KKKT Loliondo wasalia nje kisa hawamtaki Mchungaji aliyeletwa na Askofu

Huihui2

JF-Expert Member
Joined
Jan 5, 2012
Posts
9,818
Reaction score
14,585
Screenshot_20260803_072235_Lite.jpg

Mgogoro unaendelea katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Usharika wa Loliondo, Jimbo la Maasai Kaskazini, umeingia katika hatua mpya baada ya waumini kuendelea kufanya ibada nje ya jengo la kanisa kwa zaidi ya wiki nane, wakipinga kuondolewa kwa mchungaji wao, Hery Johannes Lukumay.

Wakati huohuo, wamemwomba Askofu Mkuu wa KKKT, Dkt. Alex Malasusa, kuingilia kati kabla mgogoro huo haujasababisha mgawanyiko mkubwa zaidi ndani ya kanisa.

Waumini hao wanadai mchungaji huyo aliondolewa katika mazingira yenye utata bila wao kushirikishwa.

Wanasema hatua hiyo imeyumbisha huduma za kiroho, kugawa waumini na kuwalazimu kuendelea kuabudu nje ya kanisa.

Pia wamesisitiza kuwa hawatarejea ndani ya jengo hilo hadi watakapopewa maelezo ya kina kuhusu sababu za kuondolewa kwa mchungaji wao.
 
Mytake:
Mimi ni Mkatoliki ila nashauri hivi:-

Acheni siasa chafu kanisani. Kuna tabia ya waumini kufanya unnecessary bonding na mtumishi fulani, kunakopelekea kusahau kuwa mchungaji ni mali ya dayosisi. Sio mali ya usharika fulani wala mtaa. Dayosisi ina mamlaka ya kumhamisha mchungaji kwenda sehemu nyingine na hakuna sheria inayowalazimisha kuwaomba waumini.

Mchungaji ni muajiriwa, ni kama tu mwalimu, mkurugenzi anaweza akamhamisha kutoka shule moja kwenda shule nyingine kwa lengo fulani. Tatizo la waumini wa siku hizi, wanakwenda kanisani kukutana na mchungaji(mtu) badala ya kukutana na Mungu.

Mungu aingilie kati muache kuishi kwa mihemko kanisani. Nimeyaona haya KKKT Usharika wa Kijitonyama, Dayosisi ya Konde na Kimara ambapo nguvu ya Mchungaji ni kubwa kuliko Askofu
 
Pale KKKT knyama Ilikuwa utata mkubwa sana kipind wamemuhamisha Rev Eliona Kimaro.

Ikabid apewe likizo. Alaf arudi.
 
View attachment 3642232
Mgogoro unaendelea katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Usharika wa Loliondo, Jimbo la Maasai Kaskazini, umeingia katika hatua mpya baada ya waumini kuendelea kufanya ibada nje ya jengo la kanisa kwa zaidi ya wiki nane, wakipinga kuondolewa kwa mchungaji wao, Hery Johannes Lukumay.

Wakati huohuo, wamemwomba Askofu Mkuu wa KKKT, Dkt. Alex Malasusa, kuingilia kati kabla mgogoro huo haujasababisha mgawanyiko mkubwa zaidi ndani ya kanisa.

Waumini hao wanadai mchungaji huyo aliondolewa katika mazingira yenye utata bila wao kushirikishwa.

Wanasema hatua hiyo imeyumbisha huduma za kiroho, kugawa waumini na kuwalazimu kuendelea kuabudu nje ya kanisa.

Pia wamesisitiza kuwa hawatarejea ndani ya jengo hilo hadi watakapopewa maelezo ya kina kuhusu sababu za kuondolewa kwa mchungaji wao.

Nasikia Wana KKKT huko Arusha, wanamlalamikia Sana huyo Askofu wao Mpya amekuwa mtu wa kuchangisha michango isiyoeleweka na wanaita eti sadaka.

