Dance Macabre
Member
- May 6, 2024
- 32
- 61
Enzi za RFA na Kiss FM, unasikiliza VOA, DW na BBC. Walikuwa na propaganda zao, lakini walihabarisha sana Watanzania juu ya dunia. Kijana mdogo anafahamu yanayoendelea huko Mosul, Iraq. RFA wenyewe walikuwa na vipindi vizuri kama Je Wajua. Kiss FM kwenye burudani, unasikiliza American Top 40, Weekend Top 30, n.k. Millenials wa Kitanzania walikuwa na exposure ya kihabari na burudani. Kiss FM na RFA walitufungulia dunia kihalisi.
Pengine zama za redio hizo na mtindo wao wa habari zimepitwa na wakati. Wamekuja hawa Clouds. Habari kubwa ni umbea wa mjini na michezo. Wachambuzi wao wa mambo hamna kitu, ni ujanja ujanja tu wa kuzungumza. Upande wa burudani ndiyo kabisa, utasikia wale wale wabana pua.
Zamani niliamini kuwa kizazi cha mbele kina kuwa na watu werevu na walioelimika kuliko kilichopita, kumbe si kweli. Kumbe inawezekana muda ukaenda mbele, lakini kizazi kikazidi kujaa ujinga na ushamba.