Mkalukungone Mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 3,141
- 7,205
Mwenyekiti wa Chama cha ACT Wazalendo na Waziri Kivuli wa Fedha katika chama hicho, Kiza Mayeye, amesema licha ya rutuba ya ardhi ya Tukuyu na mvua nyingi zinazonyesha kila mwaka, wananchi wa eneo hilo bado wanaishi katika umasikini mkubwa.
Akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika leo Julai 5, 2025 Tukuyu wilayani Rungwe, Mayeye amesema Tukuyu ina kila kitu kinachohitajika kwa maendeleo, lakini bado wananchi hawajanufaika.
“Pamoja na rasilimali zilizopo, kina mama bado wanalalamika huduma za afya si bora, hatuna madaktari, hatuna wauguzi wa kutosha. Serikali ilipaswa kuvuna maji haya mnayoyapata kwa wingi ili kuwaondolea kina mama mzigo wa kutembea na ndoo kichwani,” amesema.
Akitamatisha hotuba yake, Mayeye anesema ni muda wa kuwaambia Chama cha Mapinduzi (CCM) wakae pembeni, waone wapinzani watafanya nini.