Kizungumkuti Dowans

Kizungumkuti Dowans

Nakushukuru Gurudumu. Post imekuwa baridi. Bado kiu yangu ya kutaka kujua ni nini mchango wa chama cha siasa haijakatika. Je ni kuwaambia wananchi kuhusu matatizo yao? Mbona wananchi wanayajua kwa sbabu wao ndio 'wanaishi' hayo matatizo! Na magazeti yanawajulisha wananchi pia!

Kwa mfano, wachumi wa vyama vya siasa wanasemaje kuhusu deni la taifa? Wanasheria wanasemaje kuhusu Dowans? Nk
 
Nimekuwa kimya siku nyingi nikisoma tu michango ya wanaJF juu ya suala hili la Dowans na matatizo ya TANESCO. Naomba kwa leo nitoe background kidogo jinsi ninavyolielewa.

Pesa za EPA zilizosombwa toka BoT na Rostam Aziz mwaka 2005, zikapelekwa CRDB branches za Dar es Salaam ni jambo ambalo hakuna ubishi. Ni sehemu ya historia ya Benki Kuu ya Tanzania.

Kuna hata ripoti kwamba Gavana Ballali ndiye alishauri fedha hizo zitumike baada ya bosi wake Benjamin Mkapa kumwuliza ushauri juu ya namna ya kupata fedha za kampeni za CCM "kumsaidia huyu malaika"! Inasemekana kwamba TShs 40 bilioni, zikitokea EPA, zilipasishwa na Rostam Aziz kwa CCM, wakati huo akiwa ni Treasurer wa Chama cha Mapinduzi. Zilimsaidia "malaika" kweli!! Akashinda kwa kishindo!

Pamoja na kuunda kampuni ya Kagoda Agriculture Limited, R.A. alitumia fedha nyingine za EPA kuagiza turbines (mitambo ya umeme), kampuni feki ya Richmond Development,PLC. ikiingia katika mkataba na TANESCO kuzalisha umeme wa dharura. WanaJF mnafahamu kuwa kulikuwa na shinikizo toka kwa wakubwa ili mkataba huu utiwe saini haraka haraka.

Mkataba ulikuwa unalazimisha TANESCO walipe "capacity charges" hata wakati mitambo haitumiki kuzalisha umeme. Mitambo haitumiki wakati Tanesco wanazalisha umeme wa kutosheleza kwa kutumia mitambo yake ya kawaida kama maporomoko na mabwawa ya Mtera, Kihansi, Hale. Myumba ya Mungu na mitambo yao ya dizeli ya Ubungo n.k.

Itakumbukwa kwamba janja janja hizi zilifichuka wakati Kamati ya Mwakyembe ilipoundwa Bungeni mwaka wa 2007/2008. Ikabainika kuwa sio tu Richmond ilikuwa kampuni feki, bali hata uwezo wake uliotangazwa na kuzingatiwa katika kufikiwa bei, haukuwa sahihi. Ndipo pia ilipobainika kwamba kulikuwa na undue pressure toka kwa mawaziri ili mkataba usainiwe. Matokeo yake ni kwamba Waziri Mkuu na mawaziri wengine wawili walilazimika kujiuzulu.

Baada ya kashfa ya Richmond, kampuni ya Dowans (Tanzania) Ltd ikajitokeza ikanunua na kuridhi mitambo na mashughuli ya Richmond. Ilisemekana hisa za Dowans (Tanzania) Ltd hapo mwanzo zilikuwa za Mwana Mfalme wa Kiarabu. Lakini huyu Prince amekanusha kuwa hahusiki. Mwenye hisa mwingine, Dowans (Costa Rica) ni feki pia, kwa vile Serikali ya Costa Rica imethibitisha kuwa hakuna kampuni yenye jina hilo ktk orodha ya kampuni zake.

Nimesoma hii hukumu ya ICC, na kesi ilivyoendeshwa huko Paris; na Rostam Aziz anatajwa kwamba ni mmoja wa wanaohusika katika umilikaji wa Dowans (Tanzania) Limited.

Kutokana na maelezo niliyotoa, hasa kuhusiana na kuwa Richmond na Dowans ni kampuni feki, zinazohusiana na ukwapuaji wa fedha za umma toka Benki Kuu 2005 na ufisadi wa hali ya juu hapa nchini, hakuna uhalali wowote wa kulipa fedha za Serikali ama za TANESCO kwa Dowans.

