mtafuta-maisha
JF-Expert Member
- Nov 5, 2016
- 1,982
- 2,931
.
Tareha 22, mwezi wa 4 mwaka 2003, mwanamichezo wa mchezo wa kupiga makasia akiwa kwenye mtumbwi wake mdogo akifanya mazoezi katika bahari karibu na daraja lilioingia kwenye maji lijulikanalo kama Bournemouth huko Dorset Uingereza, alishituka alipoona kama mwili wa binadamu ukiwa unaelea kwenye maji. Aliamua kurudi pwani na kuwataarifu polisi juu ya ugunduzi wake.
Na hapo ndipo mpango wa njama kubwa uliopelekea mauaji ya familia nzima kwa vizazi vyote vitatu ulipogundulika. Hii ilikuwa ni kesi kubwa na ghali sana iliyo gharimu jeshi la polisi la Uingereza kiasi cha £10,000,000 katika upelelezi. Polisi iliwabidi kusafiri India, Ufaransa, Belgium na Marekani ili kukusanya taarifa na ushahidi utakaowasaidia kuweza kuwapata na kuwatia hatiani wahusika wa unyama huo. Katika kesi hiyo zaidi ya nakala 4000 zilikusanywa kama ushaidi katika harakati za polisi kutatua kesi hiyo.
Kutoka katika mwili uliopolewa majini askari polisi walikuwa wameachiwa na huyo marehemu ushahidi muhmu japo uko kwenye kipande kidogo cha karatasi ambao uliwawezesha kujua ni kitu gani kiliipata hiyo familia iliyopotea.
Amarjit Chohan
Mwaka 2003, Amarjit Chohan alikuwa na umri wa miaka 46, alizaliwa India na alihamia Uingereza akiwa ana umri wa miaka 23 kwa lengo la kusaka maisha bora na alifanikiwa kutimiza hilo. Kufikia mwaka 2003 alikuwa mfanyabiashara mkubwa akimili kampuni ya kuhifadhi na kusafirisha mizigo ijulikanayo kama Ciba Freight iliyokuwa na makao yake makuu karibu na uwanja wa ndege wa Heathrow.
Akiwa anaishi katika nyumba yak e iliyokuwa huko Heston Magharibi mwa jiiji la London, Amarjit alikuwa mtu mashuhuri kutokana na uwezo aliokuwa nao na alikuwa ni kipenzi cha watu hasa wafanyakazi wa kampuni yake ambao walimpendea upole wake na uchangamfu wake.
Amerjit alikuwa ni mtu anayependa pesa na muda wote alikuwa akitafuta njia mpya ya kutengeneza pesa zaidi hata kama ingelikuwa siyo halali lakini akaona ingemwezesha kupata pesa ya ziada alikuwa tayari kufanya.
Tarehe 13, mwezi wa 2 mwaka 2003, Amerjit aliondoka ofisni kwake kwa madai kwamba kuna mtu inabidi akutane naye kwa ajili ya mkutano wa kibiashara, kwamba mtu huyo anataka kununua kampuni ya Ciba Freight kwa malipo ya kiasi cha £ 3,000,000 pesa taslimu. Kwa bahati mbaya hakumwambia mtu ni wapi hasa alikuwa anaenda kukutana na huyo mtu na wala hakutaja jina la huyo mtu kwa yeyote.
Lakini jambo la kushangaza ni kwamba hakuonekana tena siku hiyo na siku zilizofuata. Yani ni kama alikuwa kapotea ghafla. Wafanyakazi wa kampuni yake baada ya kutomwona waliamua kutoa taarifa polisi kuwa Chohan haonekani na hajulikani alipo, lakini polisi haawakuchukulia taarifa hiyo kwa uzito kwakuwa kila siku polisi hupokea taarifa ya watu zaidi ya 500 kupotea na siyo kila taarifa uwa sahihi maana watu wengine uwa wanaamua kuondoka tu, wengine uamua kujificha hivyo polisi uwa wanachukulia taarifa kwa uzito pale endapo kutakuwa na jambo ambalo si la kawaida kama kukuta sehemu ya makazi au ofisi ya huyo anayedaiwa kupotea kumevurugwa, au aliwahi kupokea vitisho kabla ya kupotea au uenda alikuwa akijihusisha na biashara haramu. Pia polisi uwa siyo kila taarifa ya kupotea kwa mtu hupokelewa kama taarifa ya mauaji, kwasababu ikichukuliwa hivyo inaweza kuharibu uchunguzi kwa kufanya upelelezi usiyo sahihi na mwisho kuwatoa kwenye mstari.
