Kizazi kilichopotezwa katika mpango wa mauaji wa kurithi kampuni

Mkuu wa kitengo cha upelelezi Bwana David Little, aliamua kukutana na Belinda Brewin, katika mahojiano aliyofanya naye Belinda hakumwambia jambo lolote la maana ambalo lingeweza kuwasaidia polisi. Ilionekana kwamba huenda Belinda hakuna alilokuwa akifahamu zaidi ya kamba Regan alininunua kampuni ya Ciba.

Lakini Regan alikuwa ameanza kuhisi joto la upelelzi uliokuwa ukiendela na alianza kuhisi muda wowote lazima polisi watamkamata, hivyo aliona bora akimbie mapema. Alichukua usafiri wa feri kuelekea Ufaransa ili akajifiche huko akidhania polisi hawataweza kumkamata. Wenzake aliotenda nao uovu huo yani Peter Rees na William Horncy wao wanakimbia na kujificha kwa Gloster Show.

Kitendo cha Regan kutoonekana ghafla, kilizidi waaminisha polisi kuwa wanakaribia kumkamata muarifu na wako kwenye njia sahihi katika upellezi wao. Wawlikuwa na uhakika kuwa Regan ndiye muajji na huenda amekimbia kujificha kutokamatwa na vyombo vya dola. Lakini swali walilokuwa wakijiuliza zaidi ni wapi ziliko maiti nyingine za familia ya Chohan, pia walikuwa bado hawana ushahidi wa kumuunga Regan moja kwa moja kwenye mauaji hayo.

Pia Bwana Basil Purdue aliyekuwa akichunguza mwili wa Chohan, aliwataarifu polisi kuwa huenda ule mwili ulikuwa umefukiwa kwenye udongo kabla ya kutupwa kwenye maji kwakuwa inaonekana japo umeharibika lakini ulikuwa haujashambuliwa na nzi. Pia maiti ilikuwa na jeraha shingoni ambalio Basil aliwambia polisi huenda lilisababishwa na kukatwa na jembe wakati wa kufukua maiti. Taarifa hii ilibadirisha muelekeo wa polisi katika upellezi.

Polisi uwa wanafahamu wapi pa kuanzia kutazama unapokuwa unatafuta sehemu waarifu wanakoweza kuwa wamefukia maiti baada ya mauaji, kamanda wa polisi Bwana Brian Hook nadai kuwa uwa kuna kushabiiana kwa matendo na kufikiri kwa waharifu.. andai kwamba muarifu anapoamua kufukia mwili wa mtu aliyemuua, ni lazima ataufukia sehemu anayoifahamu vizuri na sehemu ambayo ana uhakika kuwa hakuna mtu atakayeweza kumsumbua. Sasa kutokana na kuwa Regan ndiye alikuwa mtuhumiwa anayehisiwa kwa muda huo, walianza kuchunguza ni sehemu gani ambazo Regan anaweza kuwa alifukia maiti hizo.

Mkuuwa kitengo cha upeleloezi Bwana Little anaamua kumhoji tena Belinda Brewin, na ndipo nawambia kuwa kuna kipindi Regan, na rafiki zaake wawili waliwahi kufanya kikao katika nyumba iliyoko kwenye shamba lake lijulikanalo kama Devon Estate. Na akazidi kuwambia polisi kuwa siku moja alienda shambani kwake ghafla alimkuta Regan na rafiki zake wawili wakiwa wanachimba kitu kama mtaro mkubwa mle shambani kwake lakini hawakumwambia ni kwa ajili ya kazi gani.

Hii taarifa ilitosha kumfanya, Little atume kikosi cha makachero shambani kwa ajili ya uchunguzi, pia walihisi huenda Regan atakuwa kajificha huko. Walipofika hakukuwa na daily zozote za uwepo wa Regan au mtu mwingine, lakini waifanikiwa kugundua sehemu iliyokuwa imetumika kama kaburi na ilikuwa kubwa sana ikiwa ina maana walikuwa wamefukia maiti zaidi ya moja. Hili liliwafanya wazidi kuwa na uhakika kuwa familia nzima iliuawa na kufukia pale na baadae kuhamishwa maana hawakukuta maiti hata moja, Belinda yeye alikana kuwa hakuwa anajua lolote kama shamba lake lilikuwa limetumika sehemu ya kufukia maiti.

Baada ya hapo askari walianza kutazama mawasiliano ya Regan toka siku iliposemekana Chohan alipotea. Walipitia simu alizokuwa akipiga, ujumbe mfuopia aliokuwa akituma na sehehmu alipokuwa kwa kutumia rekodi za minara ya simu. Hivi vyote vilikuwa vikimuweka maeneo yote ya tukio na kutengeneza ushahidi wa kimazingira.