Napendekeza kwamba, licha ya masharti ya Ibara Na. 24(2) ya Katiba yetu inayokataza kutaifisha mali ya mtu binafsi bila fidia, Serikali ya Tanzania ina uhalali wa kutwaa mali zote za hii kampuni bila fidia.

Kama ni kweli kwamba Richmond na Dowans chanzo chao ni fedha za EPA zilizokwapuliwa toka Benki Kuu ya Tanzania, hata hawa wakubwa wanastahili kufunguliwa kesi za jinai. :clap2:

Sometimes I wish Mwalimu Nyerere was alive.

Du nakubaliana kabisa na wewe Mzee wangu Richmond na Dowans wasilipwe kabisa kama mtandao wenyewe ni huo, kwani hata CRDB walichota kuagiza mitambo hiyo na bill za Tanesco tulilipa. Leo Watanzania wote tunadaiwa upya ni halali kweli au tuingie barabarani.
Keep it-up E. Mtei
 
Hakuna cha High court.

Behind the rulling hii kama nikweli kuna peoples power. watu hawajaingia mtaani lakini serikali imeshaanza ku feel the pinch. Bila presure ya wanachi hata rulling ya Higcourt inaweza kuwafavor Dowans.

Hata mahakama ikimua kwa favour ya TANESCO bado naamin nisababu ya shinikizo la wanachi sio kwasababu walipenda kufanya hivyo.

Tumewalazimisha watafute sababu ambazo ni za kweli . Kwa nn walikuw awanazifumbia machooooooo

Bravo JF na wanaharakati wote
 
sikia mr.ZUZUBRAIN we umetumwa ulaghai watu na pumba zako.....................umtukosa
 
msando,ni ngumu san kucooperate eftcvlty na gvt iliyoingia madarakani kwa wizi wa kura!that is why its very dangrs to temper wiu democracy!
 
pengine tuambie cdm mmejipangaje juu ya hayo ndipo tuanzie mjadala

Katika hili kofia ya CDM nitaiweka pembeni kwa muda nakujikosoa mwenyewe. Sijasikia tamko au taarifa yoyote ya chama inayoelezea kwa kina kuhusu deni la taifa, madhara yake na nini kifanyike au CDM itafanya nini kuzuia deni hilo lisongezeke na mwisho lipungue!

Bado kuna uzito wa kuandaa taarifa hizo na hii inawezekana ni kwa sababu mbalimbali ila naamini kwamba kama chama makini na chenye nia ya kuikomboa hii nchi ni lazima kuwe na watalaamu ambao wanafanya kazi 24/7 kutoa suluhisho kwa matatizo specific badala ya kutegemea majibu ya ilani ya uchaguzi au sera za chama!

Lazima kuwe kuna timu ya wanasheria ambao wanaweza kuandaa a legal opinion kupingana na alichosema mwanasheria wa serikali! Hatujafanya hilo! yametolewa matamko lakini sio kwa mfumo ninaousema hapa!

Ni kutokana na gap hiyo ninayoiona ndio maana umuhimu au nafasi ya vyama vya upinzani inakuwa questionable! Hawawezi kutegemea bunge na mikutano ya hadhara kama sehemu za kusemea!
 
Kufa kufaana,umaskini wa Tz,pamoja na ukosefu wa kazi si kwa sababu nchi haina rasilimali,bali ni uongozi mbovu,na mwananchi wa kawaida hawezi kuelewa maana ya deni la taifa,naamini ni wajibu wa chama cha siasa kuwajuza na kutumia nafasi hiyo kujijenga wananchin lakini pia kutumia nafasi hiyo kjijenga,hili halikwepeki,maana msingi wa uchumi mzuri,ni siasa safi na uongozi bora,hatuwezi kutenganisha matatizo ya msingi ya nchi hii na uongozi mbovu na wa kihuni wa ccm
saa ya ukombozi
 
tusifate mkumbo tuwe na utamaduni wa kusikiliza pande zote mbili na kutoa maamuzi kama Mungu alivyotufundisha. Hii ndo maana ya akili,busara na hekima.
 
Jana kwenye pita pita yangu nilikutana na Mjumbe mmoja wa Bodi ya Tanesco. Katika maongezi nae nilimuulizia kuhusu suala la Dowans. Kwenye maelezo yake ni kuwa malipo ya Dowans ni halali kabisa, kwani wanacho kidai ni gharama za umeme ambao wao walizalisha na hawakuwahi kulipwa na Tanesco mpaka mkataba pale ulipo vunjwa.
Kwa maana hiyo basi, wanadai hela yao halali kabisa ambayo umeme ulizalishwa na mie na wewe tuliutumia. Sasa hapo malipo ambayo sio halali ni yepi ? au tuna nia ya kudhulumu haki za watu ?.