Poleni Wana KKKT ARUSHA, Kuna Mwaka hela ilipigwa haswa, benki ya CRDB ikatishia kupiga mnada Hoteli yao ya Corridor Spring na Hospitali ya Selian kwa kushindwa kurejesha mkopo wa Dola za kimaremani zipatazo Milioni 9 wakati huo.

Badala ya kushughulika na Mafisadi eti wakaanzisha sadaka ya kulipa Deni la CRDB. Yaani ufisadi wafanye wao huko Dayosisi lakini Deni lilipwe na waumini. WTF

Bado tena hiyo Selian Hospital watu wananipigia tu mihela, huduma mbovu, hakuna sawa, mishahara hailipwi hadi JKCI imebidi waingilie kati kutoka Jahazi. Kwa kifupi hiyo Dayosisi ya Kaskazini Ina ufisadi Sana watu wananipigia Sana

Bado Kanisa Kuu Mjini Kati, ofisi za Dayosisi zinapojengwa, huko napo huo mradi wa ujenzi waumini wanachangishwa Kila kukicha na Pesa inayopatikana inaenda kwenye kunufaisha viongozi wa kanisa kwa ununuzi wa Magari MAPYA na ujenzi wa nyumba zao. Yaani kanisa linajengwa na wao wanajenga nyumba zao kupitia huo mradi wakishirikiana hiyo Kamati ya ujenzi.

Kuna shida sana ya ufisadi KKKT KASKAZINI...na watu wakiiba wanaishia kusema Bwana Yesu asifiwe na hakuna kuwajibishana. Huyo Askofu kapeleka kibaraka wake, waumini wamemshitukia wamegoma kumpokea lengo ni upigaji tu na waumini wameshitukia Kuna upigaji ulitaka kufanyika ndiyo maana wamemgomea kumpokea huyo Mchungaji wao Mpya

Yaani Askofu anapanga safi yake ya ulaji akishirikiana na wakuu Wa jimbo
 
Duh ! Mkuu umefunguka kinyama!! Hii inahitaji mada inayojitegemea kabisa. Yaani ufisadi kanisani hauna tofauti na wa TAMISEMI. Same criminals different platforms
 
View attachment 3642232
Mgogoro unaendelea katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Usharika wa Loliondo, Jimbo la Maasai Kaskazini, umeingia katika hatua mpya baada ya waumini kuendelea kufanya ibada nje ya jengo la kanisa kwa zaidi ya wiki nane, wakipinga kuondolewa kwa mchungaji wao, Hery Johannes Lukumay.

Wakati huohuo, wamemwomba Askofu Mkuu wa KKKT, Dkt. Alex Malasusa, kuingilia kati kabla mgogoro huo haujasababisha mgawanyiko mkubwa zaidi ndani ya kanisa.

Waumini hao wanadai mchungaji huyo aliondolewa katika mazingira yenye utata bila wao kushirikishwa.

Wanasema hatua hiyo imeyumbisha huduma za kiroho, kugawa waumini na kuwalazimu kuendelea kuabudu nje ya kanisa.

Pia wamesisitiza kuwa hawatarejea ndani ya jengo hilo hadi watakapopewa maelezo ya kina kuhusu sababu za kuondolewa kwa mchungaji wao.
Hawa jamaa huwa wana comedy sana.
 
Vita ya wachaga na wamasai hiyo

USSR
 
Hawa jamaa huwa wana comedy sana.
Hiyo ya kusali nje ya kanisa nimewahi kuishuhudia pia pale Usharika wa Kunduchi mwanzoni mwa miaka ya 2000 enzi za Askofu Jerry Mngwamba
 
Is what happen ukikaribisha insetive za wanasiasa, catholic wao walifanikiwa ku limit this
Roman Catholic kwa utawala wa Kanisa, hierachia yao ni kama Jeshi tu. Hakuna nyokonyoko wa nywinywinywi. Hutaki kwendraaa
 
Back
Top Bottom