Kizazi kilichozaliwa kuanzia miaka ya 1975 hadi 1995 ndicho kizazi bora zaidi kutokea

Kizazi kilichozaliwa kuanzia miaka ya 1975 hadi 1995 ndicho kizazi bora zaidi kutokea

Nikitoka sitorudi. Bora nile hustle ya mwisho mwisho, staki kuwa hero kwa sasa maana bado nina empty cup. At least miaka mitano baadae nitafikiria zaidi😁
Kurudi ni muhimu mkuu ili mafanikio yako yawe na thamani ina bidi yapimwe katikati ya ufukara😁
 
Kurudi ni muhimu mkuu ili mafanikio yako yawe na thamani ina bidi yapimwe katikati ya ufukara😁
Ahh wapi mkuu 😁 kila mtu atakufa na mzigo wake. Yes unaweza kujali watu na kuwasaidia sana lakini kama huridhiki au kufurahia maisha yako. Kutakuwa na sababu gani ya kuishi.

Ngoja nijipange nije huko kuongeza life expectancy 😁
 
Hicho kizazi kina watu dhaifu saana... Ni bora Tz watu wasingezaliwa kuanzia 1975-1995 ( kizaz kina waoga,waongo,wavivu,wajinga, saana)
 
Nyie
Kizazi cha 1975-1995 hakukuruhusu Nyerere atawale, kumbuka kipindi kizazi hiki.kinaingia duniani ndipo Nyerere nae akaona hakuna haja ya kuendelea, '85 akang'atuka.

Kizazi bora kabisa, naweza kusema 1975-1990. Kinashuhudia mabadiliko makubwa ya dunia, innovation nyingi zimefanyika kipindi hiki, digitalisation, matumizi ya modern technology kizazi hiki kinahusika.

Bahati mbaya sana, kizazi hiki kimezaa kizazi cha hovyo kuwahi kutokea duniani, kizazi cha 2000.
Hiko kizazi mlikuwa wabinafsi sana ndiyo mmeifikisha nchi hapa ilipo mngekuwa mnajielewa nchi ingefika mbali sana
 
Hamna kizazi bora kuwahi kutokea kati nchi hii vizazi vyote ni vya kishenzi tu
 
Nyie
Hiko kizazi mlikuwa wabinafsi sana ndiyo mmeifikisha nchi hapa ilipo mngekuwa mnajielewa nchi ingefika mbali sana
Sio kizazi cha 1975-'90, kizazi kilichoiua hii nchi ni 1955-'75 ambao wengi bado wapo madarakani.
 
mnabishania vizazi nyie wote hamna kitu kabisa!.
 
nakubaliana na wewe 100% hapo israel watoto wa miaka kuanzia miaka 15 na kuendelea wanafanya mambo makubwa usipime.
Tukitaka nchi yetu iendelee tubadiloshe mfumo wetu wa elimu. Hapa Tz mwanafunzi anandoto za kuwa Engineer lakini anafundishwa laboratory safety and apparatus akiwa na miaka 14 (form one) mpaka anamaliza form 4 amesoma vichache vinavyohusiana na Engineering matokeo yake anakosa motisha.
 
"Watu waliozaliwa kati ya mwaka 1975 na 1995 ni kizazi cha kipekee zaidi katika historia, na hii ndiyo sababu:

Walizaliwa kati ya vizazi viwili: kimoja kabla ya mtandao wa intaneti na teknolojia kuchukua nafasi kubwa, na kingine kilichofuata baada ya hayo.

Kizazi cha kabla ya 1985 kilikuwa cha kizamani, kikiamini katika kazi ngumu na thabiti, wakati kizazi kilichofuata kinaamini katika kufanya kazi kwa akili zaidi.

Kizazi hiki kimepitia yote: redio, televisheni, Mario Bros, Nokia, kanda za kaseti, VHS, DVD, Nintendo, PS4, maduka ya video, Netflix, Snapchat, na uhalisia wa mtandaoni (virtual reality).

Hiki ni kizazi kinachojua mila na desturi, lakini pia huhoji na kutoa maamuzi kwa kuzingatia mantiki. Kizazi kilichopita hakikuhoji, na kizazi kijacho hakijui mila na desturi.

Kikiwa daraja kati ya enzi ya viwanda na enzi ya mtandao, kizazi hiki kinaelewa pande zote mbili kwa uzoefu. Kizazi hiki kinapaswa kuwa kinachoongoza kila kitu. Kizazi cha zamani hakielewi kinachoendelea sasa, na kizazi kijacho hakijui asili ya kile walichonacho."
Hakuna kizazi kilichobora zaidi ya mwenzake.
Millenials wengi ilikuwa ni rahisi kupata kazi, kutokana na ubize wao wa kazi wakakosa muda mzuri wakuwalea hawa gen z. Ndo maana gen z wanepotoka kimaadili lakini walezi wao(millenials) ndo sababu ya hii.
Pia siku hizi ajira ni chache alaf wasomi wengi so Gen Z wengi wanaishia kubet na kudanga kutokana na ajira kuwa chache na wakati millenials wanawalaumu gen z kwenye masuala ya kubet wanasahau wao ndo wanawajibika kuongeza nafasi za ajira na kuzuia kampuni za kubet kwa kuwa millenials wengi wapo serikalini hasahasa wabunge lakini wanabaki kuwalaumu Gen Z.

Mungu hajawahi kuumba kizazi kilichobora zaidi ya mwenzake ni mazingira kinachoinfluence kizazi kiwe cha namna fulani.
 
Back
Top Bottom