Wakati Bwana Basil Purdue akiandika ripoti ya uchunguzi wa maiti, aliivua maiti nguo na alipoivua soksi, mguu wa upande wa kulia kwenye soksi alikuta karatasi, ambayo ilikuwa imekunjwa. Alipoikunjua alikuta ni karatasi iliyokuwa imechapwa maandishi na ikiwa na anuani ya makazi ya Regan, pia kulikuwa na maandishi ya mkono ambayo ilionekana dhahiri kayaandika marehemu Chohan na alikuwa kaandika kile kilichokuwa kikiendelea kwa ufupi.

Bada ya polisi kupewa hii taarifa, hawakutaka kusubiri maa walikuwa wamekwisha pokea ushahidi wa kujitosheleza, walianza moja kwa moja kumsaka Regan na genge lake. Walianza kwa kufuatilia kamera za baabarani wapate kujua siku ya tukio walitumia gari gani na waliweza kugundua kuwa Regan alikuwa kakodi gari aina ya Van siku ya tukio.

Baada ya kujua namba za usajili wa hilo gari, kwa kutumia kamera za barabarani waliweza kujua mahali lilipokuwa linazungukia kwa muda wote alipokuwa analitumia, pia walilifuata hilo gari kutoka kwenye kampuni alipokuwa kalichukua na polisi walianza kulifanyi ukaguzi wa kitaalamu ili kuona kama kuna chochote kitakachoweza kuaonyesha kama familia ya Chohan iliwahi kuwa mle kwenye gari.

Gari lilionekana kuwa lilikuwa limeosjwa kiwa kutumia maji yenye presha kali lakini, kitu ambacho watu hawajui maji ya hivyo uwa hayaondoi ushahidi ili uwe yanauficha kwa kuusukuma kwenye maeneo yaliyojificha kama kwenye mikunjo ya vyuma. Hivyo baada ya hilo gari kupelekwa kwenye maabara ya polisi kwa uchunguzi, polisi waliweza kupata ushahidi wa maji maji ya mwili ya familia ya Chohan na walikkuwa wameweza kupata ushahidi kwamba ni kweli ile familia iliwahi kuwa kwenye gari hilo.

Pia polisi wanaamua kwenda kufanya upekuzi kwenye makazi ya Regan na baba yake kule Wiltshire, wanakuta kila kitu ndani kimebadirisha na kutengenezwa upya hivyo wnakosa ushahidi, lakini wakati wakichunguza mazingira ya nje wanakuta kuna tone la damu ukutani ambalo walipochukua na kupeleka maabara inagundulika kuwa ni damu ya motto wa Chohan aliyekuwa an miezi miwili, na mahali lilipokuwa polisi wanaamini kwamba alikuwa amekwishauawa wakati wakubeba maiti ndipo ikagusa hapo ukutani na kuacha tone hilo.

Polisi walipata taaarifa kuwa Regan alikua ameshuka kwa feri na kuingia mji wa Calais na alikuwa njian kuelekea Uhispania,. Akiwa kafika nchi ya Ubeligiji, polisi wa Uingereza waliwasiliana na polisi wa Ubeligiji ili wamfuatilie na kumkamata na kweli aliweza kukamatiwa huko, ambapo utaratibu wa kumsafirisha kurudi Uingereza ulifanyika.

Kikosi cha polisi kitengo cha uzamiaji kilizama eneo mwili wa Chohan ulipokutwa unaelea kujaribu kutafuta miili iliyobaki na walifanikiwa kupata mwili wa Nancy na mwili wa Kaur. Nancy iligundulika aliuawa kwa kupasuliwa kichwa kwa kutumia nyundo, huku mama yake Nancy yani Bibi Kaur mwili wake ulikuwa umeharibika vibaya hivyo ilishindikana kujua chanzo cha kifo chake. Miiwli ya watoto hakuweza kupatikana kabisa mpaka leo ila polisi walihitimisha kuwa na wao wameuawa.

Regan na wenzake walifungulia mashitaka ya kuteka na kutenda mauaji ya watu watano wa familia moja. Kesi yao ilichukua miezi nane mpaka kuhukumiwa na wote walihukumiwa vifungo vya maisha tarehe 1 mwezi wa 7 mwaka 2005, ikiwa ni baada ya miaka miwili toka watende kosa hilo.

Katika utetezi wake Regan alidai kwamba polisi walimtegeshea ushahidi wa uongo kwenye mwili wa marehemu ili waweze kumfungulia kesi ya uongo ya kutenda mauaji. Polisi wao walikana utetezi wa Regan na wakadai kwamba Chohan kwa kujua hatima yake aliamua kuwaachia ujumbe utakaowasaidia polisi kutatua fumbo la ni kitu kilichotokea.

Mwisho

Tukutane tena katika story nyingine
pia kwa ambao hamjasoma story ya Mauaji katika fungate link ni hii hapa chini

Mauaji katika Fungate (je ni kweli Shrien Dewan alipanga mauaji ya mke wake?)
 
Kwanini Mods wasiunganishe hizo post mbili #15&43 zikaletwa mwanzo wa thread ili kutoa usumbufu kwa waliopendezwa na huu uzi kuzitafuta?wakuu fanyeni hivyo basi
 
Mkubwa usiache kunitag kwa story mpya
 
Back
Top Bottom