Kizazi chembamba |Mlango au Shingo ya kizazi |Cervical stenosis

Kizazi chembamba |Mlango au Shingo ya kizazi |Cervical stenosis

OCC Doctors

Senior Member
Joined
Jul 20, 2018
Posts
113
Reaction score
172
Kizazi chembamba (Cervical stenosis)
Ugumba unaweza kutokea kwa sababu manii hayawezi kupita kwenye mlango huo ili kwenda kulirutubisha yai, hali hii huweza kusababisha mkusanyiko wa damu katika mji wa uzazi (hematometra), hii ni kutokana na damu ya hedhi inaweza isitoke yote ukeni na ikarudi nyuma (backward-flow) kuathiri tabaka la ndani la uzazi na kupelekea ugonjwa wa (endometriosis), Pia usaha unaweza ukajilimbikiza au kujikusanya taratibu kwenye mji wa uzazi, mkusanyiko huu wa usaha kwenye kizazi hufahamika kama (pyometra)

Dalili zinazoweza kuashiria kwamba kizazi chako ni chembamba (cervical stenosis) ni pamoja na kutofautiana kwa hedhi, au mzunguko wa hedhi usiowakawaida (Irregular period), au mwanamke kukosa hedhi kabisa maishani mwake (no periods at all), na kwa wale watakaopata hedhi basi huambatana na maumivu makali ya hedhi (dysmenorrhea), na kutokwa na damu isiyo ya kawaida (abnormal bleeding), uwembamba wa shingo ya kizazi husababisha ugumba kwa sababu manii hayawezi kupita kwenye mlango huo ili kwenda kulirutubisha yai.
Kwa mwanamke ambae ameshafikia muda wa kukoma hedhi
Baada ya kukoma hedhi, uwembamba wa kizazi unaweza kuwepo lakini huwa hakuna dalili yoyote itayojitokeza.
Mkusanyiko wa damu au usaha kwenye kizazi unaweza kusababisha maumivu au kusababisha kuvimba kwa mji wa uzazi . Wakati mwingine wanawake wanahisi hali ya kitu kucheza au kutuna kwenye eneo la tumbo chini ya kitovu.

MATIBABU YA UWEMBAMBA WA SHINGO YA KIZAZI
▪Kupanuliwa kwa shingo ya kizazi (Widening of the cervix)
Ugonjwa wa (cervical stenosis ya kizazi) unatibiwa tu ikiwa mwanawake atakuwa na dalili za mji wa uzazi kujaa damu au usaha, kisha mlango huo wa kizazi huweza kupanuliwa (dilated) kwa kuingiza vifaa vya kupanulia vilivyotengenezwa kwa ulaini (dilators) kupitia kwenye uke mpaka kwenye shingo ya kizazi, kisha kuingiza (dilator) kubwa zaidi. Ili kujaribu kutanua mlango wa kizazi na kuwa wazi, Daktari wako (gynaecologist) anaweza kuingiza kijichupa kidogo kwenye mlango wa kizazi (cervical stent) walau kwa muda wa wiki 4 mpaka wiki 6.

67092460_514152265990553_2628114583188930560_n.png
 
Back
Top Bottom