Kizazi cha Mabadiliko si Gen Z, ni Millennials hawa ndo waliona Ahadi, Kashfa na Mfumo kwa Macho Yao

Kizazi cha Mabadiliko si Gen Z, ni Millennials hawa ndo waliona Ahadi, Kashfa na Mfumo kwa Macho Yao

ndege JOHN

JF-Expert Member
Joined
Aug 5, 2015
Posts
25,030
Reaction score
61,298
Watu wengi wanapozungumzia nguvu ya mabadiliko ya kisiasa huwa wanakimbilia sana kuipa nguvu Generation Z kwa sababu ndiyo wanaonekana zaidi mtandaoni. Lakini ukiangalia kwa undani historia ya siasa za Tanzania za miaka ya karibuni, kuna hoja kwamba kizazi ambacho kinaweza kuleta mabadiliko makubwa zaidi si lazima kiwe Gen Z, bali ni millennials.

Millennials wengi wa Tanzania walikua kwenye kipindi ambacho mijadala ya ufisadi, rushwa na matumizi mabaya ya madaraka ilianza kuonekana wazi sana kwenye vyombo vya habari na mitandaoni. Miaka ya 2000 hadi 2015 ndiyo kipindi ambacho watu wengi wa kizazi hicho walikuwa wanaanza kujitambua kisiasa. Ndiyo kipindi ambacho majina ya scandals, mijadala ya uwajibikaji, na lawama dhidi ya mfumo wa kisiasa vilikuwa vikitawala sana kwenye redio, TV na magazeti. Hivyo wengi wao walikulia kwenye mazingira ya kusikia simulizi za “mfumo uliochoka”, tofauti na wazazi wao waliokulia kwenye simulizi za uhuru na utaifa.

Tofauti kubwa ya millennials na Gen Z ni kwamba millennials waliona transition ya Tanzania kutoka zama za media za kawaida kwenda internet. Waliona maisha kabla ya social media na baada ya social media. Waliona pia matumaini ya mabadiliko ya kisiasa yakipanda na kushuka kwa macho yao wenyewe. Hilo liliwajenga kuwa kizazi chenye kumbukumbu ya frustrations za muda mrefu.

Soma Pia: Martin Maranja: Millennials Tumelifikisha Taifa hapa, hatuwezi kuiwajibisha Serikali hata inapokesea

Gen Z wengi kwa upande mwingine wamezaliwa tayari kwenye dunia ya internet, memes, trends na taarifa nyingi sana zinazobadilika kila dakika. Mara nyingi wanaonekana kuwa na energy kubwa mtandaoni, lakini pia attention yao huhama haraka sana kutoka issue moja kwenda nyingine. Ndiyo maana baadhi ya wachambuzi huona kuwa Gen Z wanaweza kuwa wazuri katika ku-create noise na trends, lakini si rahisi kuwategemea kama msingi wa movement ya muda mrefu ya kisiasa.

Millennials sasa ndiyo wanaingia kwenye umri wa kubeba uchumi, familia, taasisi na nafasi za maamuzi ndani ya jamii. Wengine ni wafanyakazi, wafanyabiashara, viongozi wa mitaa, creators, au watu wenye influence kwenye familia zao. Hicho ndiyo kizazi kinachoanza kuwa na power halisi ya kijamii na kiuchumi, si power ya hashtags pekee.

Na ukitazama kisiasa, mara nyingi mabadiliko makubwa duniani hayaletwi sana na vijana wadogo kabisa, bali na kizazi kilichoanza kufika umri wa responsibility — watu wenye hasira za muda mrefu lakini pia wenye nafasi ndani ya mfumo wa jamii. Ndiyo maana kuna hoja kwamba kama kweli kutakuwa na shift kubwa ya kisiasa Tanzania katika miaka ijayo, inaweza kusukumwa zaidi na millennials kuliko Gen Z.

Gen Z wanaweza kuwa sauti kubwa mtandaoni, lakini millennials wanaweza kuwa kundi lenye kumbukumbu, uchungu wa muda mrefu na uwezo wa kufanya maamuzi yenye impact kwenye uhalisia wa maisha ya taifa.
 
