Kizazi kilichokulia RFA na Kiss FM hakina ushamba kama hiki cha Clouds

Kizazi kilichokulia RFA na Kiss FM hakina ushamba kama hiki cha Clouds

Dunia ya sasa uchaguzi wa mtindo wa maisha ni wako....

Uishi kama zitakavyo "media" ama uishi kwa uhalisia wa maisha ya dunia ,historia za nyuma na kupanga mwelekeo wa kesho......

Bibi mmoja wa kizungu alilia kwa kusema kuwa enzi zao "kijana wa kiume alikuwa havai vinguo vya kubana vya rangi ya njano na pink" ha ha ha
 
Lawena Nsonda, "Baba mzazi baba"
Enzi hizo RFA masafa ya kati AM Redio mkoani inashi saa 7 mchana kujiunga na DW baada ya hapo inakata mpaka jioni wanajiunga na VOA (Mtangazaji mahiri Hadija Riami) baada ya hapo vipindi ni mwendo mdundo asee zamani raha sana.

Baadhi ya vipindi RFA👇🏻
1. Bolingo time (Tontoo Zuber Msabaha)
2. Je huu ni uungwana?
3. Je, Wajua? (Rebeca Muresi)
4. Michezo na RFA (Charles Mobea, Baruan Muhuza)
5. Sitasahau
6. Show Time (Skyworker & Glory Robson)
7. Usiku wa Mahaba
8. Lugha Gongana (Jumaa Ahmed Baragaza)

Endelea na wewe sasa😁😁😁

Watuma Salam maarufu kipindi hicho

1. Muhiri Obaleeeee
2. Lawena Nsonda Baba mzazi - mzee wa Makongorosi Chunya
3. Jumanne Sebarua Tingisha

Nk

Watoto wa 2000 hamtaelewa
 
Enzi za RFA na Kiss FM unasikiliza VOA, DW na BBC. Walikuwa na propaganda zao lakini walihabarisha sana watanzania juu ya dunia. Kijana mdogo anafahamu yanayoendelea huko Mosul Iraq RFA wenyewe walikuwa na vipindi vizuri kama je wajua. Kiss kwenye burudani unasikiliza American top 40, weekeend top 30 nk nk. Millenials wa kitanzania walikuwa wana exposure ya kihabari na burudani. Kiss FM na RFA walitufungulia dunia kihalisi

Pengine zama za redio hizo na mtindo wao wa habari ukapita. Wamekuja hawa clouds.Habari kubwa ni umbea wa mjini na michezo. Wachambuzi wao wa mambo hamna kitu, ni ujanja ujanja tu wa kuzungumza. Upande wa burudani ndiyo kabisa, utasikia wale wale wabana pua.

Zamani niliamini kuwa kizazi cha mbele kina kuwa na watu werevu na walioelimika kuliko kilichopita, kumbe si kweli. Kumbe inawezekana muda ukaenda mbele lakini kizazi kikazidi kujaa ujinga na ushamba.
Redio zisizofaa kusikiliza ni hizi Clouds na Wasafi, hazifai kabisa.
 
Ni copy and paste ikifika saa 1 usiku wote ni habari za michezo ana Anza East Africa anafwata Wasafi anamalizia Clouds
 
Nimekumbuka sana nilikua napenda kusikiliza kiss fm. Jumamosi ulimwengu wa soka kutoka idhaa ya kiswahili "bbc" kutoka london' wanakutangazia ligi kuu ya uingereza. Ile man utd ya kipindi cha fargason.
 
Back
Top Bottom