Na kuhusu hukumu ya mahakama ya ICC wao vitu walivyo uliza ni vichache tu, kama mitambo ipo wapi ? ilizalisha umeme au haikuzalisha ? huko nyuma walikuwa wanawalipa au hawakuwalipa? Mkataba ulivunjwa kabla ya muda ?. Majibu ya maswali yote hayo ni ndio, ndipo mahakama ikatoa huku ya Dowans kulipwa haki yao kwa kile walichotuzalishia na kukitumia.

Hii siwezi kukubali hata kidogo mimi! nasema sikubaliani nawewe sijui nanani huyo unaemsema aaaaaaah! wapi!!!!!!!!!!!1
 
Judiciary studies Dowans ruling registration request




By The guardian reporter



27th January 2011


email.png









Mvungi(7).jpg

Dr Sengondo Mvungi




Issue of whether the international court ruling awarding 94bn/- to Dowans should be registered by the High Court awaits final decision by higher judicial authorities, Deputy Registrar Salvatory Bongole said yesterday.
The latest statement by the High Court Registrar’s office follows reports that the ruling had been submitted for registration.

“We have decided to forward the matter to the judicial authorities because of its sensitivity,” he told reporters, who wanted to know about the registration of the Award.
“At the moment, I cannot say anything about the Dowans Award registration. We are waiting for the higher judicial authorities to discuss the matter and make a final decision. This is a sensitive and international law issue,” Bongole explained.
The Deputy Registrar also declined to explain what he meant by “high judicial authorities” where the matter had been forwarded.

Instead, he said his office expected to receive feedback on the decision today.
“After the decision of the higher judicial authorities, we will see if there is a need to summon Dowans to start processes for registering the Award,” said the Deputy Registrar.
According to international laws Dowans cannot be paid compensation until the International Chamber of Commercial (ICC) ruling is registered at the High Court.
The government said on Monday it would appoint a team of legal experts to explore all legal avenues to save the nation from the burden of paying Dowans the 94bn/- penalty for breach of contract.

The move followed a resolution by members of the ruling CCM parliamentary committee calling on the government to find legal ways of reducing the amount to be paid to Dowans or to not pay at all.

Recently, activists under the umbrella of the Legal and Human Rights Centre (LHRC) filed a case at the High Court (Commercial Division) to block a government decision, announced by the minister for Energy and Minerals, William Ngeleja to pay the power firm 94bn/-.

According to LHRC Executive Director Francis Kiwanga, the High Court (Commercial Division) is expected to set up the date and appoint a judge for the hearing of the case tomorrow.

“In our application, we asked the High Court to speed up the hearing of the case. We hope it will do so. We are challenging the hefty compensation. It is a huge amount of money, which is unfair to pay to Dowans,” Kiwanga told a press conference.
The LHRC has contracted prominent constitutional lawyer and university lecturer Dr Sengondo Mvungi to represent them in court.





