PreGE2025 Kiza Mayeye wa ACT Kugombe ubunge Kigoma Kiskazini

PreGE2025 Kiza Mayeye wa ACT Kugombe ubunge Kigoma Kiskazini

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Sijapewa username bado

JF-Expert Member
Joined
Aug 15, 2024
Posts
1,775
Reaction score
2,891
Mwanachama wa Chama Cha ACT Wazalendo, Kiza Hussein Mayeye Mei 03, 2025 amejitokeza kuchukua fomu ya kugombea ubunge katika Jimbo la Kigoma Kaskazini kwa tiketi ya chama hicho.

Kiza Mayeye ambaye pia ni Mwenyekiti wa ACT Wazalendo Mkoa wa Kigoma, amekabidhiwa fomu hiyo na Katibu wa ACT Wazalendo Jimbo Kigoma Kaskazini Ilaki Issa Ramadhani katika ofisi za jimbo zilizopo Mwandiga, Wilaya ya Kigoma.
 
Hivi hao ACT wazalendo hawakusikia No reforms, no election?
 
Nilizani anaitwa Kiza Mayele nikataka kuhoji uraia wake, nikimkumbuka mzee wa kutetema Fiston Kalala Mayele
 
ACT wanajitia kiherere ku take loop pahala pa CHADEMA wakidhani wataokota majimbo mawili matatu, labda waachiwe, vinginevyo kwa hali ilivyo wataangukia pua, na nasema waangukie pua kisawasa ili iwe fundisho kwa vyama kiherere kuingia kwenye uchaguzi wa abrakadabra
 
Mashabiki wa simba wanaweza kuingiwa na hofu kwa kufikiri labda huyo jamaa ni Mayele, badala ya Mayeye.
 
Back
Top Bottom