The Watchman
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 2,186
- 4,940
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Kigoma Kaskazini kupitia Chama cha ACT Wazalendo, Kiza Mayeye, amesema iwapo wananchi watampa ridhaa ya kuwa Mbunge wao, atahakikisha anapigania maslahi ya wananchi kwa kuhakikisha bajeti zinazopitishwa bungeni zinawagusa moja kwa moja wananchi na si kufujwa kwenye mambo yasiyo na msingi.
Akizungumza wakati wa Uzinduzi wa Kampeni Jimboni humo Septemba 08, 2025, Kiza amesisitiza kuwa Jimbo la Kigoma Kaskazini bado linakabiliwa na changamoto nyingi kwenye sekta muhimu, ikiwemo maji ambapo miradi mikubwa imetelekezwa, pamoja na ukosefu wa huduma bora za afya na kijamii kwa ujumla.
“Ndugu zangu, siasa ni maisha. Ni wanasiasa wanaopanga bajeti zetu, barabara zinapangwa na wanasiasa, afya inapangwa na wanasiasa, elimu inapangwa na wanasiasa. Huwa mnaona wabunge kila mwaka kuna bajeti, lakini ni asilimia ndogo tu ndiyo inakuja kwa ajili ya wananchi walalahoi mnaolipa kodi na mnaoteseka na ugumu wa maisha. Bajeti nyingi zinaenda kwenye mambo mengine ambayo hayana maendeleo kwa wananchi,” amesema Kiza.