SOURCE: THE GUARDIAN
 
• Sasa kuibana serikali kila kona mpaka walipwe HATIMAYE kampuni ya kufua umeme ya Dowans Holdings SA na Dowans Tanzania Ltd zimewasilisha rasmi ombi la kuomba fidia ya sh bilioni 94 isajiliwe katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam. Fidia hiyo ni ile iliyoamriwa kulipwa na TANESCO kwa kampuni hiyo baada ya shirika hilo la ugavi wa umeme nchini kutiwa hatiani na mahakama ya kimataifa ya usuluhishi migogoro ya kibiashara (ICC), kwa kile kilichoelezwa kuwa ilivunja mkataba baina yake na kampuni hiyo kinyume cha taratibu. Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana mchana jijini Dar es Salaam, Naibu Msajili Mwandamizi wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, Salvatory Bongole, alisema ombi hilo la Dowans dhidi ya TANESCO, liliwasilishwa Januari 25 mwaka huu mahakamani hapo na wakili wa kujitegemea ambaye anaiwakilisha kampuni hiyo, Kennedy Fungamtama. Bongele alisema ombi hilo limepewa namba 8/2011 na jaji wa kulisikiliza ameshapangwa ingawa tarehe ya kuanza kusikilizwa kwa ombi hilo bado haijapangwa. “Kimsingi Dowans imeshawasilisha ombi la kuiomba Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam isajili tuzo ya fidia ya sh bilioni 94 waliyoishinda TANESCO katika Mahakama ya ICC…na kweli mahakama imelipokea ombi hilo na kulipatia namba na jaji wa kuanza kuisikiliza…na tuzo hiyo iliwasilishwa hapa Mahakama Kuu na mahakama ya ICC wiki iliyopita. “Kwa hiyo naomba Watanzania wafahamu kuwa tuzo ya hukumu iliyotolewa na ICC kwa Dowans iliwasilishwa mahakamani hapo wiki iliyopita na iliwasilishwa na mahakama ya ICC yenyewe kwa kuwa huo ndiyo utaratibu wa sheria unavyotaka. “Na kilichofanywa na Dowans Januari 25 mwaka huu, kupitia wakili wao Fungamtama ni kuwasilisha ombi la kuiomba Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam isajili tuzo yao hiyo …kwa hiyo ieleweke kwamba tuzo ya Dowans bado haijasajiliwa kwani taratibu za kisheria zina kwenda hatua kwa hatua, ”Alisema Bongole. Hata hivyo, taarifa nyingine za uhakika zinasema kuwa Dowans pia imesajili ombi lao hilo katika mahakama moja nchini Uingereza na kwamba mahakama hiyo inatarajia kutoa notisi ya siku 21 kwa TANESCO kutoa utetezi wake kuhusu kuridhia au kukataa kulipa fidia hiyo. Hatua hiyo imeelezwa kuwa ni mbinu ya tahadhari iliyochukuliwa na kampuni hiyo ili kujihakikishia kuwa inalipwa fidia yake hata kama maamuzi ya mahakama kuu ya hapa nchini yatabatilisha fidia yao waliyotunukiwa na ICC. “Iwapo mahakama hiyo ya Uingereza itaridhia moja kwa moja kulipwa kwa fidia hiyo na TANESCO ikikataa, basi Dowans watawatumia mawakala wa kitaifa wanaofanya kazi ya kufilisi mali za wadaiwa, ili wakamate mali za serikali ya Tanzania zitakazolingana na thamani ya fidia hiyo ya sh bilioni 94,” alithibitisha zaidi mtoa taarifa wetu. Tuzo hiyo ya Dowans iliamriwa na ICC Novemba 15 mwaka jana baada ya kampuni hiyo kuishinda TANESCO katika kesi yake ya kudai fidia ya kuvunjiwa mkataba iliyokuwa imefunguliwa rasmi Novemba 20 mwaka 2008 na kupewa namba 15947/VRO. Tangu ICC itoe hukumu ambayo iliipa ushindi Dowans baadhi ya wananchi, wanasiasa wakiwemo na mawaziri walijitokeza hadharani kuitaka serikali isilipe fidia hiyo kwa madai kuwa kuilipa ni sawa na kuwazawadia mafisadi waliolidanganya taifa tangu ilipoletwa kwa kampuni dada ya Richmond ambayo baadaye ilikujagundulika kuwa ni ya kitapeli. Hata hivyo, wanasiasa wachache wamekuwa wakiitaka serikali ilipe fidia hiyo kwani kutofanya hivyo ni kukiuka misingi ya utawala wa sheria na mikataba mbalimbali ya kimataifa kuhusu haki za raia na mataifa ambayo Tanzania imeridhia kuiheshimu na kuitekeleza. na Happiness Katabazi Tanzania Daima
 
Mkuu Masando hiyo kofia ya chama usiweke kando tutakunyang'anya.....Umetoa ushauri mzuri sana tunaomba chama kiwe na watumishi wa kutoa majawabu ya matatizo ya watanzania kitaalamu na siyo kisiasa kwa hiyo kunahitajika kuwa na wataalamu ambao kazi yao itakuwa kushirikiana na viongozi wa chama kutoa hoja au majibu mbadala ya chama. Kwavile kwa kufanya hivyo chama kitaonesha kwa wananchi uwezo wake wa namna ya kutatua matatizo ya watanzania. Au viongozi wetu wa juu wawe makini katika kutoa majawabu mbadala ya matatizo chungu mzima ya watanzania.
 
