Kizazi cha dhahabu cha watawala nguli katika geopolitics na diplomasia ukanda wa SADC na Africa Mashariki kimefifia sana

Kizazi cha dhahabu cha watawala nguli katika geopolitics na diplomasia ukanda wa SADC na Africa Mashariki kimefifia sana

Yoda

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2018
Posts
48,475
Reaction score
70,102
Ukanda wa SADC na Africa Mashariki umewahi kuwa na watawala nguli sana wa geopolitics na diplomasia mwaka 2015 kurudi nyuma.

Nyerere, Mandela, Thabo Mbeki, Mkapa, Chisano na Kikwete ambaye ni kama alifunga ukurasa huu walikuwa wanaweza hata kuitisha kikao cha pande zinazogombana, zinazopigana au kuzozana watu wakaitikia wito wakazungumza au wakakemea jambo walengwa wakaweka nidhamu kidogo.

Siku hizi ukirejea yanayoendelea Congo DRC ni kama kila mtu ameota sharubu, hakuna mtu mwenye sauti, hakuna anayesikiliza au anayeweza kutoa kauli ikatiliwa maanani.
 
Back
Top Bottom