Watu wengi wanapozungumzia nguvu ya mabadiliko ya kisiasa huwa wanakimbilia sana kuipa nguvu Generation Z kwa sababu ndiyo wanaonekana zaidi mtandaoni. Lakini ukiangalia kwa undani historia ya siasa za Tanzania za miaka ya karibuni, kuna hoja kwamba kizazi ambacho kinaweza kuleta mabadiliko makubwa zaidi si lazima kiwe Gen Z, bali ni m

Gen Z wanaweza kuwa sauti kubwa mtandaoni, lakini millennials wanaweza kuwa kundi lenye kumbukumbu, uchungu wa muda mrefu na uwezo wa kufanya maamuzi yenye impact kwenye uhalisia wa maisha ya taifa.
uko sahihi 100%,

naunga mkono hoja 🐒
 
Mabadiliko huwa yanaanzia na watu mjini wa vizazi vyote.
 
Kuna kitu ambacho watu wengi wa kisiasa bado hawajakielewa vizuri kuhusu kizazi cha millennials Tanzania. Hiki si kizazi ambacho unaweza kukivuta kirahisi kwa slogans za kisiasa kama katiba mpya, tume huru au uhuru wa vyombo vya habari pekee. Millennials wengi wamefika hatua ambayo wanapima siasa kwa maisha yao ya kila siku, si kwa maneno makubwa ya kisiasa yanayozunguka mtandaoni.

Tofauti na vizazi vya nyuma vilivyokuwa vinaongozwa sana na historia ya chama au ideology za kisiasa, millennials wengi wamekua kwenye kipindi cha mabadiliko ya uchumi, scandals za ufisadi, ahadi nyingi za kisiasa na kupanda kwa gharama za maisha. Ndiyo maana wengi wao wamekuwa pragmatic zaidi kuliko emotional. Hawaulizi sana nani anaongea vizuri kisiasa, bali wanauliza maisha yatabadilika vipi.

Ndiyo maana leo hii ukisimama mbele ya millennial ukamwambia aandamane kwa ajili ya katiba mpya au tume huru, si rahisi kumgusa moja kwa moja kama ambavyo watu wa mtandaoni wanavyodhani. Kwa sababu ndani kabisa wengi wao tayari wanaamini kuwa hata uchaguzi ukiwa huru kwa asilimia mia moja bado CCM itaendelea kuwa na nguvu kubwa ya kisiasa kutokana na mfumo wake mpana, historia yake na mizizi yake ndani ya jamii. Hivyo kwao, hoja ya uchaguzi huru peke yake haionekani kama guarantee ya mabadiliko ya maisha yao.

Vivyo hivyo kwenye suala la katiba mpya. Wengi hawaioni kama jambo lisilo muhimu, lakini pia hawaioni kama kitu kitakachowatoa moja kwa moja kwenye pressure za maisha wanazopitia kila siku. Kwa sababu hata vipengele vikibadilika, bado wanajua kesho wataamka kupambana na kodi ya nyumba, bei ya cement, ajira ngumu, biashara zisizoenda vizuri na gharama za maisha zinazopanda kila mwaka.

Ndiyo maana ukitaka kuwavuta millennials kisiasa, huwezi kuanza na stories za ideology au activism pekee. Lazima uanze na uchumi. Waambie namna watakavyopata kazi, namna bei za vifaa vya ujenzi zitakavyoshuka, namna biashara zitakavyokuwa rahisi, namna kipato kitakavyoongezeka au namna maisha yatavyokuwa nafuu. Hapo ndipo utaanza kugusa hisia zao za kweli.

Hata kwenye suala la uhuru wa vyombo vya habari, millennials wengi wamekuwa skeptical sana. Wamekua wakiona jinsi media, waandishi, influencers na hata watu maarufu wanavyoweza kubadilika kulingana na maslahi au fedha. Ndiyo maana ukimwambia mtu “pigania uhuru wa media” si lazima aone hiyo kama agenda inayobadilisha maisha yake moja kwa moja. Kwa mtazamo wake, hata media zikiwa huru bado mchezo wa maslahi unaweza kuendelea vilevile.