Pia polisi waligundua kulikuwa na sababu ya Chohan kutaka kukimbia au kupotea. Mwaka 1996, Chohan alikutwa na makosa 13 yanahusu ukwepaji kodi na kuhukumiwa kwenda jela miaka mitatu. Alikuwa ana tabia ya kutumia njia haramu katika biashara kuongeza mapato ambazo alidai alizipata akiwa gerezani. Pia alikuwa kajenga urafiki na watu hatari hasa wa magenge na wanaojihusisha na uuzaji wa dawa za kulevya wengi alikuwa amekutana nao wakati akitumikia kifungo chake.
Kwa hiyo kutoka na mambo aliyokuwa akifanya, muda wote alikuwa akihofia kuwa ikitokea uchunguzi wa aina yoyote kwenye kampuni yake, basi anaweza kukutwa na hatia akarudishwa gerezani. Pia alikuwa na kosa la kuoa mke wa pili aitwaye Nancy ambaye alikuwa ndiye anaishi naye kwa muda huo, pasipo kumtaraki mke wake wa kwanza. Hivyo alijua muda wowote anweza kuwa mikononi mwa vyombo vya dola.
Hivyo kutokana na hayo alikuwa ni lazima aishi maisha ya kuogopa vyombo vya dola na pia kwakuwa alikua ana kampuni ambayo ilikuwa ikiingiza kiasi kikuba cha pesa kila siku alikuwa pia akihofia usalama wake kutokana na watu alikuwa akifanya nao biashara za magendo.
Jambo la kushangaza ni kwamba alipopotea, hakuna aliyetoa taarifa mapema, siyo familia yake wala wafanyakazi wa kampuni yake waliokuwa na hofu juu ya kupote kwake. Ilikuwa ni kawaida kuondoka na asionekane kazini kwake kwa muda mrefu bila kumuaga mtu, lakini wakati wao wakiwaza hayo kumbe Chohan alikuwa kashikiliwa mateka baada ya kutekwa na watu watatu ambao mmoja wa hao watu ndiye alikwenda kukutana naye. Alikuwa kashikiliwa mateka kwenye nyumba iliyoko nje ya mji wa London kiasi cha Maili 100. Humo ndani alikuwa akilazimishwa kupiga simu kwa familia yake na kuwaambia kuwa wasiwe na wasiwasi yuko njiani anarudi, lakini jambo ambalo hakuwa nalifahamu ni kwamba wakati kashikiliwa na kulazimisha kupiga simu, wawili kati ya watekaji hao walikuwa njiani kuelekea nyumbani kwake huko London.
Huko nyumbani kwake ambako alikuwa akiishi na mke wake wa pili aitwaye Nancy, na watoto wao wawili mmoja akiwa na umri wa miezi 18 na mwingine miezi 2 pamoja na mama yake Nancy aliyekuwa katoka India kuja kuwatembelea, walishtushwa na mlngo wa mbele ukigongwa. Mlango ulipofunguliwa, wanaume wawili wakiwa na bunduki walivamia na kuingia ndani kwa nguvu, wakawalazimisha wote kutoka nje na kuingia kwenye gari walilokuja nalo na kuondoka kwa kasi.
Hakuna mtu ambaye alikuwa na ufahamu wa tukio hili kwa siku kadhaa kwamba Chohan na familia yake walikuwa wamepotea kasoro tu wafanyakazi wenzake ambao walipiga simu polisi kutoa taarifa kwakuwa hawakumuona kwa siku nyingi na simu yantumbani kwake ilikuwa ikiita pasipo kupokelewa, lakini pia polisi hawakucukulia kwa uzito taarifa hiyo.
