Kizza Besigye apelekwa hospitali akiwa mahututi, Afya yazidi kudorora

Kizza Besigye apelekwa hospitali akiwa mahututi, Afya yazidi kudorora

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,153
Chama cha People’s Front for Freedom (PFF) kimetoa tahadhari kali kuhusu hali ya afya ya kiongozi wake, Kizza Besigye, kikisema kuwa hali yake imedhoofu zaidi akiwa kizuizini.

Kwa mujibu wa chama hicho, Besigye akiwa mahututi alihamishwa usiku wa manane kutoka gereza la Luzira kwenda kituo cha afya kilichopo Kijiji cha Bugolobi chini ya ulinzi mkali, bila maelezo rasmi kutolewa kuhusu matibabu aliyopata.

PFF imesema hatua hiyo imeongeza hofu miongoni mwa wafuasi wake na kuibua maswali kuhusu namna kiongozi huyo wa upinzani anavyotendewa akiwa kizuizini.

Chama kimeilaumu Serikali na mamlaka za magereza kwa ustawi wake, kikitaka familia na madaktari wake binafsi waruhusiwe kumwona bila vikwazo vyovyote.

Chama hicho kinasisitiza kuwa kuendelea kushikiliwa kwa Besigye ni kinyume cha sheria na kimetaka aachiliwe mara moja ili apate matibabu anayostahili. Wafuasi na waumini wa demokrasia wamehimizwa kuendelea kumuombea, huku PFF ikiahidi kutoa taarifa zaidi kadri zitakavyopatikana.

Besigye amekuwa kizuizini tangu Novemba 2024, baada ya kuchukuliwa kinguvu na maafisa wa Polisi huko Nairobi Nchini Kenya alipokuwa akihudhuria uzinduzi wa kitabu cha Mwanaharakati wa Haki za Binadamu na Mwanasiasa nchini humo, Martha Karua.

Baadaye alifikishwa katika mahakama ya kijeshi nchini Uganda akikabiliwa na mashtaka mbalimbali, huku wakili wake akieleza kuwa afya yake imeathirika vibaya kutokana na kifungo cha muda mrefu, jambo ambalo limezua wasiwasi mkubwa miongoni mwa mashirika ya haki za binadamu.

1768976626833.png

===========

Ugandan opposition leader Besigye in critical condition, party says​


Kampala. Uganda’s opposition People’s Front for Freedom (PFF) has claimed that the health of veteran opposition figure Dr Kizza Besigye has deteriorated to a critical level, saying he was rushed from prison to a medical facility under tight security.

In a statement posted on X in the early hours of Tuesday, January 20, the party said it had received what it described as “credible reports” that Dr Besigye had been transferred overnight from Luzira Prison to a medical facility in Kampala.

“The People’s Front for Freedom wishes to inform the public and all supporters of freedom that the health of our leader, Dr Kizza Besigye, has reached a critical and deteriorating state,” the party said, without giving further details about his condition.

PFF claimed that Besigye was taken to a medical facility at Bugolobi Village Mall under heavy security and accused Ugandan authorities of denying him adequate medical care.

“It is tragic that a man who has devoted his life to the health and freedom of others is now being denied his own right to medical dignity,” the statement said, adding that prison authorities and the government should be held fully responsible for his wellbeing.

The party demanded that Besigye’s personal doctors and family be granted immediate and unrestricted access, insisting that his continued detention violates the law.

“He must be released to receive the care he deserves,” the statement added, urging supporters to remain alert and keep him in their prayers.

By press time, prison authorities had not responded to requests for comment, and the claims could not be independently verified.

Dr Besigye, a former personal doctor to President Yoweri Museveni and one of his longest-serving political challengers, has unsuccessfully contested the presidency four times.

He has been in detention for more than 350 days without trial following his arrest after being returned from Nairobi, and is facing treason-related charges.

At their last appearance before the Kampala High Court on December 30, 2025, Besigye and his co-accused, Obed Lutale and Capt Denis Oola, entered not-guilty pleas by court order after declining to plead. The case was adjourned to January 21, 2026, for scheduling.

Last year, Besigye was also reported to be critically ill after staging a hunger strike demanding justice. At the time, President Museveni dismissed the move as political pressure, arguing that prison facilities were capable of providing medical care for all inmates.

Source:The Citizen
 
Back
Top Bottom