Kizazi hiki kimechoka siasa za maneno makubwa yasiyoonekana kwenye uhalisia wa maisha yao. Wanataka matokeo yanayoshikika. Wanataka kuona maisha yanakuwa nafuu, si kusikia debates zisizoisha kila uchaguzi unapokaribia. Ndiyo maana watu wengi wanakosea wanapodhani kelele za mtandaoni zinaweza kuwasha taifa lote. Ukweli ni kwamba millennials wengi wamehamia kwenye siasa za practical life kuliko siasa za ideology.

Na hapo ndipo tofauti kubwa kati ya activism ya mtandaoni na uhalisia wa jamii inaanza kuonekana wazi kabisa.
 
Watu wengi wanapozungumzia nguvu ya mabadiliko ya kisiasa huwa wanakimbilia sana kuipa nguvu Generation Z kwa sababu ndiyo wanaonekana zaidi mtandaoni. Lakini ukiangalia kwa undani historia ya siasa za Tanzania za miaka ya karibuni, kuna hoja kwamba kizazi ambacho kinaweza kuleta mabadiliko makubwa zaidi si lazima kiwe Gen Z, bali ni millennials.

Milleials wanaweza kuwa kundi lenye kumbukumbu, uchungu wa muda mrefu na uwezo wa kufanya maamuzi yenye impact kwenye uhalisia wa maisha ya taifa.
Millennials ndio wanaongoza kwa kuwa machawa, wako mitandaoni, wamejaa bungeni, serikalini nk wakifanya uchawa, sidhani kama kuna matumaini kwa kizazi chochote. Tena bora hata Gen Z
 
Kuna kitu ambacho watu wengi wa kisiasa bado hawajakielewa vizuri kuhusu kizazi cha millennials Tanzania. Hiki si kizazi ambacho unaweza kukivuta kirahisi kwa slogans za kisiasa kama katiba mpya, tume huru au uhuru wa vyombo vya habari pekee. Millennials wengi wamefika hatua ambayo wanapima siasa kwa maisha yao ya kila siku, si kwa maneno makubwa ya kisiasa yanayozunguka mtandaoni.
Hali ngumu ya maisha kwa vijana na kukata tamaa ndio italeta presha na shinikizo la mabadiliko kwa CCM hasa ukizingatia zaidi ya 60% ya population ni vijana.
 
Kuna kitu ambacho watu wengi wa kisiasa bado hawajakielewa vizuri kuhusu kizazi cha millennials Tanzania. Hiki si kizazi ambacho unaweza kukivuta kirahisi kwa slogans za kisiasa kama katiba mpya, tume huru au uhuru wa vyombo vya habari pekesa za ideology.


Na hapo ndipo tofauti kubwa kati ya activism ya mtandaoni na uhalisia wa jamii inaanza kuonekana wazi kabisa.
Unasifia tu kwa kuwa na wewe ni millennial ila actually millennials wengi ni very dissapointing
Ndio wanagalagala chini kwenye vumbi Samia akiwatembelea kwenye wilaya zao, ndio walikuwa wanabebwa kwenye treni kama mifugo kwenda kutupwa kwenye mikutano ya hadhara ya CCM. There's no way kukawa na hope kwa millennials. No way
 
Millennials ndio wanaongoza kwa kuwa machawa, wako mitandaoni, wamejaa bungeni, serikalini nk wakifanya uchawa, sidhani kama kuna matumaini kwa kizazi chochote. Tena bora hata Gen Z
mkuu unawaona millennials waliopo kwenye mfumo halafu unadhani ndio kizazi kizima. Ukweli hao ni asilimia ndogo sana wanaonufaika na mfumo. Kuna mamilioni ya millennials wa kawaida huku nje hawana ajira, wanapambana na maisha na hawafaidiki na chochote. Tofauti ni kwamba wao hawaonekani kama waliopo bungeni, serikalini au mitandaoni wakifanya uchawa. Na wengi wa hao ‘machawa’ wa mfumo wanafanya hivyo kwa survival na maslahi, sio lazima kwa mapenzi ya kweli ya kisiasa
 
Back
Top Bottom