Lakini katika nyumba aliyokuwa kashikiliwa Chohan kuna jambo lilikuwa likiendelea, alikuwa analazimishwa kusaini karatasi tupu zenye nembo ya kampuni yake kwa juu. Watekaji hawa walikuwa na biashara na hizo karatasi tupu walizokuwa wakimlazimisha Chohan kusaini. Waliokuwa wakiishi kwenye hiyo nyumba alimokuwa kashikiliwa Chohan alikuwa Kenneth Regan na baba yake.
Majirani hawakujua kama kuna mfanyabiashara mkubwa kapotea na alikuwa akishikiliwa mateka humo kwenye nyumba ya jirani yao, lakini kuna jambo lisilo la kawaida walikuwa wakihisi linaendelea kwenye nyumba hiyo. Jirani mmoja anadai kuna siku asubuhi sana aliamka akatoka nje, na aliona gari jeupe lilifunikwa bila vioo sehemu ya nyumba (Van). Alisogea hadi nje ya nyumba ya Bwana Regan alimuona Regan akiwa kasimama nje nyuma ya hilo gari. Anadai Regan alipomuona alikuwa kama kashtuka kweli, na hakuongea bali alirudi ndani na kufunga mlango. Jirani anadai taa za ndani zilikuwa zimeasha ila palikuwa kimya sana.
Wiki kadhaa zilipita na hakuna aliyekuwa kashtuka na kuchukua hatua, hakuna aliyejua kuwa hata familia yake ilikuwa imepotea hivyo watekaji mipango waliyokuwa wamepanga ilionekana inaenda sawa sawia kabisa. Huenda mambo yangebaki hivyo kwa muda mrefu, ila Nancy alikuwa ana kaka yake aliyekuwa akiishi Newzealand. Kwa wiki tatu mfululizo alikuwa akijaribu kumpigia Nancy simu lakini alikuwa hapatikani kila anapojaribu. Mwisho akaamua asafiri mpaka London kwenda kuangalia kuna tatizo gani mbona dada yake hapatikani.
Alipofika alishangaa kukuta nyumba ikiwa tupu na hakuna dalili za mtu hata mmoja wa ile familia, jambo hili lilimstaajabisha akaenda kutoa ripoti polisi. Ripoti hii ndiyo iliwashtua polisi kuwa huenda mwanzo walipuuzia kesi ya maana sana, na ndipo walitengeneza kikosi cha makachero wa upelelezi kuanza kufuatilia tukio la kupotea kwa familia nzima. Na ni kwamba kwa muda huo ilikuwa imekwishapita kiasi cha miezi miwili toka familia hiyo ipotee.
Polisi waliwaza kuwa labda kaamua kuondoka na kurudi India kutokana na mambo yake ambayo alikuwa akihofia yanaweza kumrudisha gerezani au kuawa, kumbe pia hata wafanyakazi wake walikuwa wakiwaza kuwa karudi India kwakuwa siku nne baada ya Chohan kupote, alikuja Mzee flani ajulikanaye kama Kenneth Regan aliyedai ameinunua ile kampuni na alikuwa na vithibitisho vyote vikiwa na sahihi ya Bwana Chohan kuthibitisha mauzo ya ile kampuni kwake. Baada ya kujitambulisha na kupokelewa na wafanyakazi alimleta mwanamama ajulikaye kama Belinda Brewin, kuwa ndiye Mhasibu Mkuu wa kampuni wakati mama huyo hakuwa hata na elimu yoyote ya uhasibu, ila alikuwa akimlipa mshahara mkubwa.
Je Kenneth Regan ni nani?
Kwa zaidi ya miaka kumi, Regan aliyekuwa anajulikana kwa jina la utani kama Captain Cash, alikuwa akiingiza madawa haramau UK, akitakatisha pesa chafu na kutengeneza hati feki za kusafiria kwa mamia. Mwaka 1996, alikuwa ni kati ya genge la watu ambao walikuwa kwenye mpango kabambe wa kuingiza kiasi cha tani 15 za bangi yenye thamani ya £40,000,000 Uingereza kwa kutumia nyambizi yake iliyokuwa imetengezwa kienyeji, lakini ilimbidi aitelekeze nay eye kukimbia huku akiacha nyambizi yake ikiwa na bangi hiyo baada ya polisi kugundua mpango huo.
