KKKT Loliondo wasalia nje kisa hawamtaki Mchungaji aliyeletwa na Askofu

KKKT ina shida hasa suala la uongozi aseeh, niliona kule mwanza huko Arusha ndo kila kukicha wanakuja na jipya na huko kanisa hilo lilishagawanyika
 
Tatizo la makanisa yasiyo na sera sahihi (yaani yenye sera mbovu) au yasiyo na sera kabisa ... matokeo yake ni kupandikizwa itikadi za kipumbavu na machawa
 
Pale KKKT knyama Ilikuwa utata mkubwa sana kipind wamemuhamisha Rev Eliona Kimaro.

Ikabid apewe likizo. Alaf arudi.
Ila Mch Kimaro aliomba msamaha ndipo akarudishwa. Tena mbele ya Askofu malasusa kanisani. Ndipo akasamehewa na kurudishwa. Bila kuomba msamaha wangemtema mazima.
 
Ila Mch Kimaro aliomba msamaha ndipo akarudishwa. Tena mbele ya Askofu malasusa kanisani. Ndipo akasamehewa na kurudishwa. Bila kuomba msamaha wangemtema mazima.
Eeh ni sawa. Ila Sikumbuki vizur. Hivi ni yeye ndio aligoma kuondoka na akawaamrisha na waumini wamuunge mkono ?.
 
Nadhani wajisomee biblia; Mathayo 23:4 ...mstari wa 4 "Wao hufunga mizigo mizito na kuwatwika watu mabegani mwao; lakini wasitake wao wenyewe kuigusa hata kwa kidole chao"......
 
Kuna sababu mpaka CCM walimpigania sana Malasusa ashinde badala ya Bagonza. Ukiona CCM wameingia front kumpigania mtu basi shtuka - ufisadi, uchawa, majungu....
 
Aisee umenikumbusha mbali, ile hospital ya Selian pale mjini kati ukiona majengo yanavutia haswaa, siku nilipojua wafanyakazi wanalipwa mshahara tarehe 60 hadi 70 nilichoka aisee. Kwa ujumla KKKT kuna shida ya uongozi na ni janga la muda mrefu, hawa viongozi watadaiwa roho za waumini zinazopotea kwa uzembe wao.
 
Mambo ni mengi, makanisa yameingiliwa na siasa Kuna team utawala na upinzani.
 
Hao hawatakaa wawe na amani maana chimbuko la kanisa lao toka kwa Luther ni ufarakano.
Kule Dayosisi ya Konde tayari kuna mmeguko. Kumeanzishwa Kanisa la Kiluteri la Kiinjili Afrika Mashariki (KKAM)
 
Ila Mch Kimaro aliomba msamaha ndipo akarudishwa. Tena mbele ya Askofu malasusa kanisani. Ndipo akasamehewa na kurudishwa. Bila kuomba msamaha wangemtema mazima.
Hata Elionora Kimaro walimkosea kwa vile wanamuogopa. Walipaswa wamhamishie huko sweken Tandahimba ili tuone na morning glory yake ingefika wapi
 
Karatu kijiografia iko Mkoa wa Arusha, lakini KKKT ya Karatu iko chini ya Dayosisi ya Kilimanjaro. Just imagine?
Mipaka ya makanisa sio lazima ifuate mipaka ya serikali, hata kwa wakatoliki mipaka yao ya majimbo ni tofauti na mipaka ya kiserikali
 
Mipaka ya makanisa sio lazima ifuate mipaka ya serikali, hata kwa wakatoliki mipaka yao ya majimbo ni tofauti na mipaka ya kiserikali
Huwezi kufananisha overlap ya majimbo ya RC na huo mkannganyiko wa Karatu. Hebu tumia akili.

Ya RC yanapakana. Kwa mfano Jimbo la Mbeya linaishia Chimala na linaanza jimbo la Iringa/Njombe wakati mpaka uko mbele ya Igawa.

Au Jimbo la Dar es Salaam llinaishia Kibaha huku Jimbo la Morogoro likianzia Kongowe na sehemu zikizobaki hadi Moro.

Yaani majimbo ya RC yanagusana. Ila sasa Karatu unavuka wilaya za Monduli, Arumeru, Arusha, Hai ndipo uende Moshi Mjini kwa Askofu wako. This is insane, na ndiyo mambo ambayo KKKT inaendekeza na yanawatafuna
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…