Mzee Mtei tunashukuru sana kwa mchango wako kuhusu DOWANS. Haya ndiyo mambo tumefanyiwa kwa muda mrefu sana hapa Tanzania mpaka baadhi yetu wakaibatiza nchi kuwa ni "shamba la bibi". Hawa criminal gangsters wanafanikiwa kuwashawishi viongozi wetu wakijifanya kuwa ni wawekezaji lakini wanakuja nchini bila chochote. Wanatafuta kipande kidogo tu cha ardhi tena cha kukopeshwa na aliyetangulia,mara wanapata mikopo mara wanaanza kuingia Ikulu kama wanaingia bafuni. Hapa ndiyo matatizo mengi yameanzia na ndiyo maana tumefika hapa. Mkapa aligeuza Ikulu kuwa soko la biashara zisizoeleweka au zisizo na faida kwa Taifa. Katika safari zangu nje nimewahi kukutana na kijana wa kihindi na wakipakistani (mwanzoni nilidhni wote ni wahindi) walipofahamu mimi ni mtanzania wakaanza kuisifu Tanzania wakisema ni nchi nzuri ina amani. Nikawashtukia nikawauliza mmejuaje nanyi mmesema hamjawahi fika huko? Wakasema hatujafika lakini tunajua, tunajamaa zetu huko wanasifu sana nchi yenu. Nikawadadisi mpaka hatimaye wakakiri kuwa ndugu zao walikuja hawana chochote lakini sasa ni matajiri wa kupindukia. Wakakiri pia kuwa nchi yenu inaheshimu sana wageni. Eti mgeni akija anaweza hata kupata Mkopo wa mamilioni bila kubaguliwa na anaanzisha biashara kubwa tu na watu hawana ubaya. Mmoja akarukia, 'hata ardhi ya nchi wanauziwa kubwa tuu bila kujali ukubwa wake hata uraia wao'. Maneno ya viijana hawa yalinifanya nikaota vipele mwilini kwa kukumbuka watu wanvyotaabika na umaskini nchini.
Dowans ni muendelezo tu wa alichokianza Mkapa, EPA, Kagoda, Meremeta Deep Green etc etc. Kwa hali ilivyo sasa ingebidi serikali ya Kiwete ifanye maamuzi mazito, kama unavyoshauri, ya kuwageukia na kuwauliza walivyopata fedha za kununulia hiyo mitambo na wakishindwa ku-prove then kila kitu kitaifishwe na wamiliki wawekwe ndani kwa manufaa ya umma. Hili ndiyo litakuwa suluhisho la hili swala la DOWANS/RICHMOND saga.
 
Hii sinema tamu......wale wajuzi wa sheria ambao wametoa hoja na rai nzuri hapa JF sasa ni wakati muafaka kuchukua hatua ili kuokoa hayo mahela. Mahela yatakayosaidia kupata paracet katika zahanati zetu.
 
kama ni cinema ya kihindi basi hapa ilipofikia kama sio Intermission, au sterling anaenda kumuokoa mama yake na demu wake, sasa tuone kama atafanikiwa kuwaokoa kwa Adui ashanti, yangu macho.
 
Jana kwenye pita pita yangu nilikutana na Mjumbe mmoja wa Bodi ya Tanesco. Katika maongezi nae nilimuulizia kuhusu suala la Dowans. Kwenye maelezo yake ni kuwa malipo ya Dowans ni halali kabisa, kwani wanacho kidai ni gharama za umeme ambao wao walizalisha na hawakuwahi kulipwa na Tanesco mpaka mkataba pale ulipo vunjwa.
Kwa maana hiyo basi, wanadai hela yao halali kabisa ambayo umeme ulizalishwa na mie na wewe tuliutumia. Sasa hapo malipo ambayo sio halali ni yepi ? au tuna nia ya kudhulumu haki za watu ?.

Na kuhusu hukumu ya mahakama ya ICC wao vitu walivyo uliza ni vichache tu, kama mitambo ipo wapi ? ilizalisha umeme au haikuzalisha ? huko nyuma walikuwa wanawalipa au hawakuwalipa? Mkataba ulivunjwa kabla ya muda ?. Majibu ya maswali yote hayo ni ndio, ndipo mahakama ikatoa huku ya Dowans kulipwa haki yao kwa kile walichotuzalishia na kukitumia.


Kweli Tanzania kuna mambo!

Mwisho wa siku yote yatajulikana. Ebu tusubiri hukumu isajiliwe mahakama kuu.

Kuweni makini na wajumbe wa Bodi zetu, umesahau wa BoT walisema Liyumba aliongeza ghorofa bila izini yao!

 
Back
Top Bottom