Regan aliamua kujiingiza kwenye biashara ya Bima kafungua kampuni iliyojulikana kama Serez International ikiwa na ofisi zake katika mtaa wa Regent huko katika jiji la London Uingereza. Alitumia biashara hiyo kupitisha na kutakatisha pesa chafu kwa mamilion ya Pound zilizotokana na mauzo ya dawa za kulevya kati ya mwaka 1996 na mwaka 1998.
Yeye na jamaa mwingine ajulikanaye kama William Horncy waliwauzia wasafarishaji wa dawa za kulevya na wahalifu wengine pasi za kusafiria zipatazo 1,000 kwa kipindi cha miaka kumi.
Bahati yake ya kujihusisha na biashara haramu pasipo kukamatwa ilifikia kikomo wezi wa sita mwaka 1998, ambapo polisi walivamia wakati Regan na genge lake wakiwa katika harakati za kuingiza dawa za kulevya eneo la London ya Kaskazini. Regan alijaribu kukimbia kwa kutumia gari lake na alimgonga polsi wa kike na kumjeruhi sana. Alifunguliwa mashitaka ya kujihusisha na uingizaji wa Heroine na kumjeruhi afisa wa polisi. Kwa kujua kuwa anakabiliwa kifungo gerezani kisichopungua miaka ishirini, Regan alikiri makosa yake na kuingia makubariano ya kutoa ushahidi dhidi ya wenzake kwa makubarinao ya kupewa adhabu ndogo zaidi.
Alihojiwa mara 15, na makachero kutoka katika kitengo cha Upelelzi wa makosa ya jinai, na Regan aliwapa taarifa kuhusu genge linalohusika na uingizaji wa dawa za cocaine zenye thamani ya £100,000,000, jambo lililosaidia kukamatwa kwa viongozi wa juu kabisa wa makundi ya uharifu na kukamatwa kwa pesa mamilionii ya pound yaliyopatikana kwa uuazaji wa madawa.
Pia Regan alifanya kazi na polisi katika kesi ambayo ilikuwa ina maika mitano pasipo kupata ushahidi, yeye aliwasaidia kuwapa ushahidi ambao ulisaidia waharifu 15 kufungwa baada ya kupatikana na hatia.
Waashirika wake Regan wao walikataa mashitaka yaliyofunguliwa juu yao, lakini kutokana na ushahidi wa Regan alioutoa juu yao walikutwa na hatia na kupewa vifungo vya muda mrefu.
Jaji alimwambia hivi Regan wakati akimsomea hukumua “ kutokana na ushirikiano uliotoa kwa polisi, hutoaminiwa tena na wenzako, hivyo hutoweza kurudia tena kufanya kazi ya uhalifu, na uadui baina yako na wao utafanya uishi kwa uangalifu… hivyo wale ambao huwageuka waarifu wenzao inabidi wapate punguza kubwa la adhabu.” Regan alihukumiwa kifungo cha miaka minane lakini aliachiwa baada ya miaka mitatu tu.
Jamaa mmoja aliyewahi kuwa mfungwa ambaye hakutaka kutaja jina lake anadai kwamba Regan alijua kamba kuna donge nono limetolewa na ,agenge ya wahalifu kwa atakayefanikiwa kumuua, lakini Regan hakuonyesha kujali wala kuogopa. Anasema alikuwa mtu ukimuuliza kuhusu hilo anakwambia achana na hizo habari. Anazidi kusema kwamba hakuna jinsi yeyote Regan angeweza kuishi kwa mani baada ya kifungo. Anadai kila mtu aliamini akiachiwa tu basi atakuta risasi inamsubiri mtaani.
Alipotoka akiwa ana uhitaji mubwa wa pesa, na akijua kwamba muda wowote anaweza kuawa, Regan alihitaji kumiliki kampuni ya Ciba. Hivyo akamwambia Chohan kuwa anahitaji kununua kampuni yake kwa kiasi cha £3,000,000 lakini ukweli ni kwamba hakuwa na pesa. Badala yake walipokutana karibu na mji wa Stonehenge siku ya tarehe 12, mwezi 2 mwaka 2003, yeye na genge lake la watu wawili wakamteka na kumlazimisha asaini karatasi tupu ambazo walienda kuandika mkataba wa mauziano.
inaendelea kwenye comment #15 na 43