKUMA wenzake wa Jimbo la KISHAPU kuwa kaka yake hafai. Huyu kiyabo nadhani ni mtoto wa nje ya ndoa kifupi ni mwanaharamu mtu mwenye maadili awezi kuonyesha utupu wa kakaye hadharani ili tu ashindwe UBUNGE. Shame on u KIYABO ustahili hata kuwa kiongozi wa familia, hata mke uliyemuoa kala hasara wanao hafazali wangekuwa yatima kuliko kuwa na baba kama wewe. HASARA TUPU. Ngoja kampeni ziishe ndipo utakapojua CCM sio watu ndugu yangu utaona kwa macho yako JK na RIDHIWAN wake na MAKAMBA na JANUARY wake wakati wewe na Mpendazoe wako amtazamani usoni
 
aibu tupu! Unaombaje uongozi wa jamii, ilhali nyumba yako inakushinda kuongoza?

kiyabo mwinie huyooooo, dah yaani kweli ccm imeoza na imeishiwa. Yaani hata mtoto mdogo anajua kuwa kiabo ni taahira. Ushabiki mwingine ni wa kijinga na kujidhalilisha mbele za watu, hata kama wewe ni cccm damu but iweje uje kuamini kwa 100% maneno ya kiyabo wakati wamjua fika kuwa hana akili nzuri? Unabahati sana nimeogopa tu kukwambia kuwa uwezo wako wa kufikiri ni sawa na zero.
 


MWENYEKITI mwanzilishi wa Chama Cha Jamii (CCJ), aliyetangaza kuhamia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Richard Kiyabo, jana alianza rasmi kazi ya kuinadi CCM kwa kumshushia shutuma nzito, aliyekuwa msemaji mkuu wa CCJ ambaye sasa ni mgombea ubunge wa Jimbo la Segerea kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Fred Mpendazoe.

Kiyabo alisema baada ya kumuomba Katibu Mkuu wa CCM, Yusuf Makamba kujiunga na CCM na kukubaliwa mbele ya vyombo vya habari ameomba kupewa kazi rasmi ya kuinadi CCM katika Jimbo la Segerea kwa vile ana kazi maalumu katika jimbo hilo.

Katika mkutano wa uzinduzi wa kampeni za CCM katika Kata ya Kimanga uliofanyika jana, Kiyabo alimshambulia Mpendazoe akisema ni mtu asiye makini na ambaye ana uwezo wa kushika wadhifa wa Balozi wa Nyumba Kumi tu na si vinginevyo.

Mgeni rasmi katika uzinduzi huo alikuwa Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Dar es Salaam, John Guninita. Wengine waliohudhuria ni mgombea Ubunge katika Jimbo la Segerea kupitia CCM, Dk.

Makongoro Mahanga, Mwenyekiti wa CCM wa Wilaya ya Ilala, Suleiman Karanje na mgombea Udiwani wa Kata ya Kimanga, Pastory Kyombya.

Alisema ingawa Mpendazoe ni kaka yake wa damu, lakini hana uwezo wa kuongoza na kwamba udhaifu wake huo umesababisha kumfanya kushindwa hata kuiongoza familia yake na kuifanya kuishi kwa tabu na mashaka.

"Mpendazoe ni kaka yangu, tumenyonya pamoja lakini yeye mwenyewe hajitambui. Ni hatari kuongozwa na mtu asiyejitambua.

Familia yake ilimshinda na mimi ni shahidi kwani nilipata shida sana katika kumtunza mkewe na wanawe Vitalis na David, hafai kuwa kiongozi.

"Nawaombeni itakapofika Oktoba 31, (siku ya upigaji kura kwa uchaguzi mkuu), mgombea wa CCM katika Jimbo la Segerea (Dk. Makongoro Mahanga) apate ushindi wa asilimia 99.5.

Nawaomba msimpigie kura hata moja Mpendazoe maana hafai. "Kwa wakati huu Mpendazoe hawezi kumudu kuongoza nafasi yoyote labda wakati mwingine atakapoomba ndio tutamuangalia.

Na hata kama atarejea CCM mimi nadhani uwezo wake ni kuongoza katika nafasi ya Balozi wa nyumba kumi, tumpime kwanza katika ngazi hiyo kabla ya kumpa kazi nyingine yoyote," alisema Kiyabo.

Akizungumza katika uzinduzi huo, Dk. Mahanga alisema ana uhakika wa kuwa Mbunge wa Jimbo hilo na tayari ameshampata fundi wa kumshonea suti atakayoivaa wakati atakapokwenda bungeni Dodoma kuapishwa.

Kwa upande wake Kyombya alisema kutokana na kazi nzuri aliyoifanya akiwa Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Kimanga na kupewa ridhaa ya kushika wadhifa huo katika vipindi viwili, sasa ni wakati muafaka kwake kuchaguliwa kuwa Diwani wa Kata ya Kimanga ili aweze kuingia katika vikao vya Baraza la Madiwani katika Halmashauri ya Manispaa ya Ilala na kuwasilisha matatizo ya wananchi wa Kimanga kirahisi zaidi.

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Guninita, alisema ana uhakika CCM kuibuka na ushindi mkubwa kutokana na kuwa na wagombea makini na wanyenyekevu kwa wananchi wakiongozwa na Rais Kikwete.

source: habari leo



Hivi wadau, huyu jamaa anafanya kazi gani? ili mkono uende kinywani, maanake unaweza kukuta njaa ndo inamsumbua hadi kuamua kumtukana kaka yake mpendazoe

Tatizo siyo Kiyabo na CCM wake bali njaa za walio ndani ya CCM
Kiyabo amedhihirisha kwamba siyo tu hawezi kutunza familia lakini yupo tayari kusaliti familia kwa vijisent vichache. Kama anasema mpendazoe hafai uongozi, mbona alikuwa mbunge aliyeakilisha vyema watu wake na akajipambanua bungeni kuwa yupo mstari mnyoofu? Mbona CCM walikuwa na mkakati wa kumfukuza kabla hajawastukia?

Ushindi wa kishidno wa CCM utatokana na LAZIMA TUSHINDE yao
 
Richard Kiyabo,
Mkuu wangu kama Mpendazoe ni kaka yako basi wee huna hata aibu na ustaarabu kwani kutoa siri za nyumba ya ndugu yako inatisha sana. Na mbona hukuzungumza kwamba uliwahi kumsalandia pia mkewe Mpendazoe? Au unataka vijana wa mjini tukutoe uchi na ufuska wako!
..Kumbe anavyosema alimsaidia mke wa mpendazoe alikuwa anamsaidia ktk majamboz?
kijana HANA ADAB KABISA YULE
 
Nafikiri Kiyabo ndo hana uwezo wa kuongoza maana angekuwa nao, CCJ isingemfia mikononi mwake.
Aisee. naona unapiga madochi ya uso mkuu.
Tukubali alitumwa na ccm kuanzisha ccj kupima joto la siasa za mabadiliko
 
Hivi Makongoro anawatunza wale watoto aliozaa na mabaa meidikadhaa kwenye maeneo ya Ubungo, Mwenge na Sinza kati ya mwaka 1994 na 1996?
 
Kama yeye Mpendazoe ni ndugu yake wa kunyonya kwa nini hayo mambo ya kifamilia Kinabo anayapeleka kwenye kampeni. Ndiyo yaleyale ya vyumbani mnaleta kwenye majukwaa.
 
Back
Top Bottom