''WAKATI mjadala wa matokeo mabaya ya kidato cha nne ukiendelea kulitikisa taifa, kashfa mpya ya matokeo hayo imeibuliwa.
Kashfa hiyo mpya imeibuliwa na Mkurugenzi wa Shule ya Green Acres, Julian Bujugo, kwamba matokeo ya baadhi ya shule nchini ikiwamo yake yamechakachuliwa.
Akizungumza na gazeti hili jana, Bujugo alisema kuwa baadhi ya wanafunzi kwenye shule yake hawakufanya mitihani ya kidato cha nne, lakini matokeo yanaonesha wamefaulu kwa kupata alama za juu.
Alitaja mfano wa mwanafunzi, Humphrey Sanga, mwenye namba 01197/148, ambaye hakufanya mitihani hiyo lakini matokeo yanaonesha amefaulu kwa kupata alama nzuri.
Huyu mwanafunzi tulimsimamisha na hakufanya mitihani, lakini matokeo yake yanaonekana amepata hivi; Civics D, Historia D, Jiografia C, Kiswahili D, English C, Physics D, Chemistry C, Biology C, Basic Mathematics D, ambapo amepata daraja la tatu pointi 24, alisema Bujugo.
Alimtaja mwanafunzi mwingine, Martin Rushaigwa, namba 01197/0173, ambaye alifanya masomo ya Arts.
Alisema matokeo ya mwanafunzi huyo yanaonesha kuwa ameongezewa alama za masomo ya biashara ya Bookeeping na Commerce, ambayo hakuyafanya kabisa.
Alimtaja mwanafunzi mwingine aliyefanya mtihani huo lakini matokeo yake yanaonesha amewekewa absent na mwanafunzi mwingine, Mbazi Volta, hakufanya mitihani lakini amepewa alama za ufaulu.
Matokeo hayo yananipa wasiwasi kwamba yanaweza kuwa yamechakachuliwa, alisema Bujugo.
Mkurugenzi huyo anaiomba Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kurudia kusahihisha mitihani hiyo ili kuondoa ukungu ulioligubika taifa kwa sasa kuhusu matokeo ya kidato cha nne.''
Source: Tanzania Daima 21 Feb 2013
Ikithibitika kama hili ni kweli, mheshimiwa rais JK please timua hiyo timu ya wizara ya elimu na uweke wachapa kazi wengine.
Waziri wa elimu na Ndalichako watakuwa wameshindwa kutekeleza majukumu yao.